GE2025 Askofu Gwajima Aonya na Kutoa Ushauri, Kufanyike Nini Haraka Kabla Ya Uchaguzi

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Hamatan

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2020
Posts
7,840
Reaction score
18,115
USHAURI
Gwajima amesema kuwa ameshauri mara nyingi, na anashauri tena.
Askofu Gwajima amesema kwamba nchi imegawanyika sana, na mtu yeyote mwenye akili timamu hawezi kukubali kwenda kwenye uchaguzi nchi ikiwa kama hivi ilivyo.

Akisistiza umuhimu wa watawala kusikiliza ushauri wa wananchi, alinukuu kitabu cha Mithali, akasema kuwa hiki ni kitabu kinachokubalika na wote, wakristo na waislam, akasema:

Mithali 29:1​

Aonywaye mara nyingi akishupaza shingo, Atavunjika ghafla, wala hapati dawa.
Gwajima akasema kuwa anawashauri watawala wafanye damage control haraka kabla ya uchaguzi, lakini tusikubali kwenda kwenye uchaguzi katika hali hii.

Amesema kuwa mambo yafuatayo, yameleta mgawanyiko mkubwa kiasi cha watu kuichukia CCM, na kuuona uchaguzi hauna maana:.
1. KUMWEKA LISU GEREZANI.
Amesema kuwa Lisu ni mtu asiye wa kawaida, alipigwa risasi 16, lakini bado anaishi, na yupo anaendelea kupigania haki kupitia siasa. Kwanza kwa kupigwa risasi zote zile, bado watu hawaoni kuwa huyu siyo mtu wa kawaida? Huwezi kusema ni nguvu yake, Mungu kamweka kwa kusudi maalum. Halafu unamweka ndani mtu huyu bila kosa lolote. Akasema kuwa Lisu anaonewa huruma na watanzania wengi, hata wanaCCM, siyo wanaCHADEMA pekee yao. Hivi unadhani watu hawa wanaomwonea huruma Lisu kwa sababu anaonewa, wataenda kuoiga kura?

2. KUVAMIWA NA KUJERUHIWA KWA PADRE KITIMA.
Akasema kuwa Kanisa Katoliki lina maaskofu, mapadre na waumini. Lakini Kanisa Katoliki ni Baba na mlezi wa wakristo wote kwa sababu makanisa yote yametokana na Kanisa Katoliki. Mwanzilishi wa Kanisa la Lutheran alikuwa Padre wa Kanjsa Katoliki, Mfalme Henry aliyeanzisha Kanusa la Anglikana alikuwa askofu wa Kanisa Katoliki, na vivyo hivyo kwa makanisa yote, waanzilshi wao walitokana na Kanisa Katoliki, directly au indirectly. Wakristo wote msingi wa imani yao ni mmoja kuwa Yesu Kristo alizaliwa kwa nguvu ya Roho Mtakatifu, Akateswa, akafa, akazikwa, akafufuka, akapaa mbinguni, atarudi tena kuwahukumu wazima na wafu. Unamvamia na kumshambulia Padre wao kwa sababu anakemea uuzwaji wa bandari, hivi unadhani wakatoliki, wanaopenda haki, na wakristo wanaoamini katika umoja wa Kristo, wataenda kuoiga kura huku kiongozi wao anavamiwa na kujeruhiwa, na hakuna anayeadhibiwa?

3. KUWAZUIA WAUMINI WA MAKANISA YA UFUFUO NA UZIMA KUFANYA IBADA
Askofu Gwajima anasema kuwa makanisa ya ufufuo na uzima, yapo zaidi ya elfu 2 nchi nzima, waumini wasiopungua milioni 2, wachungaji pamoja na familia zao wasiopungua elfu 8, wamezuiwa kuabudu, wanasumbuliwa, wanapigwa. Akauliza, hivi tunategemea hawa wataenda kupiga kura?

4. WALIOTEKWA, WALIOUAWA NA WALIOPOTEZWA NA KUUMIZWA
Askofu Gwajima amesema kuwa sote tunajua kuwa kuna watanzania wenzetu, wametekwa, wameuawa, na wengine kupotezwa. Akauliza, hivi wanafamilia, ndugu, marafiki na watanzania wote wanaochukia uovu huu wa kuteka na kuua wanaokosoa, tunatarajia wataenda kupiga kura? Lazima waliotrkwa na kupotezwa watafutwe, kama ni hai au wameuawa, lazima waoatikane.

Akamalizia kwa kusema kuwa yeye hataacha kamwe kuwa sauti ya wanaonewa na kudhulumiwa.

Soma pia PreGE2025 - Askofu Gwajima: Utekaji si utamaduni wetu na halitakiwi kuchekewa!
 
