Askofu Gwajima na siasa za ukabila, unafiki, uzandiki na jitihada za kuligawa taifa kwa mwamvuli wa dini

Askofu Gwajima na siasa za ukabila, unafiki, uzandiki na jitihada za kuligawa taifa kwa mwamvuli wa dini

Kama ambavyo Bi Mkubwa ana chuki dhidi ya Tundu Lissu na CHADEMA.
huyo mropokaji wa chadema kumbe ndio alikua kiongozi mkuu wa genge la uhalifu la utekaji nchini.
hivi sasa chadema imekufa na utekaji umetokomea waTanzania wananishi kwa amani bila hofu.

Mungu ni mkubwa sana kwa waTanznia, amewaumbua na kuwadhihirisha watekaji mchana kweupe pamoja na kiongozi wao ambae pia ni kibaraka wa mabwenyenye ya magharibi :putinWalk:
 
Tatizo umeandika kama mwanachama wa ccm
Jaribu kuwa neutral then uje na andiko lingine, andika kama mtu asiye na chama, na uje na mapendekezo bila kuegemea upande wowote
 
huyo mropokaji wa chadema kumbe ndio alikua kiongozi mkuu wa genge la uhalifu la utekaji nchini.
🗑
Kumbe wewe ndiye mropokaji Og.

Lissu akiwa mahabusu, kuna wananchi walitekwa pale mahakamani Kisutu kwenye kesi yake, wakapelekwa msituni Mabwepande wakaumizwa vibaya mno na kutelekezwa pale, aliongoza vipi huo utekaji?

Ukidanganya uwe unatumia akili angalau kidogo
 
👉Lakini tukio la kupigwa risasi kwa Lissu lilitokea mwaka 2017, wakati wa utawala wa Magufuli, na Gwajima akiwa ndani ya Bunge. Hakuinua sauti wala kuonyesha mshikamano wa kibinadamu
🚮
Uongo huu,
Mwaka 2017 Gwajima hakuwa mbunge.
Allingia bungeni baada ya uchaguzi mkuu wa 2020, yaani kuanzia November 2020, na hiyo ndiyo ilikuwa mara yake ya kwanza kuwa mbunge
 
🚨𝐆𝐰𝐚𝐣𝐢𝐦𝐚 𝐧𝐚 𝐬𝐢𝐚𝐬𝐚 𝐳𝐚 𝐔𝐤𝐚𝐛𝐢𝐥𝐚, 𝐔𝐧𝐚𝐟𝐢𝐤𝐢, 𝐔𝐳𝐚𝐧𝐝𝐢𝐤𝐢 𝐧𝐚 𝐉𝐢𝐭𝐢𝐡𝐚𝐝𝐚 𝐳𝐚 𝐊𝐮𝐥𝐢𝐠𝐚𝐰𝐚 𝐓𝐚𝐢𝐟𝐚 𝐤𝐰𝐚 𝐌𝐰𝐚𝐦𝐯𝐮𝐥𝐢 𝐰𝐚 𝐃𝐢𝐧𝐢.

👉Hivi punde, Kupita ukurasa wake katika mtandao ya YouTube, Mchungaji Josephat Gwajima, kama ilivyo ada yake, amezungumza tena na umma wa Watanzania, hotuba ambayo kwangu binafsi, haileti mwanga kwa Taifa mbeleni, bali kiza kinene kilichojaa udini, ukabila, unafiki na hatari ya kuligawa Taifa.

👉Gwajima amejaribu kuonesha taswira kuwa Taifa lipo njia panda na kwamba CCM itaanguka endapo haitamsikiliza yeye kuelekea Uchaguzi Mkuu. Ameitaja serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa shutuma mbalimbali, ikiwemo madai ya mauaji, utekaji, kufungiwa makanisa na hata kumtaja Tundu Lissu kama mhanga wa dhuluma.

