GE2025 Askofu Fernandes amwambia Samia wakati akiapishwa: Taifa limegawanyika na Mioyo ya Watu imejeruhiwa

GE2025 Askofu Fernandes amwambia Samia wakati akiapishwa: Taifa limegawanyika na Mioyo ya Watu imejeruhiwa

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Mwenyekiti mpya wa Umoja wa Maaskofu wa Makanisa ya Kipentekoste (CPCT) Askofu Vernon Fernandes wakati wa kuapishwa Samia huko Dodoma amesema; "Umepokea jukumu kubwa la kihistoria, Mhe. Rais Taifa limegawanyika na Mioyo ya Watu imejeruhiwa kwa namna mbalimbali, ombi langu kwako kwa niaba ya umma wa watanzania ulilete Taifa pamoja kuiponya Mioyo hii, hili likiwa kipaumbele chako"

 
Hivi hawa vijana madai yao ni nini.

Wamemwambia nani na hawakuwahi kusikilizwa.

Haiwezekani kuendelea kulea ujinga wa watu wachache na kuacha wengi waumie.

Waseme wanataka nini waambiwe kama wanachokihitaji kinawezekana au la.

Maana sio lazima kila unachokitaka ukipate. Maisha hayapo hivyo.
 
Back
Top Bottom