Jaji Mfawidhi
JF-Expert Member
- Feb 20, 2016
- 15,835
- 23,776
Anaandika Askofu EMMAUS BANDIKILE MWAMAKULA....
TUNDU LISSU YUKO SALAMA KWA KIASI GANI?
Nayaandika haya kama Askofu! Ndiyo! Askofu aliye katika Msafara wa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Tundu Lissu.
Tarehe 23 Septemba 2020, Msafara wa Tundu Lissu uliwasili Bukoba. Ulipofika Jamhuri Road katika Ofisi ya CCM, mawe yalianza kuporomoshwa kutoka katika jengo la ghorofa ambalo lina Ofisi za CCM.
Warusha mawe walivaa sare za CCM wakiwa katika Ofisi za CCM. Chini ya jengo kulikuwa na watu wazima waliokuwa wamevalia sare za CCM. Kama hiyo haikutosha, pembeni kulikuwa na Askari Polisi ambao hawakuchukua hatua zozote!
Msafara wa Mheshimiwa Lissu ulikuwa unaongozwa na Gari Polisi ambalo kwa kuwa lilikuwa mbele zaidi huenda hawakuona (huenda hawa hawana hatia).
Tukio la jana limetupa maswali mengi sana. Ikiwa mambo kama haya yanaweza kufanywa mchana kweupe na watu wanaojulikana mbele ya macho ya Askari Polisi, iweje wakati wa usiku?
Hivi OCD wa Bukoba na RPC wa Kagera wamelichukuliaje tukio hilo? Wale Askari Polisi waliokuwa wanawatazama CCM wakimrushia mawe Lissu walikwenda kutoa ulinzi ili CCM watimize zoezi lile? Uongozi wa CCM Wilaya, Mkoa na Taifa, unalichukuliaje jambo hili?
Mawe yale yaliyokuwa yakilenga kichwa cha Lissu aliyekuwa akiwapungia mikono watu akiwa amesimama yaliishia katika mikono ya Wasaidizi wake waliokuwa wakipangua mawe yale.
Mimi kama Askofu, ninawatahadharisha Jeshi la Polisi na vyombo vya dola kwa ujumla kuongeza umakini na uwajibikaji katika eneo la ulinzi wa Wagombea wote wa Urais akiwemo Lissu.
Ninawaomba CCM walichunguze tukio la Bukoba na wachukue hatua na kuhakikisha kuwa Ofisi zao hazihifadhi watu wa vurugu.
Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Mkuu - Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki