#COVID19 Askofu Gwajima Kaathiriwa na Filamu za Hollywood "Fiction movies" Pamoja na Mambo dhahania

Na kaswali kamoja tu ivi kwanini hamjibu hoja zake?

Hii nchi inachekesha Sana.
Sasa hoja ya Gwajima ni ipi ili ijibiwe?

Mtu anaongea porojo zake ambazo hazina MANTIKI alafu unategemea apewe hoja zenye MANTIKI. Wewe uliona wapi mambo ya hivyo??

Yaani mtu aangalie Filamu ya Hulk, au Batman alafu akuambie inawezekana mtu akawa vile, utamjibu nini Kama sio akili za kitoto.

Gwajima Hana hoja isipokuwa anatumia haki yake kutoa maoni yake ya Filamu za Hollywood
 
Viongozi wangapi walipingana na Jiwe? ... ilibaki tu kila mtu akilinda ngozi yake ... ili familia yake iendelee kumuona!
 
nini umuhimu wa chanjo kama mtu akichanja bado anaweza kuambukizwa, chanjo inamana gani kama mtu akichanjwa bado inambidi asikae kwenye mikusanyiko? nini maana ya chanjo kama nikichanja bado naendelea kuvaa barakoa? chanjo inaulazima gani kama nikichanja bado naweza kuumwa corona na nikafa kabisa, nini tofauti kati ya aliye chanjwa na asie chanjwa? gwajiboy ana hoja na inabidi zijibiwe na kama kupinga chanjo ayo mataifa mnayo yaabudu hata wao raia wao wanawasiwasi na hizo chanjo na juzi tu kulikuwa na maandamano ufaransa marekani wametoa adi ofa ya dolla mia kwa kila raia atakae chanjwa, kuna kitu nyuma ya chanjo ila usiniulize ni nini?
 
... hiyo nanotechnology anayoongelea Gwajima ni 'pure science fiction' ukilinganisha na nanotechnology halisi ambayo bado ipo kwenye mapambazuko yake ... yaani Gwajiboy anaongelea njozi za NANOTECHNOLOGY!
NB: Naotechnology ikifikia level za Gwajiboy basi hata Robots zitakuwa 'self aware' na ataweza kuzihubiri GOSPEL!
 
Tangu aseme ule mkono sio wake ni wa baunsa sina ham nae tena yan
Nashaangaa sana watu wanaomtazama kwa jicho la uaskofu..mshenz,mzinzi,muongo kimacho macho[emoji15] hivi unamuogopaje huyo mtu!!!
 
Hayo yote uliyoyauliza mbona yameshaelezewa hata humu JF.
 
Hayo yote uliyoyauliza mbona yameshaelezewa hata humu JF.

mkuu tunaomba uyajibu tafadhali itapendeza sana kama yakijibiwa ili tumuaibishe gwajiboy aache kutuchonganisha na serikali yetu pendwa sana
 
Sasa Kama mtu hujawahi kupande Ndege na huna mpango wa kwenda nchi za mbali unafikiri hili la Chanjo linakuhusu Mkuu?

Binafsi siiogopi hiyo Chanjo, yaani niogope kisa nimemsikia muangalia Filamu za kizombi akinitisha πŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒ
Nakushauri uingie kwenye tovuti ya CDC ujionee mwenyewe mambo ya zombie preparedness sio tu mnakimbilia kumhuku Gwaji boy
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ ndege
Unaenda wapi na hizo ndege mkuu?
 
Nakushauri uingie kwenye tovuti ya CDC ujionee mwenyewe mambo ya zombie preparedness sio tu mnakimbilia kumhuku Gwaji boy

Nilitegemea ungenambia niende sehemu Fulani hapa duniani nitaonana na hao mazombi sasa wewe unanieleza kwenye Tovuti zenye Fiksi Mkuu.

Kuna Fiction stories, MOVIES, na hizo websites
 
mkuu tunaomba uyajibu tafadhali itapendeza sana kama yakijibiwa ili tumuaibishe gwajiboy aache kutuchonganisha na serikali yetu pendwa sana

Huwezi muaibisha mtu Kama Gwajima, mtu anayeishi kidhahania huwezi muaibisha kabisa.
 
Nilitegemea ungenambia niende sehemu Fulani hapa duniani nitaonana na hao mazombi sasa wewe unanieleza kwenye Tovuti zenye Fiksi Mkuu.

Kuna Fiction stories, MOVIES, na hizo websites
Kama walichokiandika CDC ni fix kwa mjibu wako basi hata product wanazozitoa pia ni fix. Au huelewi CDC ni akina nani hapa duniani.

Yani kifupi WHO ni tawi tu ambalo liko attached na shina liitwalo CDC

Na kuhusu uzombie mbona wamefanikiwa sana kuwatengeneza. Angalia jamii inayokuzunguka hapo hujaona mazombie kweli. Hivi kwa akili ya kawaida mwanamke unaweza tembea uchi balabalani tena mchana kweupe kweli? Labda hujanielewa namaanisha uvaaji wa nguo za kulalia ambazo kama si kuonyesha laivu maumbile ya siri basi yatachorwa bila kificho, huo si uzombi ni nini.

Uvaaji wa nywele za maiti wa kizungu ili tu afanane na mzungu(kujikana nafsi) mpaka wengine zinatoa harufu ya panya aliekuafa kichwani si uzombie ni nini

Mtoto wa kiume kupaka makeup na kutoboa masikio sasa wengine wanapaka mpaka lip shine hujaona uzombie hapo

Watoto wetu siku hizi hawafundishiki yani ni vilaza hatari mpaka imepelekea serikali kupanua goli ili angalau ionekane wamefalu wengi huo si uzombie pia?

Hiyo ni mifano michache sana ya zombie praredness
Eb ww nambie uzombi unautarajia ni upi
 
Wewe unazungumzia ishu za kimaadili, mabadiliko ya kiutamaduni, NK.

Hapa tunazungumzia ishu kibaiolojia
 
Shia sio Gwajima, tatizo hili walilianza wenyewe wataalamu, wamebadili gear angani ghafla bin vu bila maelezo ya kutosha.
https://www.facebook.com/Hawa ndiyo waliotupoteza wala siyo Askofu Gwajima.
 
Shia sio Gwajima, tatizo hili walilianza wenyewe wataalamu, wamebadili gear angani ghafla bin vu bila maelezo ya kutosha.
https://www.facebook.com/Hawa ndiyo waliotupoteza wala siyo Askofu Gwajima.

Ni kweli kabisa.

Basi hoja ya Gwajima ilipaswa iwe Kwa nini hao Viongozi wamebadilisha Gear angani, na sio hizo hadithi zake anazozitolea kwenye Hollywood
 
gwajiboy ni wa mirembe tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…