Askofu Dr Bagonza: Mwongozo wa Kuhama Chama

Akili kubwa sana hii.
 
Askofu ni Bagonza tu, na siyo kila anayejiita askofu ni askofu. Wengine ni watoa hofu tu.
 
MWONGOZO WA KUHAMA CHAMA

Katika msimu wa Ligi yoyote, huwa kuna wachezaji kuhama klabu zao. Hata kwenye siasa, dini na hata ndoa, imeanza kuzoeleka watu kuhama au kuachana. Napendekeza Mwongozo wa kuhama:

1. Unapohama, tueleze uzuri wa unakokwenda, si ubaya wa unakotoka. Tayari tunajua utokako ni kubaya ndiyo maana umeondoka.

2. Tueleze uzuri na ubaya wako, si uzuri na ubaya wa watu unaoachana nao. Mapenzi yana upofu wa kudumu. Mwenye neno “MAPINDUZI” katika jina lake, anamshtaki mwenye harufu tu ya jina la “UHAINI”.

3. Jitahidi kukumbuka kuwa unayemwacha aliwahi kuwa mwema kwako (Baby) mpaka mkazaa watoto. Kwa ajili ya watoto, songa mbele kimya kimya. Usimtukane.

4. Ukiweza hamia uendako kimya kimya, tutakuona ukiwa huko. Ukitaka kurudi, rudi kimya kimya. Usipoahidi kitu hutadaiwa kitu. Lakini ukiwa na maneno mengi utamtisha mpenzi mpya.

5. KUMBUKA: Hakuna chuki ya kudumu wala mahaba ya kudumu. Mahaba ya kutongozea siyo ya mahaba ya kutunzia ndoa. Unaweza kukimbia kikwapa ukaangukia kwenye shombo.!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…