#COVID19 Askofu Gwajima, Hutaki Kuchanja Nakuelewa, Lakini Kwanini Unashawishi na Wengine Wasichanje?

#COVID19 Askofu Gwajima, Hutaki Kuchanja Nakuelewa, Lakini Kwanini Unashawishi na Wengine Wasichanje?

Rationale

Member
Joined
Mar 13, 2021
Posts
24
Reaction score
98
Kwa muda mrefu sasa Askofu Gwama ametangaza wazi wazi kwamba hataki kuchanja chanjo ya Corona, ninamuelewa kwani ni haki yake binafsi kukataa, maana chanjo ni hiari. Mahali ambapo simuelewi ni pale anapofanya kampeni ya makusudi, ya waziwazi, tena kwa kutumia lugha kali sana kuwashawishi na kuwatishia watu (wafuasi) wake anaodai kwamba ni familia yake, kwamba wakchanja watakufa. Kama yeye hataki kuchanja si awaache wengine watumie haki yao? !?

Lakini pia, kwa kuwa Rais wa nchi anafanya kampeni ya kuwasihi watu wachanje, lakini yeye anakwenda kinyume na Rais, hii si kama usaliti kwa mamlaka?

Anayemwelewa atusaidie
 
Wengi wameanza kuchanja zile kelele za mitandaoni kuogopa chanjo zilikuwa upepo tu, watu wameona heri nusu shari kuliko shari kamili.
 
Anahofia sadaka zisije kufa na marehemu. Hivi wauminu wake ni watu wa aina gani ? Yaani wanasubiri akasome mitandaoni halafu akawahadithie kanisani.
 
Kwa muda mrefu sasa Askofu Gwama ametangaza wazi wazi kwamba hataki kuchanja chanjo ya Corona, ninamuelewa kwani ni haki yake binafsi kukataa, maana chanjo ni hiari. Mahali ambapo simuelewi ni pale anapofanya kampeni ya makusudi, ya waziwazi, tena kwa kutumia lugha kali sana kuwashawishi na kuwatishia watu (wafuasi) wake anaodai kwamba ni familia yake, kwamba wakchanja watakufa. Kama yeye hataki kuchanja si awaache wengine watumie haki yao? !?

Lakini pia, kwa kuwa Rais wa nchi anafanya kampeni ya kuwasihi watu wachanje, lakini yeye anakwenda kinyume na Rais, hii si kama usaliti kwa mamlaka?

Anayemwelewa atusaidie
Kwa hiyo haki Ni kuchanja!!!
Kutochanja si haki??
Ndugu hii chanjo Ni hiari, Kama ilivyo hiari Kama ilivyo hiari ya kuchagua dini unayotaka, na bado Kuna watu wanawashawishi wenzao kuchagua dini wanazoziamini wao na Wala hawajaonekana na makosa, hiari ya kununua bidhaa fulani lakini bado haiwazuii watu kuipigia debe, hiari ya kuchagua kiongozi lakini bado utashawishiwa kumchagua mtu fulani kupitia kampeni.
Hiari yashinda utumwa, sasa wewe wataka hiari yenye utumwa, yaani mtu akitoa ushauri kwa watu ili wawe na msimamo fulani amepotosha?
Kwani kawalazimisha?
Hata kufuata maneno ya Gwajima Ni hiari, hiari kwenda mbele hivyo hata kufuata msimamo wako pia Ni hiari,.
Kuwa mpole tu mkuu, usilete udikteta ambao serikali haina.
Acha wananchi tusikilize pande zote mbili tufanye maamuzi.
Hivyo unapoteza muda wako kimshambulia mtanzania mwenzio, badala ya kueleza ubora wa chanjo yako ambayo mwenzio kaipinga.
 
Back
Top Bottom