SI KWELI PreGE2025 Askofu Gwajima asema Padri Kitima alipigwa na vijana wa CHADEMA

SI KWELI PreGE2025 Askofu Gwajima asema Padri Kitima alipigwa na vijana wa CHADEMA

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Source #1
View Source #1
photo_2025-05-26_08-16-51.jpg
 
Tunachokijua
Josephat Gwajima ni Askofu na mwanzilishi wa kanisa la 'Glory of Christ Tanzania Church' GCTC (Ufufuo na Uzima Ministries), kadhalika ni mwanasiasa ambaye mwaka 2020 alichaguliwa kuwa mbunge wa jimbo la Kawe kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi CCM.

Tarehe 24 Mei, 2025 Gwajima alifanya mkutano na waandishi wa habari ambapo alisema kumekuwa na mlolongo wa matukio ya watu kutekwa pamoja na kupotea hivyo kutokana na hayo, ameamua kuitisha mkutano na waandishi wa habari kuongelea kuhusu suala hilo na kisha kutoa ushauri wake.

Katika mtandao wa X imechapishwa taarifa iliyotumia utambulisho wa Jambo TV kuwa kutokana na mkutano huo Gwajima alisema Padri Kitima alipigwa na vijana wa CHADEMA, na vyombo vya usalama vinajua.


Je, ni uhalisia wa taarifa hiyo?
Kupitia ufuatiliaji wa kimtandao kwa kutumia utafutaji wa maneno muhimu (Key Word Search) pamoja na marejeo ya video ya mkutano huo, JamiiCheck imejiridhisha kuwa taarifa hiyo si ya kweli.

Chapisho lililotumika kusambaza taarifa hiyo si la kweli, bali ni la kutengenezwa kwani halijachapishwa na Jambo TV kupitia kurasa zake rasmi za mitandao ya kijamii.

Aidha kupitia mkutano wake na waandishi wa Habari Gwajima hakutoa kauli yoyote iliyowajata vijana wa CHADEMA kuhusika na tukio la kushambulishwa kwa Padri Dkt. Charles Kitima bali alitoa ushauri wa namna ya kukomesha matukio ya utekaji nchini huku akigusia tukio la Padri Kitima kama sehemu ya mfano wa matukio yanayostahili kukomeshwa.​
Back
Top Bottom