tpaul
JF-Expert Member
- Feb 3, 2008
- 24,225
- 22,632
Mnamo tarehe 29/08/2020 Askofu Josephat Gwajima aliwaeleza waumini wake kuwa ana ‘kitu’ ndani yake kilichomuambia asikalie kiti na kutumia kipaza sauti alichokuwa amepangiwa na mwenyekiti wa kamati ya wa Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge.
Kwa tafsiri nyingine ni kuwa Kamati ya Bunge walipanga kumuua kwa kumuwekea 'misumari' kwenye kiti na kipaza sauti lakini akaokolewa na 'kitu' kilichopo ndani ya mwili wake. Askofu huyo ameyasema hayo leo wakati akiwahubiria neno la Mungu waumini wake kwenye kanisa la Ufufuo na Uzima. Hebu msikilize mwenyewe hapo chini:
Maoni yangu
Namshangaa sana askofu kwa kuwatuhumu kamati ya Bunge bila ushahidi wowote wa kiukweli au kimazingira. Hivi kweli serikali ikitaka kumuua mtu itashindwa? Mbona wengi na hawakuweza kufua dafu? Tuache kuipakazia serikali mambo ya ajabu. Tuiache serikali ifanye kazi yake bila kuingiliwa na mtu yeyote.