Gwajima ahojiwi kwa kukataa chanjo bali matamshi ya kukataa. Kuna tuhuma nzito kwa Serikali katika matamshi yake. Alisema wanaoshadadia chanjo wamehongwa kukubali iingie! Yani Rais kahongwa, sasa akathibitishe kuhusu hili.
Pili alisema kwamba zoezi hili viongozi walikuwa wanadungwa 'maji' siyo chanjo kuhadaa umma. Hii ni very serious accusation ujue! Akathibitishe.
Tatu alisema lengo la chanjo ni kuua watu na kuwapa ulemavu, akaenda mbali zaidi kusema taasisi za ulinzi na usalama wasichanjwe maana tutakosa wapiganaji!
Nne alisema chanjo inatumika na wapinga Kristo kwa lengo la kufanya tracking ya kiasi gani Dunia inapokea matakwa yao. Yani ukichanjwa, umekuwa tracked! Akathibitishe.
Gwajima alipaswa kuifata tu option ya HIYARI ya Serikali kwamba chanja au acha ila kaa kimya usipotoshe wengine.
Miongoni mwa watumishi wa Mungu wenye ushawishi na wafuasi wengi ni Mwamposa, umewahi kumsikia anasema kuhusu hili? He knows nguvu ya imani, he knows exactly kwamba madhababu siyo sehemu ya kupiga vijembe, kusuta, kubishana na mamlaka.
Gwajima ni attention seeker, kwake kufatiliwa na watu kujaa kanisani ni a big deal.
Mark this tweet, akitoka katika kamati he won't be the same.