The Palm Beach
JF-Expert Member
- Dec 30, 2015
- 4,249
- 11,592
View: https://youtu.be/bcL6AEYmMXA?si=u4EQo7Wo1DtZr7c7
Kwa ufupi kabisa Askofu Gwajima anasema:
👉 DC Albert Msando anatuita twende ofisini kwake kufanya nini wakati aliyeandika barua ya kufunga kanisa ni Msajili wa vyama vya kiraia...?
👉Na je, Ina maana huyu DC Msando hajui kuwa kuna kesi mahakamani kuhusu mgogoro huu na kanisa letu...?
👉Anachofanya DC wa Ubungo Albert Msando ni brainwashing na sisi hatuko tayari kuwa brainwashed...
👉Kama ameagizwa kutoa tamko la kufungua kanisa, basi wala hahitaji kutuita twende ofisini kwake, bali kinachotakiwa kufanyika ni yule aliyeandika barua ya kufunga kanisa kiharamia kuandika barua nyingine na kulifungulia kanisa...
👉 DC Albert Msando ni wa kuhurumia tu maana hana lolote analoweza kufanya kwa suala hili...
Anamalizia kwa kusema kuwa, nina mengi sana ya kusema. Lakini mimi ni kiongozi na ni mwanachama wa CCM. Mfano, kuvunjwa kwa kanisa la Kanisa la Kiinjili la KKWT kwa madai kuwa limejengwa kwenye hifadhi ya barabara ya TANROAD ni uongo mtupu kwani jirani na kanisa na lilipokuwa kanisa lililobomolewa kuna misikiti ya waislamu na haijibughudhiwa kwa vyovyote.
Kwa hiyo kama kiongozi nakuwa na tahadhari kidogo ktk kuongea kwangu ili nisije nikaongea mambo ambayo yanaweza kuivuruga kabisa CCM. Hata ikibidi kuongea basi, nitafanya hivyo kwa wakati uonaofaa..
Kama hawataki mgogoro na kufanya mambo kuwa mabaya zaidi, wana jambo moja dogo tu la kufanya - kufungulia kanisa ili watu waendelee kuabudu Mungu wao kwa uhuru na bila usumbufu au kuumiza watu basi...