Askofu Gwajima atoke hadharani aombe msamaha na kuapa kutorudia tena makosa yake ili afunguliwe Kanisa lake

Askofu Gwajima atoke hadharani aombe msamaha na kuapa kutorudia tena makosa yake ili afunguliwe Kanisa lake

unasema Mama ana huruma, atamfungulia halafu unasema tena, ni sheria ndiyo iliyofunga kanisa.

kumbe huruma nowdays imekuwa ni sheria. acheni kushauri hivi jamani, acheni sheria ichukue mkondo wake si mna uhakika alivunja sheria.
Nimeeleza vyema kabisa katika andiko langu juu ya jambo hilo
 
Huyo mama yako ni nani mpaka Gwajima ajitokeze na kumuomba msamaha!! Hivi unafahamu sehemu kubwa ya akili ya mtoto anachukua kwa mama yake? Sasa kama wewe mwenyewe ni kilaza, huyo mama yako si atakuwa ni kilaza×2!
Ungeacha wenye akili Timamu wajadili hoja
 
Nimesoma kabla ya kuandika. Ujumbe niliopata ni kua "mama" aombwe misamaha ili kanisa lifunguliwe.
Simple logic ni kuwa yeye ndie alieamuru lifungwe pasina haki.
Kwa lugha nyepesi hapa kua na utawala wa Sheria katika kulifikia hili jambo, ni jazba na pengine chuku au kukurupuka.
Uchawa mwengine huu mnaweza kuona mnatengeneza kumbe mna haribu.
Majibu yapo ndani ya andiko langu
 
Ukishazoea vya kupewa, uwezi jua haki yako.

Utalamba miguu siku zote kwa sababu ushakuwa ‘psychologically conditioned’ you are nobody.

Nchi ina inaongozwa kwa sheria na taratibu sio fadhila za watu kama unavyoamini.

Gwajima ana wanasheria wake na mahakama huru serikali aishindi kesi.

Katiba inatambua uhuru wa kuabudu, na kama kuna sheria ya kufungia nyumba ya ibada (kwakuwa tuna copy and paste only) hiyo sheria lazima itakuwa inalalamikia hiyo dini kuwa na elements za (cult), mambo ambayo uwezi muhusisha nayo Gwajima miaka 800.

Moreover Gwajima ajaongea siasa, kazungumzia moral issues (utekaji) hayo ni maswala ambayo yapo ndani ya boundaries za church morals.

Kuzoea kwako kulamba miguu watu, sio mtazamo wa kila mtanzania. Nchi inaendeshwa kwa katiba na sheria sio utashi wa mtu.
 
Aombe msamaha kwa kukemea utekaji?

CC: Ndugai
 
Church morals 👇

“Thou shalt not kill.” Exodus 20:13

Sasa wewe unataka Askofu anyamizie, mambo ambayo anatakiwa kukemea kwenye injili.

Na tena aombe msamaha.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Namshauri sana Askofu Gwajima atoke hadharani aombe msamaha kwa yale yote aliyoyafanya. Amuombe msamaha Rais wetu Mpendwa ambaye Ni Mama mwenye huruma na Upendo , Ni Mama mwenye Kujali watu wake na msikivu.

Mama yetu Mpendwa na kipenzi chetu watanzania amesamehe wengi sana ,amewafungulia wengi sana milango ,amewasikiliza wengi sana . Ni mama wa upatanisho, ni Mama wa Amani ,Ni Mama wa huruma ,Ni Mama wa Wote ,Ni Mama wa watanzania wote. Ni Mama mcha Mungu ,Ni Mama mwenye hofu ya Mungu,Ni Mama ambaye hachoki kusamehe ,ni Mama ambaye kwake kutoa msamaha siyo jambo gumu.

Ni Mama ambaye ni msikivu ,ni mama wa Imani. Ni Mama mwenye kuachilia msamaha siku zote. Ndio maana kuna watu wamemtukana sana ,kumdhalilisha sana ,kumsengenya ,kumsaliti lakini wote amewasamehe na kuwafungulia ukurasa mpya wa amani na upendo. Ndio Maana ya kuja na 4R zake.

Hivyo basi askofu Gwajima kwa kutambua makosa aliyoyafanya anapaswa kutoka hadharani kwa hekima , unyenyekevu na upole wa hali ya juu sana kuliomba msamaha Taifa ,kumuomba msamaha Rais wetu,Kuomba msamaha kwa chama chetu cha Mapinduzi na watanzania wote kwa ujumla wake.kwa maneno,matamshi na kauli ambazo alizitoa kwa waandishi wa habari pamoja na madhabahu ya kanisa lake.

Aombe msamaha na kukiri makosa yake na kuahidi kutorudia tena makosa yake. Ya kugeuza madhabahu kuwa uwanja wa kueneza chuki , uchonganishi na mtafaruku. Lazima aombe msamaha kwa kutoa maneno na matamshi yenye kumshambulia Rais na taasisi ya Urais na hivyo kuishushia heshima na kuifedhehesha pamoja na kuichafua kwa maneno yasiyo na ukweli wale ushahidi wa aina yoyote ile.

