Askofu Gwajima: Mungu ana jambo lake juu ya nchi ya Tanzania, na lazima litimie

Askofu Gwajima: Mungu ana jambo lake juu ya nchi ya Tanzania, na lazima litimie

Rabbon

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2022
Posts
25,937
Reaction score
41,161
Salaam, Shalom!

Ameanza kwa kusema kuwa SI Kila nchi ni sawa na ingine, Kenya SI Uganda na Uganda SI Tanzania.

Israel ni nchi kama tu zingine, lakini ni nchi special, nchi takatifu sababu Bethlehemu ya Uyahudi, alizaliwa Yesu.

Kadhalika Vatikani, Rome Italy, Au Saudi Arabia, ni nchi zenye historia.

Sasa hapa Nyikani ni nchi ya kipekee, ni nchi iliyochaguliwa na Mungu kuwa taifa la makimbilio kwa mataifa mengi duniani.

Vita na majanga yanakwenda kutokea kwa ukubwa duniani kote, ila hapa Tanzania, 🇹🇿 Mungu amepaandaa paje kuwa sehemu salama ya watu wa Mungu kujificha na kuwa salama watokao Pembeni zote za Dunia.

Tanzania ni nchi pekee ambayo patakuwa na Amani ya kweli wakati Dunia ikitaabika, ni nchi ambayo itakuwa salama.

Nyikani atainuka mtawala ambaye atakaa Katika kiti Cha ufalme akiwa ni nabii wa Mungu, mtumishi wa Mungu, atakaa kitini kuleta haki kwa wananchi, wana wa Mungu baada ya wanasiasa kushindwa. Nadhani tabiri mbalimbali umewahi kuzisikia.

Sasa kuwa kuwa ulimwengu wa Giza unalijua Hilo tayari na wanajua halizuiliki, wanajaribu kufunga nyumba za ibada Ili watu wasiombe na jambo Hilo lisitimie au kucheleweshwa.

Sasa kwa kuwa jambo hili lijalo limeamriwa na Mungu kutimia Katika majira haya , ni sharti litimie maana tangu mwanzo, Mwanadamu hajawahi kuweza kuzuia kusudi la Mungu kutimia duniani.

Mungu Mbariki Nabii wetu mzalendo Mchungaji Gwajima,

Mungu ibariki Nyikani.

Karibuni
 
Back
Top Bottom