Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,242
- 34,917
Ninapenda kuwashukuru wote wanaonifuatilia katika ukurasa wangu. Wapo watu wanaouliza ni kwa nini Askofu haonekani kumtetea Rais Magufuli anapodhalilishwa mtandaoni lakini anaonekana kuwatetea zaidi viongozi wa vyama vya upinzani pamoja na makundi mengine yakiwemo ya wanaharakati na wanahabari wanaposumbuliwa na Vyombo vya Dola, watu wasiojulikana, nk?
Jibu rahisi na lililowazi ni kuwa Rais anavyo vyombo vya dola na haiwezekani vyombo vya dola vikamnyanyasa Rais! Lakini pia, endapo Rais atadhalilishwa basi vyombo vya dola vinaweza kuchukua hatua hata asipovituma!
Pia, ni vigumu kwa viongozi wengine wa CCM kunyanyaswa na vyombo vya dola kimakosa au kwa makusudi kwa sababu Serikali ya CCM ndiyo yenye vyombo vya dola. Hata hivyo, pale ilipotokea kada wa CCM amenyanyaswa na vyombo vya dola kwa makosa au kwa namna ye yote ile, Askofu hajasita kupaza sauti kama ilivyotokea kwa kada mmoja wa CCM pale Lumumba aliyewekwa ndani na Jeshi la Polisi kwa muda mrefu mwaka jana pasipo kupelekwa mahakamani!
Lakini kwa kuwa viongozi wa vyama vya upinzani na wanaharakati pamoja na waandishi wa habari ndio wanakuwa wahanga wakubwa na kwa kuwa hawana dola na hawana wa kuwasemea, basi ni lazima sauti ya Askofu ipae juu na mara kwa mara! Kama ikatokea chama cho chote cha upinzani kikashinda uchaguzi na kushika dola na CCM ikawa chama cha upinzani, basi sauti ya Askofu itaanza kuwatetea wasiokuwa na dola ikiwemo CCM kama itapoteza uchaguzi!
Sauti ya Askofu siku zote ipo kwa ajili ya wanyonge, wasio na nguvu, wasio na sauti na wanaokandamizwa (Isaya 61:1-4). Chama tawala na serikali yake haviwezi kuwa sehemu ya kundi hilo. Kamwe sauti ya Askofu haiwezi kuwa sauti ya kusifia watawala na wenye nguvu na mamlaka! Kinyume chake ni sauti ya kuonya na kukemea (Ezekieli 33:1-20).
Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
++Emmaus Bandekile Mwamakula - Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki