Askofu Gwajima aushangaa ubalozi wa Marekani kuzungumzia suala la Mbowe aliyedondoka au kuvamiwa

Askofu Gwajima aushangaa ubalozi wa Marekani kuzungumzia suala la Mbowe aliyedondoka au kuvamiwa

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Akizungumza katika kipindi cha Aridhio kinachorushwa mubashara na TBC, askofu Gwajima amesema balozi wa Marekani nchini hapaswi kuingilia mambo ya ndani ya taifa letu.

Gwajima amesema juzikati balozi wa US amezungumzia swala la Mbowe aliyeanguka au kuvamiwa na kuacha kuzungumzia mambo ya nchi yake ambako askari wamemuua raia mwenye asili ya Afrika kinyama kabisa.

Askofu Gwajima amewataka Watanzania kuwa macho na mabeberu hasa wakati huu tunapoelekea kwenye uchaguzi.

Chanzo: TBC Aridhio!
 
Safi sana, nimekuwa nikitafakari huu ubalozi wa Marekani nchini mwetu Nabaki kushangaa, inafikia kipindi wanaanza kuzungumzia mambo personal ya nchi yetu

Mbona sioni ubalozi wa China, Italy, Sweden, Norway nk ukijihusisha na mambo yetu?

Mtumishi wa mungu ndugu Gwajima kaona mbali, Mungu ambariki sana

Sent from my TECNO KB7j using JamiiForums mobile app
 
Huyo Gwajima na zile tuhuma zake zenye ushahidi mpaka wa video nani bado anamuamini mpaka leo?

Atakuwa na matatizo, ameuvaa ulimwengu zaidi ya kuwa kiongozi wa kiroho, bora nae atafute jimbo huko kwao akagombee, atabebwa na mwenzie.
 
Huyo sio Askofu bali ni muhuni kama wahuni wengine. Maaskofu wanafahamika wanaoongoza makanisa taasisi, sio hilo genge la wahuni. Halafu maoni yenyewe anatolea TBC!

Mzee mgaya unakwama wapi, mbona huzungumzii hiyo bajeti ya kampeni ya ccm? Naona ccm wamegeuza bajeti ni eneo la kufanyia kampeni, matokeo yake watu wameipuuza wala hakuna anayeijadili kwa hivyo. Hata ww naona umeipotezea.
 
Kuna watumishi wa Mungu na kuna watumishi wa shetani ambao wamegeuza imani za watu kama mitaji au chanzo chao cha mapato(wajasiriamali wa kidini).

Ni jukumu lako kumtambua kiongozi wako wa kidini anaangukia kundi gani.
Huyu ni Mtanzania ana haki zote kuisemea nchi yake , Kwa upande wako Balozi wa Taifa jingine ana mamlaka gani ya kuhoji mambo ya ndani ya Taifa jingine au huji mipaka ya mabalozi?
 
Huyo sio Askofu bali ni muhuni kama wahuni wengine. Maaskofu wanafahamika wanaoongoza makanisa taasisi, sio hilo genge la wahuni. Halafu maoni yenyewe anatolea TBC!

Mzee mgaya unakwama wapi, mbona huzungumzii hiyo bajeti ya kampeni ya ccm? Naona ccm wamegeuza bajeti ni eneo la kufanyia kampeni, matokeo yake watu wameipuuza wala hakuna anayeijadili kwa hivyo. Hata ww naona umeipotezea.
Nimejichimbia naipitia bajeti kwa kina bwashee!
 
Back
Top Bottom