- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Wakuu wa JamiiCheck huku kimewaka tunaomba uhalisia wa taarifa hii.
- Tunachokijua
- Josephat Gwajima ni Askofu na mwanzilishi wa kanisa la 'Glory of Christ Tanzania Church' GCTC (Ufufuo na Uzima Ministries), kadhalika ni mwanasiasa ambaye mwaka 2020 alichaguliwa kuwa mbunge wa jimbo la Kawe kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi CCM.
Taarifa inayosambazwa mtandao wa Facebook ikimhusisha Askofu Gwajima
Baadhi ya watumiaji wa mtandao wa Facebook wamechapisha taarifa inayonukuu andiko linalodaiwa kuchapishwa na Askofu Gwajima kupitia ukurasa wake mtandao wa Instagram kuwa amesema 'Kawe tusiunge mkono wasaliti' ambapo grafiki zenye utambulisho wa Millard Ayo na Mwananchi zikitumika kusambaza taarifa hiyo.
Je, ni upi uhalisia wa taarifa hiyo?
Ufuatiliaji wa Kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia utafutaji wa maneno muhimu umejiridhisha kuwa andiko lililonukuliwa katika taarifa hiyo si la kweli ni la kutengenezwa na wapotoshaji kwani halikuchapishwa na Askofu Gwajima kwenye ukurasa wake wa Instagram.
Vilevile grafiki zilizotumika kusambaza taarifa hiyo si za kweli, ni za kutengenezwa na wapotoshaji kwani vyombo hivyo (Mwananchi, Millard Ayo) havikuchapisha taarifa hiyo, bali wapotoshaji walitumia utambulisho huo ili kusambaza taarifa potoshi.
Kumbuka wapotoshaji wanaweza kutengeneza chapisho kwa kutumia utambulisho wa watu maarufu au vyanzo vya taarifa vya kuaminika ili kusambaza taarifa zisizo za kweli, hivyo ni muhimu kujenga utaratibu wa kuhakiki taarifa kila unapokutana nayo iwe mtandaoni ama nje ya mtandao.