Kuna sheria na kuna busara na hekima. Kwa magoti na kujutia ajitokeze hadharani na ikiwezekana atafute wazee wa kumsindikiza kuomba msamaha kwa watanzania na kwa Rais wetu Mpendwa.

Ifahamike ya kuwa kanisa la askofu Gwajima limefungwa na sheria na siyo mtu binafsi au au taasisi fulani. Ikumbukwe ya kuwa kila kitu kuongozwa kwa mujibu wa sheria ,kanuni ,katiba na miongozo. Hivyo ifahamike ya kuwa kanisa la askofu Gwajima lilifungwa kwa kukiuka mambo hayo yenye kuongoza uendeshaji wa ibada ambao unakataza mambo ya kuchanganya siasa na Dini hususani mahubiri yenye kuchochea chuki na kuleta uchonganishi pamoja na kuwagawa watu..

Kwa hiyo ifahamike kuwa kanisa halijafungwa na Rais Samia na serikali yake bali limefungwa kwa Mujibu wa sheria, miongozo na kanuni za uendeshaji wake. Lakini pamoja na kufungwa huko kwa kukiuka sheria bado kuna nafasi mbele ya moyo wa Rais wetu ambaye ni msikivu na mwenye moyo wa huruma ,upendo na kusamehe.

Rais wetu Ni mwanadamu na anayependa sana kuona amani na upendo vikitawala huku watu tukisameheana. Naamini askofu Gwajima akikiri na kuomba msamahama atasamehewa na kufunguliwa kanisa lake ili ibada za kweli na zenye kuhubiri neno la Mungu ziweze kuendelea kama kawaida na watu waendelea kuabudu.

Inawezekana askofu alidanganywa au kushawishiwa na watu au kupotoshwa na kupewa taarifa za uongo. na yeye kuamua kubeba bila kufanya utafiti wa kina kupata ukweli. Naamini anayo nafasi ya pili kama mwana mpotevu kurejea kwa Mama yetu kipenzi kuomba msamaha na kufungua ukurasa mpya.

Mama yetu ninayemfahamu mimi kwa siku nyingi tangia nimeanza kufuatilia siasa naamini atamsamehe na kutoa maagizo.

Askofu Gwajima rudi kwa Mama ,rejea kwa unyenyekevu. Na uombe msamaha na utasamehewa tu.

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Kwa kosa gani alilofanya wewe kiazi......hivi kwa mfano hata ukapewa kauteuzi, kwa akili zako za kichawa utasaidia nini sasa wewe zaidi ya kujikosha na kujipendekeza zaidi.
 
Uwe na adabu ewe Uliyekosa malezi ya wazazi wako
Ukiita watu misukule lazima unakamiwa na unashonwa mbaya...
ukitaka kuheshimiwa heshimu watu pia unataka Gwajima aombe radhi Kwa kosa gani? Kukemea utekaji na mauaji?? Pumbafu kabisa!!!
Wewe ulilelewa kijinga ndomana unatabia ya kujipendekeza kama mchepuko! Unatetea mauaji na UMWAGIKAJI DAMU alafu unataka uheshimiwe?? Hata wewe kamiwa tuu maana Huna adabu
 
Ukishazoea vya kupewa, uwezi jua haki yako.

Utalamba miguu siku zote kwa sababu ushakuwa ‘psychologically conditioned’ you are nobody.

Nchi ina inaongozwa kwa sheria na taratibu sio fadhila za watu kama unavyoamini.

Gwajima ana wanasheria wake na mahakama huru serikali aishindi kesi.

Katiba inatambua uhuru wa kuabudu, na kama kuna sheria ya kufungia nyumba ya ibada (kwakuwa tuna copy and paste only) hiyo sheria lazima itakuwa inalalamikia hiyo dini kuwa na elements za (cult), mambo ambayo uwezi muhusisha nayo Gwajima miaka 800.

Moreover Gwajima ajaongea siasa, kazungumzia moral issues (utekaji) hayo ni maswala ambayo yapo ndani ya boundaries za church morals.

Kuzoea kwako kulamba miguu watu, sio mtazamo wa kila mtanzania. Nchi inaendeshwa kwa katiba na sheria sio utashi wa mtu.
Amshavunja katiba na sheria za usajili wa kanisa lake na hata yeye mwenyewe anatambua jambo hilo
 
Amshavunja katiba na sheria za usajili wa kanisa lake na hata yeye mwenyewe anatambua jambo hilo
Kuvunja sheria sio swala la kujiamulia tu, linahitaji legal justification mahakamani.

Ni vipi amevunja sheria? Hadi kufungia kanisa zaidi ya watu huko serikalini kutoheshimu katiba.

Gwajima alikuwa very careful kwenye kauli zake, hana kesi ya kujibu zaidi ya serikali kukurupuka.
 
Back
Top Bottom