Nimefanikiwa kuwashawishi wazazi wangu mwaka huu wasiende kupiga kura
Kwa kweli kama mambo yatabakia kama yalivyo sasa, utakuwa ni mwendawazimu kwenda kwenye vituo vinavyoitwa vya kupigia kura, wakati wahuni wamekwishafanya maamuzi tayari, na hawategemei kura ya mtu yeyote. Sana sana unaenda tu kuthibitisha na kujiunganisha na mashetani kuwa nawe ni miongoni au muungaji mkono wa dhuluma dhidi ya watanganyika, na kwamba unaunga mkono utekaji na mauaji ya watu wasio na hatia, na hivyo upo tayari kulaanika pamoja na wauaji.
 
twende tu tukija kushtuka kila mtu analia....sisi ni taifa moja waonywao wajirekebishe waonyao wasamehe pia
Tatizo shetani ameishikilia akili na mioyo yao, ndiyo maana wametamka wazi kuwa wao ni vyura viziwi, yaani hata mseme na kushauri vipi, hawashtuki wala hawatabadilika kamwe.
 
Sisi watanzania Wakristu kwa waislamu na hata wale wasio na dini hatuwezi kugawanywa kwa misingi ya chuki za kidini inayo chochewa na watu hao ambao nia yao ni kuvuruga amani, utulivu na maelewano miongoni mwetu, ambayo yamedumu kwa karne nyingi.
 
Kwani ni nani anachochea chuki za kidini? Kuna muislam anamchukia mkristo, au mkristo anayemchukia muislam kwa sababu ya uislam wake?

Tatizo kubwa ni kwamba tuna watawala mashetani, hawajali wewe ni mkristo au muislam, alimradi ni msema ukweli na unaweza kuwakosoa, wanakuteka, wanakuua au kukushambulia. Walimwua Kibao, muislam, wamemwua Mdude, Soka, sijui ni wa dini gani, wamemshambulia Padri Kitima, siyo kwa sababu ni mkristo, bali kwa sababu alikemea uovu wao; wamemfunga Lisu siyo kwa sababu ya dini yake, bali kwa sababu alikemea ufisadi wa Roster na Abdlu kupitia uchimbaji makaa ya mawe, huko Mbinga.

Hakuna suala la chuki za kidini bali ni dhamira chafu ya watawala dhidi ya kila anayetamka haki.
 
Machawa watakuwa wanausoma kwa mbali
 
USHAURI
Gwajima amesema kuwa ameshauri mara nyingi, na anashauri tena.
Askofu Gwajima amesema kwamba nchi imegawanyika sana, na mtu yeyote mwenye akili timamu hawezi kukubali kwenda kwenye uchaguzi nchi ikiwa kama hivi ilivyo.

Akisistiza umuhimu wa watawala kusikiliza ushauri wa wananchi, alinukuu kitabu cha Mithali, akasema kuwa hiki ni kitabu kinachokubalika na wote, wakristo na waislam, akasema:

Mithali 29:1​

Aonywaye mara nyingi akishupaza shingo, Atavunjika ghafla, wala hapati dawa.
Gwajima akasema kuwa anawashauri watawala wafanye damage control haraka kabla ya uchaguzi, lakini tusikubali kwenda kwenye uchaguzi katika hali hii.

Amesema kuwa mambo yafuatayo, yameleta mgawanyiko mkubwa kiasi cha watu kuichukia CCM, na kuuona uchaguzi hauna maana:.
1. KUMWEKA LISU GEREZANI.
Amesema kuwa Lisu ni mtu asiye wa kawaida, alipigwa risasi 16, lakini bado anaishi, na yupo anaendelea kupigania haki kupitia siasa. Kwanza kwa kupigwa risasi zote zile, bado watu hawaoni kuwa huyu siyo mtu wa kawaida? Huwezi kusema ni nguvu yake, Mungu kamweka kwa kusudi maalum. Halafu unamweka ndani mtu huyu bila kosa lolote. Akasema kuwa Lisu anaonewa huruma na watanzania wengi, hata wanaCCM, siyo wanaCHADEMA pekee yao. Hivi unadhani watu hawa wanaomwonea huruma Lisu kwa sababu anaonewa, wataenda kuoiga kura?

