Askofu Gwajima alikataa kutumia kiti alichoandaliwa kukwepa mtego au ndio hofu tu ilimjaa?

Askofu Gwajima alikataa kutumia kiti alichoandaliwa kukwepa mtego au ndio hofu tu ilimjaa?

MWALLA

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2006
Posts
16,952
Reaction score
10,500
Nimejaribu kujjifikirisha kuhusu hili la Askofu Gwajima kukwepa kutumia kiti alichoandaliwa na pia kukataa kutumia microphone katika kikao alichoitwa hapo mjini Dodoma kuhusiana na suala la chanjo ya Corona.

Je, kuna hisia gani zilimpata bwa Gwajima mpaka kufikia kufanya tofauti na alivyopangiwa ikiwemo kukataa kukalia kiti pia na kukataa kutumia kipaza sauti.

Je, alihisi amewekewa yale mambo yetu? au aliwekewa sumu? Au vipi?

Hii imenikumbusha kitimoto kilee alichowekewa Marehemu Kolimba matokeo yake akayeyuka. Hii inanifikirisha kuwa hawa CCM hii mambo za kupotezana kwa style hii ndio njia wanayoitumia sana hawa CCM katika kuwamaliza wale wanaojaribu kuwatunishia kifua kama alivyofanya Kolimba kipindi hicho na wengineo wengi na sasa ni Gwajima nae amejaribu.

Ila kwa sasa Gwajima amestuka mapema kwa kumbukizi zao za matukio ya nyuma kuwa ukiitwa kwenye kiti moto cha hawa wajuba wanakuwa na mengi ya kukufanyia ikiwemo hata kukudhuru.

Ni hisia tu au inawezekana ni kweli? Je, Gwajima amekwepa mtego au ndio hofu tu ilimjaa?

 
Imekaa kiigizo igizo maana unakataa kiti na mike halafu unawaomba hao hao uliowakatalia wakupe nyingine.
 
USHAURI TU KWA CCM huu mtindo nadhani wangeuacha kutokana umepitwa na wakati halafu katika zama hizi za teknolojia ni rahisi kuumbuka tofauti na zamani.
 
Imekaa kiigizo igizo maana unakataa kiti na mike halafu unawaomba hao hao uliowakatalia wakupe nyingine.
Yuko sawa maana kuchagua mic nyengine ni bora inakuwa haina madhara ni salama. ile kama iliwekewa mtego ni ile na ukistukia hawawezi kutengeneza nyingine kwa wakati huohuo.
 
Anajiona kidume sasa woga wote wa nini. Huo ulikuwa woga wake tu kwani mwenyewe anajua aweza hata bambikiwa tu na akapewa jina baya.
 
Ni ujinga tu ulee bosi. Zipo njia nyingi sana za kutoa roho mwanadamu hasa ambaye hana ulinzi wa dola na anachangamana kwenye jamii. Thanks to God watanzania ni waungwana na hawana tabia hiyo kwa saaaana.

Gwajima yeye kila siku anajinadi ni mtumishi wa kweli na ana imani kiasi cha kutoiogopa hata Corona maana ni shetani....imekuaje tena aogope kiti na mic huku yeye anaroho mtakatifu anamlinda aka ulinzi wa kiroho.
 
Anajiona kidume sasa woga wote wa nini.Huo ulikuwa woga wake tu kwani mwenyewe anajua aweza hata bambikiwa tu na akapewa jobs baya.
Huwezi kujua huenda leo tungeongea mengine. Je, ungeweza kusema haya unayoyasema?
 
R I P zingekuwa nyingi tu humu JF
 
ni ujinga tu ulee bosi... Zipo njia nyingi sana za kutoa roho mwanadamu hasa ambaye hana ulinzi wa dola na anachangamana kwenye jamii...thanks to God watanzania ni waungwana na hawana tabia hiyo kwa saaaana..

Gwajima yeye kila siku anajinadi ni mtumishi wa kweli na ana imani kiasi cha kutoiogopa hata Corona maana ni shetani....imekuaje tena aogope kiti na mic huku yeye anaroho mtakatifu anamlinda aka ulinzi wa kiroho....
Unachuki za kijinga mno mkuu!
 
Unachuki za kijinga mno mkuu!

sijui hapo chuki iko wapi....au tafsiri ya neno "chuki" mimi au wewe mmoja wetu halifahamu vizuri..

Binafsi nimezungumza kulingana na matendo na matukio ya Gwajima...siwezi kumchukia Gwajima kwa lolote chief ila tu sipendezwi na matendo yake mfano, alituahidi kumfufua Amina chifupa hakumfufu, anapotosha watu juu ya chanjo ilihali sio mtaalam wa Afya....nk ila Gwajima in personal sina chuki naye kama ambavyo sina chuki na mwanadamu yeyote yule duniani..
 
Back
Top Bottom