Askofu Gwajima afanya mkutano wa Injili Kongwa, wengi wahudhuria mapepo yalipuka

Askofu Gwajima ambaye pia ni mbunge wa Kawe jana alifanya mkutano mkubwa katika jimbo la Spika mstaafu mzee Ndugai katika kata ya Kibaigwa.

Maelfu ya wana Kongwa walihudhuria na kupokea uponyaji ikiwemo kutolewa majini na mashetani pia.

Mungu wa mbinguni awabariki sana!
Sijaelewa. Alienda kama mchungaji ama kama mbunge?
 
Mkuu umeandika kishabiki sana,nimefungua uzi haraka sana na kujiuliza kwanini anaenda kufanya mkutano huko
 
Gwajima ni mfanyabiashara na siku zote hutafuta fursa na kuitumia, dini ndio mtaji wake. Jiulize kwanini siku zote hajawahi kwenda Kongwa ila baada ya yalitokea kwa Ndugai (ikiwa tayari pia alishatumia fursa ya kujifanya anamuonya Ndugai sababu ya hitilafu yao) ndio kaamua kwenda huko; akiwa na hakika ya kupata wafuasi wakumsikiliza.
Sijasikia alichohubiri ila nina hakika asilimia 98 ilikuwa ni vijembe kwa Ndugai na asilimia 2 ndio ilikuwa masuala ya dini.
 
Na hizo 2% ni za kuhimiza na kuhamasisha michango
 
Kwahio yupo kwenye shughuli za Kibunge ?

Au Ubunge ni Part Time....
 
Hakuna aliyewahi cheza na Gwajima akabakia salama. Alimfuta makonda kwenye ulimwengu wa roho akaliwa kichwa na wajumbe. Huku mahakama ikimtafuta
 
Jobo hakuudhuria Kwa Nini jaman? Yani aise jobo alitakiwa kuombewa Ili Pepo litokeeeee la kumfokea Raisi Samia eti ni mwanamke akae kikike
 
Askofu Gwajima ambaye pia ni mbunge wa Kawe jana alifanya mkutano mkubwa katika jimbo la Spika mstaafu mzee Ndugai katika kata ya Kibaigwa.

Maelfu ya wana Kongwa walihudhuria na kupokea uponyaji ikiwemo kutolewa majini na mashetani pia.

Mungu wa mbinguni awabariki sana!
Yani ameamua kumfata Ndugai mpaka jimboni kwake 😃😃😃
 
Back
Top Bottom