Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Wakuu,
Askofu Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Dkt. Josephat Gwajima, ameonekana mara ya kwanza kwenye madhabahu ya kanisa hilo lililopo Ubungo Kibo, Dar es Salaam, katika ibada ya mkesha wa mwaka mpya tangu lilipofungwa Juni 2, 2025.
Katika mahubiri yake, amegusia changamoto walizokabiliana nazo waumini wake na kusema: "Magumu yaliyokupata wewe ni kwasababu mimi nilikataa utekaji, mpaka leo nakataa vilevile."
Gwajima alifungiwa kanisa baada ya kuhusishwa na kauli za kukosoa matukio ya utekaji, huku Jeshi la Polisi likiwahi kutoa wito wa kumtaka afike kituoni kwa mahojiano kuhusu tuhuma mbalimbali.
Licha ya hilo, kurejea kwake kanisani hakukuripotiwa kuwa na hatari yoyote kwa usalama wake, tukio lililozua mjadala mpana wa kisiasa na kijamii.