2. KUVAMIWA NA KUJERUHIWA KWA PADRE KITIMA.
Akasema kuwa Kanisa Katoliki lina maaskofu, mapadre na waumini. Lakini Kanisa Katoliki ni Baba na mlezi wa wakristo wote kwa sababu makanisa yote yametokana na Kanisa Katoliki. Mwanzilishi wa Kanisa la Lutheran alikuwa Padre wa Kanjsa Katoliki, Mfalme Henry aliyeanzisha Kanusa la Anglikana alikuwa askofu wa Kanisa Katoliki, na vivyo hivyo kwa makanisa yote, waanzilshi wao walitokana na Kanisa Katoliki, directly au indirectly. Wakristo wote msingi wa imani yao ni mmoja kuwa Yesu Kristo alizaliwa kwa nguvu ya Roho Mtakatifu, Akateswa, akafa, akazikwa, akafufuka, akapaa mbinguni, atarudi tena kuwahukumu wazima na wafu. Unamvamia na kumshambulia Padre wao kwa sababu anakemea uuzwaji wa bandari, hivi unadhani wakatoliki, wanaopenda haki, na wakristo wanaoamini katika umoja wa Kristo, wataenda kuoiga kura huku kiongozi wao anavamiwa na kujeruhiwa, na hakuna anayeadhibiwa?

3. KUWAZUIA WAUMINI WA MAKANISA YA UFUFUO NA UZIMA KUFANYA IBADA
Askofu Gwajima anasema kuwa makanisa ya ufufuo na uzima, yapo zaidi ya elfu 2 nchi nzima, waumini wasiopungua milioni 2, wachungaji pamoja na familia zao wasiopungua elfu 8, wamezuiwa kuabudu, wanasumbuliwa, wanapigwa. Akauliza, hivi tunategemea hawa wataenda kupiga kura?

4. WALIOTEKWA, WALIOUAWA NA WALIOPOTEZWA NA KUUMIZWA
Askofu Gwajima amesema kuwa sote tunajua kuwa kuna watanzania wenzetu, wametekwa, wameuawa, na wengine kupotezwa. Akauliza, hivi wanafamilia, ndugu, marafiki na watanzania wote wanaochukia uovu huu wa kuteka na kuua wanaokosoa, tunatarajia wataenda kupiga kura? Lazima waliotrkwa na kupotezwa watafutwe, kama ni hai au wameuawa, lazima waoatikane.

Akamalizia kwa kusema kuwa yeye hataacha kamwe kuwa sauti ya wanaonewa na kudhulumiwa.
Hata kama humpendi Gwajibo bado ni ngumu sana kutozupenda Hoja zake
 
Kwa kweli kama mambo yatabakia kama yalivyo sasa, utakuwa ni mwendawazimu kwenda kwenye vituo vinavyoitwa vya kupigia kura, wakati wahuni wamekwishafanya maamuzi tayari, na hawategemei kura ya mtu yeyote. Sana sana unaenda tu kuthibitisha na kujiunganisha na mashetani kuwa nawe ni miongoni au muungaji mkono wa dhuluma dhidi ya watanganyika, na kwamba unaunga mkono utekaji na mauaji ya watu wasio na hatia, na hivyo upo tayari kulaanika pamoja na wauaji.
Aisee, nikae kimya
 
USHAURI
Gwajima amesema kuwa ameshauri mara nyingi, na anashauri tena.
Askofu Gwajima amesema kwamba nchi imegawanyika sana, na mtu yeyote mwenye akili timamu hawezi kukubali kwenda kwenye uchaguzi nchi ikiwa kama hivi ilivyo.

Akisistiza umuhimu wa watawala kusikiliza ushauri wa wananchi, alinukuu kitabu cha Mithali, akasema kuwa hiki ni kitabu kinachokubalika na wote, wakristo na waislam, akasema:

Mithali 29:1​

Aonywaye mara nyingi akishupaza shingo, Atavunjika ghafla, wala hapati dawa.
Gwajima akasema kuwa anawashauri watawala wafanye damage control haraka kabla ya uchaguzi, lakini tusikubali kwenda kwenye uchaguzi katika hali hii.

Amesema kuwa mambo yafuatayo, yameleta mgawanyiko mkubwa kiasi cha watu kuichukia CCM, na kuuona uchaguzi hauna maana:.
1. KUMWEKA LISU GEREZANI.
Amesema kuwa Lisu ni mtu asiye wa kawaida, alipigwa risasi 16, lakini bado anaishi, na yupo anaendelea kupigania haki kupitia siasa. Kwanza kwa kupigwa risasi zote zile, bado watu hawaoni kuwa huyu siyo mtu wa kawaida? Huwezi kusema ni nguvu yake, Mungu kamweka kwa kusudi maalum. Halafu unamweka ndani mtu huyu bila kosa lolote. Akasema kuwa Lisu anaonewa huruma na watanzania wengi, hata wanaCCM, siyo wanaCHADEMA pekee yao. Hivi unadhani watu hawa wanaomwonea huruma Lisu kwa sababu anaonewa, wataenda kuoiga kura?

