PreGE2025 Askofu Gwajima amefikiwa, Maria Sebastian achukua fomu ya kumrithi Kawe

PreGE2025 Askofu Gwajima amefikiwa, Maria Sebastian achukua fomu ya kumrithi Kawe

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Mwenyekiti wa Uchumi, Uwezeshaji na Fedha katika Kamati ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa, Maria Alphonce Sebastian, amejitokeza kuchukua fomu ya kuwania Ubunge wa Jimbo la Kawe kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, 2025.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuchukua fomu katika Ofisi za CCM Mkwajuni, Wilaya ya Kinondoni, Maria amesema amejipanga kikamilifu na anaamini huu ni wakati mwafaka wa kuwatumikia wananchi wa Kawe na Taifa kwa ujumla.

Maria, ambaye ana historia ya kushika nafasi mbalimbali ndani ya chama na serikali, amesema anajitosa kwenye kinyang'anyiro hicho akiwa na uzoefu mkubwa na uthubutu unaotokana na ushindani aliowahi kukutana nao katika nafasi alizogombea, ikiwemo Ujumbe wa Mkutano Mkuu wa Mkoa, Wilaya ya Kigamboni, Mkutano Mkuu wa Taifa, na Ubunge wa Afrika Mashariki (EALA).

Ameeleza kuwa uamuzi wake wa kugombea unatokana na imani kwamba Jimbo la Kawe linahitaji kiongozi mwanamke mwenye uthubutu, dira ya maendeleo na maono ya kijumuishi kwa wananchi wa jinsia zote.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Aidha, amempongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwa kielelezo cha uongozi bora wa mwanamke na kuhimiza usawa wa kijinsia kupitia sera ya uongozi wa 50 kwa 50 katika nafasi za kisiasa na za kiutendaji.

Jimbo la Kawe lilikuwa linawakilishwa bungeni na Askofu Josephat Gwajima WA Kanisa la Ufufuo na Uzima.

 
Ujana wa wana CCM unaishia miaka mingapi,, anayejua hili atwambie.
 
Mwenyekiti wa Uchumi, Uwezeshaji na Fedha Kamati ya Jumuiya ya vijana ya Chama Cha Mapinduzi CCM Taifa (UVCCM), Maria Sebastian amechukua fomu ya kugombea nafasi ya ubunge jimbo la Kawe.

Maria amekabidhiwa fomu hiyo leo Jumapili Juni 29, 2025, na Katibu wa Vijana CCM Wilaya, Amos Richard.

mbeyaubung.png
 
Back
Top Bottom