Askofu Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, amesema Kanisa halitayumbishwa wala kujadiliana katika masuala yanayohusu imani yake, akisisitiza kuwa yuko tayari kuisimamia imani hiyo kwa gharama yoyote.
Akizungumza katika ibada ya kufunga mwaka 2025 na kuukaribisha mwaka 2026 iliyofanyika usiku wa kuamkia Januari 1, 2026 katika Makao Makuu ya Kanisa la Ufufuo na Uzima, Ubungo Chai Bora jijini Dar es Salaam, Askofu Gwajima amesema baadhi ya viongozi wa kanisa hilo wamelazimika kwenda nje ya nchi ili kuokoa maisha yao kutokana na changamoto walizokumbana nazo, akieleza kuwa kanisa litaendelea kuwaombea ili Mungu awape nafasi na ulinzi.
Askofu Gwajima amesema misimamo ya kanisa hilo imejengwa juu ya imani bila mjadala wowote, akisisitiza kuwa yeyote asiye tayari kusimama imara katika imani hiyo hawezi kuwa sehemu ya msingi ya kanisa.
Ameeleza kuwa ingawa Wakristo hufundishwa unyenyekevu, uvumilivu na huruma, kuna nyakati ambazo kusimama kidete katika masuala ya imani ni jambo lisiloepukika, akiongeza kuwa hawezi kurudi nyuma wala kujadiliana katika masuala yanayohusu Mungu wake.
Soma pia Askofu Gwajima: Utekaji si utamaduni wetu na halitakiwi kuchekewa!
Askofu Gwajima: Utekaji si utamaduni wetu na halitakiwi kuchekewa!