2. KUVAMIWA NA KUJERUHIWA KWA PADRE KITIMA.
Akasema kuwa Kanisa Katoliki lina maaskofu, mapadre na waumini. Lakini Kanisa Katoliki ni Baba na mlezi wa wakristo wote kwa sababu makanisa yote yametokana na Kanisa Katoliki. Mwanzilishi wa Kanisa la Lutheran alikuwa Padre wa Kanjsa Katoliki, Mfalme Henry aliyeanzisha Kanusa la Anglikana alikuwa askofu wa Kanisa Katoliki, na vivyo hivyo kwa makanisa yote, waanzilshi wao walitokana na Kanisa Katoliki, directly au indirectly. Wakristo wote msingi wa imani yao ni mmoja kuwa Yesu Kristo alizaliwa kwa nguvu ya Roho Mtakatifu, Akateswa, akafa, akazikwa, akafufuka, akapaa mbinguni, atarudi tena kuwahukumu wazima na wafu. Unamvamia na kumshambulia Padre wao kwa sababu anakemea uuzwaji wa bandari, hivi unadhani wakatoliki, wanaopenda haki, na wakristo wanaoamini katika umoja wa Kristo, wataenda kuoiga kura huku kiongozi wao anavamiwa na kujeruhiwa, na hakuna anayeadhibiwa?

3. KUWAZUIA WAUMINI WA MAKANISA YA UFUFUO NA UZIMA KUFANYA IBADA
Askofu Gwajima anasema kuwa makanisa ya ufufuo na uzima, yapo zaidi ya elfu 2 nchi nzima, waumini wasiopungua milioni 2, wachungaji pamoja na familia zao wasiopungua elfu 8, wamezuiwa kuabudu, wanasumbuliwa, wanapigwa. Akauliza, hivi tunategemea hawa wataenda kupiga kura?

4. WALIOTEKWA, WALIOUAWA NA WALIOPOTEZWA NA KUUMIZWA
Askofu Gwajima amesema kuwa sote tunajua kuwa kuna watanzania wenzetu, wametekwa, wameuawa, na wengine kupotezwa. Akauliza, hivi wanafamilia, ndugu, marafiki na watanzania wote wanaochukia uovu huu wa kuteka na kuua wanaokosoa, tunatarajia wataenda kupiga kura? Lazima waliotrkwa na kupotezwa watafutwe, kama ni hai au wameuawa, lazima waoatikane.

Akamalizia kwa kusema kuwa yeye hataacha kamwe kuwa sauti ya wanaonewa na kudhulumiwa.

Siyo Siri hata kidogo, Chuki ni kubwa sana kupita kiasi katika Nchi hii kwa sasa.

Vyanzo vikuu vya kuwepo kwa Chuki kubwa imetamalaki:-

1. Utekaji Watu, Utesaji, uporaji, kubambikia Watu Kesi za uongo, Mauaji ya makusudi ya raia wema.

2. Siasa chafu Sana za majitaka.

3. Ufisadi, Rushwa, upendeleo,

4. Waovu na Wahalifu kuiteka nchi (State Capture) n.k
 
Eti Askofu Gwajima anatoa ushauri namna ya kuongoza nchi, yaani Serikali iwe yakusikiliza kila mtu anachowaza, hapana aisee.
Ukimsikiliza Gwajima maana yake unapaswa kutusikiliza hata masela ya Tandika.

Nafikiri kuna mahala tulitereza na kila mtu kuona ana uwezo wa kuwa sehemu ya dola.

ndani ya mitaa ya Benghazi -Libya.
 
Hata kama humpendi Gwajibo bado ni ngumu sana kutozupenda Hoja zake

Makosa ya baadhi ya watu wanayoyafanya, ni kuangalia hoja imtolewa na nani badala kuangalia content ya hoja.
 
Eti Askofu Gwajima anatoa ushauri namna ya kuongoza nchi, yaani Serikali iwe yakusikiliza kila mtu anachowaza, hapana aisee.
Ukimsikiliza Gwajima maana yake unapaswa kutusikiliza hata masela ya Tandika.

Nafikiri kuna mahala tulitereza na kila mtu kuona ana uwezo wa kuwa sehemu ya dola.

ndani ya mitaa ya Benghazi -Libya.

Hupo sahihi hata kidogo. Yaani unataka ushauri usipokelewe kwa sababu umetolewa na mtu fulani? Rudi kwenye hekima, ushauri unapokelewa au kutopokelewa kwa kuzingatia mantiki ya ushauri, siyo umetolewa na mtu gani!

Ungekuwa na weledi, japo kidogo, ungeyajadili matatizo aliyoyatamka Gwajima, kama yapo au hayapo, kisha ungeenda kwenye ushauri wake, na kuangalia kwa umakini kama huo ushauri unaweza kutatua matatizo aliyoyataja.
 
Back
Top Bottom