Gwajima ameongea point Sana lakini watu msio jielewa mnanwabwaja tu fanyeni utafiti kuhusu hii chanjo mme kaa kwenye kibodi tu hapo mnaandika vitu msivyo vijua
Ngwajima kawa Daktari lini!, We unafikiri upatikanaji wa dawa zote unazotumia au maarifa mengi ya kimaisha pamoja na technologia tumevipata bila ya upendo wa Muumba wetu.Watu walogundua Computer unayotumia kuweka maoni yako ,gari unalotumia,na umeme Tanesco wanaokukatiaga,wengi hata huyu mungu hawakumwamini.Lakini Muumba kavileta kupitia kwao,na akawabariki na utaalamu na ujuzi,leo wewe mwamini Mungu unajimwambafai hapa jf.
Ngwajima kuwa na kanisa hakumpi yeye uwezo wa kujua vitu vya kitaalam,kwa maneno mengine,kuamini Mungu hakuna maana unajua kila kitu cha kidunia,vitu vya kitaalam vinahitaji mawazo ya kitaamu sio porojo.
Ili ujue mambo ya madawa lazima uende shule na usomee,Elimu imeletqa na muumba na kuijua kunasaidia binadam kutatua matatizo yetu ya kimaisha,dini zinatuweka sawa ili tuitumie elimu vizuri.Chanjo zipo miaka na miaka na kuna magonjwa yamepotea sababu ya upatikanaji na chanjo,mfano mzuri ni Polio.
Enzi za mikate kuanguka toka angani zimepita,enzi hizi Muumba wetu katubariki na elimu ya kulima ngano,kutengeneza moto,na kuoka mkate,kinachohitajika ni kutumia akili na kuacha uvivu ili tule mkate,na hii ndo baraka ya zama zetu.