#COVID19 Askofu Gwajima awataka watu wasiingilie imani ya kanisa lake, hawachanjwi, watakaojaribu kuiingilia wataingia kwenye "crusher" watasagwa

#COVID19 Askofu Gwajima awataka watu wasiingilie imani ya kanisa lake, hawachanjwi, watakaojaribu kuiingilia wataingia kwenye "crusher" watasagwa

Cannabis

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2014
Posts
11,557
Reaction score
33,535
Leo katika kanisa la ufufuo na uzima Askofu Gwajima asema watu wasiingilie imani ya kanisa lake, amesema kuwa kiimani wakristo na hata waislamu wanaamini pombe ni dhambi na mahubiri hutolewa kupinga matumizi ya pombe, Je hao wanaohubiri wanatakiwa wakamatwe kwa sababu wanaikosesha serikali mapato?

Amesema wale wanaojaribu kuingilia imani ya kanisa lake wanaingia kwenye "crusher" watasagwa sagwa. Askofu Gwajima amesisitiza imani ya kanisa lake ni hawachanjwi na hivyo wasitishwe na yoyote.

Askofu Gwajima anaenedelea kumwashia moto Waziri Afya, more updates to follow

===

Askofu Gwajima awataka Waziri wa Afya na Naibu Waziri wa Afya wajiuzulu kwa sababu walizunguka nchi nzima kuelezea athari za chanjo kisayansi miezi michache iliyopita, lakini hivi sasa wameanza kuzunguka tena kuwaambia watu wachanjwe bila kutoa elimu ya kisayansi.

Amesisitiza Waziri wa Afya Dr. Dorothy and Naibu Waiziri wa Afya Dr. Mollel wajiuzulu kwa sababu wamemsaliti Rais, wanalazimisha watu kuchanjwa japokuwa chanjo ni hiari.

Amemshutumu Dr. Dorothy kwa kuwaita watanzania waliokataa chanjo ambao ni takribani 70% wajinga.
 
Leo katika kanisa la ufufuo na uzima Askofu Gwajima asema watu wasiingilie imani ya kanisa lake, amesema kuwa kiimani wakristo na hata waislamu wanaamini pombe ni dhambi na mahubiri hutolewa kupinga matumizi ya pombe, Je hao wanaohubiri wanatakiwa wakamatwe kwa sababu wanaikosesha serikali mapato ?

Amesema wale wanaojaribu kuingilia imani ya kanisa lake wanaingia kwenye "crusher" watasagwa sagwa. Askofu Gwajima amesisitiza imani ya kanisa lake ni hawachanjwi na hivyo wasitishwe na yoyote.

Askofu Gwajima anaenedelea kumwashia moto Waziri Afya, more update to follow
[emoji1787][emoji1787]
Ngoja tusubir kesho kwenye kamati ya maadili ya Bunge
 
Huyu bingwa wa teolojia kapiga kwenye kichwa cha joko lenyewe sawasawa.
 
Mimi ni muislam lakini kwenye hili la kuchanjwa nakubaliana na Gwajima, kwasababu najiuliza suali moja bila ya kupata jibu. Ni hivi:-
Magufuli alikataa chanjo katakata na viongozi wote walikuwa wana kubaliana nae, kwanini baada ya Samia kuwa Rais jambo la mwanzo kubwa analo kazania ni chanjo? Tena viongozi walewale walio kataa wakati wa Magufuli sasa hivi wanakubali au Magu kaondolewa ili hii ajenda ya chanjo ifanyike?

Lunatic [emoji2957][emoji2957][emoji2957]
 
MAMA SAMIA YEYE NI MUUMINI WA KUTAKA TUPEWE HERA BUREBURE SO ALILAZIMISHA TUCHUKUE CHANJO. HATA MAGUFURI WALIMUSHAURI AKUBALI LAKINI ILIONEKANA HIZO CHANJO ZINAZOLETWA SIYO ZILEWANAZOTUMIA ULAYA. SHIDA WANASANYI WATANZANIA HAWAJIBU HOJA...KWA MFANO KWANINI NIKICHANJWA LAZIMA NISAINI FORM YAKUSEMA NIKIPATA MADHARA SITAWASHITAKI SERIKALI? LAPILI KWANINI NIKICHANJWA LAZIMA NIENDELE KUVAA BARAKOA?
 
Screenshot_20210822-070836_WhatsApp.jpg
Screenshot_20210822-070902_WhatsApp.jpg
Screenshot_20210822-070850_WhatsApp.jpg
Screenshot_20210822-070823_WhatsApp.jpg
Screenshot_20210822-070816_WhatsApp.jpg
IMG-20210822-WA0052.jpg
 
Huyu siku zake zinahesabika.. Wako kimya wananuacha kwanza amalize kupayuka... Anawachokonoa kwa namna zote lakini wako kimya kabisa.... Inatia hasira sana kwake WAMEMPUUZA...NA INAMUUMIZA SANA HII
 
Huyu siku zake zinahesabika.. Wako kimya wananuacha kwanza amalize kupayuka... Anawachokonoa kwa namna zote lakini wako kimya kabisa.... Inatia hasira sana kwake WAMEMPUUZA...NA INAMUUMIZA SANA HII
Kweli Kaka Mshana selikali isipo chukua hatua mapema taasisi yote ya ikulu inachafuka.Mh Rais Samia Hassan achukie hatua mapema kabla Mambo hayajaharibika.
 
Proven beyond doubt.... Gwajima hana hekima, mropokaji na anayechanganya family matters na siasa
Wote majiganyanza. Waziri naye ndo kabisaaa...

Tena leo Askofu kamleta na baba yake kabisa na amesema huyo Dorothy atafute jina jingine kwa sababu familia ya Gwajima haitaki atumie jina lao.

Na tukisema ukweli hoja zingine za Gwajima zina uzito. Inabidi wizara itoe elimu ya chanjo ili wananchi waelewe badala tu ya kutumia nguvu hasa ukizingatia kuwa ni serikali hiyo hiyo iliyokuwa imewaaminisha wananchi kuwa chanjo ni hatari miezi michache tu iliyopita.
 
Kweli Kaka Mshana selikali isipo chukua hatua mapema taasisi yote ya ikulu inachafuka.Mh Rais Samia Hassan achukie hatua mapema kabla Mambo hayajaharibika.
Na hatua mojawapo nzuri ni kuwafukuza hao mawaziri wa Wizara ya Afya. Gwajima yeye sidhani kama ana la kupoteza. Kama ni pesa anazo za kutosha hata wakimfuta Ubunge na uanachama wa CCM siyo ishu kivile kwake.
 
Kama una hekima utajua tu downfall ya huyu mtu iko karibu kufika!
Nawahurumia tu waumini,unachoma mafuta gari unafika kanisani kusikia story ya dorothy gwajima alivyoolewa kwenye huo ukoo!
Hizi habari zitakusaidiaje kuingia mbinguni?
Nadhani hata mbingu zinashangaa sana,
 
Back
Top Bottom