FRANCIS DA DON
JF-Expert Member
- Sep 4, 2013
- 38,920
- 44,970
Hii haiwezekani, umeme kukatika ni jukuma la Tanesco, tangu lini mwenye nyumba akahuska na masuala ya Tanesco?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sasa Askofu Gwajima kafanyaje kwenye hiyo nyumba????Kuna clip nimeiona facebook, gwajiboy ametembelea wananchi, ikatokea mwananchi mmoja wanasema alilalamika kwamba nyumba yake imeuzwa.
1. Alimpangisha muuza bucha
2. umeme ukakatika, nyama za bucha la mpangaji zikaharibika
3. mwenye bucha akasema mwenye nyumba amlipe nyama hizo 4m
4. wamevutana mwenyenyumba anaonekana hana hela, wakaenda mahakamaya Mwanzo Kawe
5. Mahakamaya mwanzo ikaamuru mwenye nyumba awekwe ndani miezi 6, na akakaa huko.
6. alipokuwa ndani, wakauza nyumba hiyo kwa mil.8.
7. thamani ya nyumba iliyoko barabarani ni kama 100m.
hoja yangu, kama hili jambo ni la kweli, naamini jamii inahitaji kuingilia kati. Pia, umuhimu wa Mahakama za mwanzo uchunguzwe kama bado zina umuhimu au tuache kesi zianzie district court. kwa wanasheria wenzangu wameshaelewa ninachomaanisha.
1. Jaji prof.Juma na mahakama yako ingilieni kati.
2. Hakimu aliyeamua kesi hiyo achunguzwe competence yake na credibility yake na kama anafaa kuendelea kuwa hakimu.
3. Mahakama za mwanzo limekuwa kimbilio la wazurumaji, ukitaka upore haki ya mtu, nenda tu primary court, honga hakimu, imeisha hiyo. hadi huwa natamani zifutwe tubaki na mahakama kuanzia wilaya na kuendelea.
Hii haiwezekani, umeme kukatika ni jukuma la Tanesco, tangu lini mwenye nyumba akahuska na masuala ya Tanesco?
Wakuu habari,
Week iliyopita bwana nikiwa kwenye misafara yangu kule maeneo ya kunduchi ununio,
Sasa nikakuta vurugu pale kunduchi mtongani,
Polisi purukushani na Raia,
Sasa hiko ivi: KUNA jamaa pale mtongani ana nyumba mbele Ina mafremu ya biashara Kama matatu hivi, Kuna fremu moja amempangisha jamaa aliweka butcher, Sasa kumbe akawa anamdai Kodi yule mwenye butcher akawa anamzungusha,
Imeenda enda,hiyo kesi tangu mwaka wa juzi nasikia, Sasa Kuna siku yule mpangaji wa butcher akawaagiza watu wakamletea nyama alfajili ,wakafungua wakamuwekea ndani kwenye mafriji,then wakasepa.
Walivyoondoka wale walioleta nyama, huku nyuma baba mwenye nyumba akachukua kufuli lake akafunga kwa juu yake pale kwenye lango la fremu, sasa bwana Jamaa mwenye butcher anafika asubui hili afungue afanye biashara,anakuta Kuna kufuli juu ya kufuli lake, mmh, akajiuliza kulikoni"
Ikabidi amuite baba mwenye nyumba hili amuulize kulikoni"
Baba mwenye nyumba akamjibu" sifungui Hadi unipe Kodi yangu , Jamaa akamlai Sana amfungulie afanye biashara Kwanza,hayo mengine watayamaliza tu,
Baba mwenye nyumba akagoma katakata, jamaa akaita Hadi watu wakaribu wamshawishi father house lakini wapi, Basi bwana kilichofuata Sasa......
Jamaa yule mwenye butcher akaenda serikali za mtaa kushtaki,Bado mwenye nyumba anachotaka pesa yake tu, yule wa butcher sikuile akahamua aondoke akarudi Baada ya week, akaenda baraza la kata kushtaki nasikia,, kesi ikasikilizwa, mwenye nyumba anaitwa haendi,
Mara kesi ikaenda mahakama ya mwanzo, amri ikatoka jamaa amlipe, maana nyama ilishaharibika kwa muda wote huo, jamaa mahakamani akawa haendi analeta tu usela mavi,
Deni na ghalama ya kesi ikafika milioni nane nasikia, Bado jamaa ana dhalau, Sasa ikafikia nyumba yake ikafanyiwa valuation ,ikauzwa kwa mnada kwa Bei ya milioni 11,
Hila kiukweli pale thamani tu ya eneo inafika milioni 35 au Zaid, Basi nyumba ikauzwa, mdai akapewa pesa zake,
Sasa aliyenunua kipindi chote hiko alikuwa kimiya, wale wakapelekewa taarifa wahame Bado wanakaidi, aliyenunua nyumba akaenda mahakamani kuwambia wamuhamishe hili apate nyumba yake, Basi wiki iliyopita ndio polisi Sasa kwa amri ya mahakama wakaenda hili wamuhamishe jamaa,
Kufika pale wanamkuta mzee wa watu na kitaulo anatoka kuoga, wanamuambia kavae suruali tuondoke,Kwanza umedhalau mahakama kipindi chote,pili tumekuja kukuhamisha, mzee akagoma, Basi polisi wakamshika hili wamtie kwenye difenda lao, bwana mzee akawa mtata, mara paaaap Taulo likaanguka mbele ya watoto na wajukuu, na watu Wengine, wanae Wengine ni madereva wa bajaji, Basi ikawa vurugu Hadi gari ya polisi ikavunjwa vioo na raia,
Mwisho wa siku polisi wakaondokanae, na aliyenunua nyumba akakabidhiwa nyumba yake,
Siku ya pili polisi walirudi na madifenda nasikia Kama yote, walibeba aliyekuwemo, na asiyekuwemo, kisa walivunjiwa gari yao, .
CHA KUJIFUNZA WENYE NYUMBA AU WATU TUSIPENDE KUTUMIA UBABE AU NGUVU, ITATUGHALIMU KISHERIA,
mwandiko mbaya nimepiga bapa mtanisamehe!
Gwajima alienda kwenye hiyo nyumba akahoji aliyedhulumiwa nyumba na muuza bucha, kuna clip inazunguka.Sasa Askofu Gwajima kafanyaje kwenye hiyo nyumba????
Sijaelewa content zako vs Gwajima.