👉Hata hivyo, hoja zake si ngeni kwa masikio ya Watanzania, na kama zilivyo mara nyingi, zimejaa upotoshaji, unafiki wa kisiasa na ajenda binafsi hatarishi kwa mshikamano wa taifa.

🔴𝑁𝑖𝑡𝑎𝑎𝑛𝑧𝑎 𝑘𝑢𝑒𝑙𝑒𝑧𝑎 ℎ𝑎𝑝𝑎 𝑘𝑤𝑎𝑛𝑖𝑛𝑖 𝐺𝑤𝑎𝑗𝑖𝑚𝑎 𝑛𝑖 𝑚𝑛𝑎𝑓𝑖𝑘𝑖. 𝐹𝑢𝑎𝑡𝑎𝑛𝑎 𝑛𝑎𝑚𝑖..👇👇👇

Leo hii Gwajima anajitokeza hadharani akilalamikia kufungwa kwa makanisa kana kwamba hili limeanza chini ya Rais Samia.??

Ukweli ni kuwa makanisa yalifungwa hata wakati wa Rais John Pombe Magufuli, kipindi ambacho Gwajima alikuwa Mbunge wa CCM kupitia Jimbo la Kawe;

⛪️Kanisa la EAGT Arusha Road Dodoma lilifungwa. ⛪️Assemblies of God Morogoro ilisitisha ibada kwa maelekezo ya serikali, na makanisa kadhaa Dar es Salaam yalifungwa kwa sababu za kisheria na kiutawala.

👉Gwajima hakusema chochote wakati huo, hakuandaa hotuba ya YouTube, hakuandamana na hakuwa msemaji wa ukristo kama anavyojionyesha leo. Ukimya huo unathibitisha kuwa msimamo wake wa sasa si wa kweli bali ni silaha ya kisiasa dhidi ya Rais Samia.

👉Kuhusu Tundu Lissu, Gwajima anataka umma uamini kuwa Lissu anaonewa leo.

👉Lakini tukio la kupigwa risasi kwa Lissu lilitokea mwaka 2017, wakati wa utawala wa Magufuli, na Gwajima akiwa ndani ya Bunge. Hakuinua sauti wala kuonyesha mshikamano wa kibinadamu.

👉Leo anajifanya mtetezi wa Lissu si kwa sababu ana uchungu wa dhati, bali kwa sababu jina hilo ni rahisi kulitumia kama nyenzo ya kumshambulia Rais Samia.

👉Isitoshe, kauli yake kwamba wakristo nchi nzima wasimpigie kura Rais Samia ni sumu ya mbaya kwa mshikamano wa Taifa. Misingi ya nchi yetu imejengwa juu ya mshikamano wa umoja, na historia ya dunia imejaa mifano ya mataifa yaliyoporomoka kutokana na siasa za udini, kama vile Sudan na Nigeria, ambako uchaguzi unageuka kuwa uwanja wa kugombania imani badala ya sera na maendeleo.

👉Hoja ya Gwajima inaibua hofu kwamba chuki zake zinachochewa na ukweli kuwa Rais Samia ni Muislamu, jambo linaloonyesha wazi nia ya kuingiza mgawanyiko wa kidini kwenye siasa za Tanzania. Hili si jambo la mzaha; ni hatari inayoweza kuharibu amani na mshikamano tulioujenga kwa miongo mingi.

👉Gwajima pia ametumia hoja za marekebisho ya sheria za uchaguzi, akitaka CCM ifanye kile anachokiita “minimal reforms” ambayo mengi yanabebwa na madai ya CHADEMA ya "No Reform No Election".

👉Ukweli ni kwamba madai haya yalianza zamani, kabla ya Rais Samia kuingia madarakani. Kipindi cha Magufuli, madai haya yalikuwepo lakini Gwajima hakuwahi kuyaunga mkono. Kauli yake ya leo haina uhalisia wa kiitikadi bali inalenga kudhoofisha CCM chini ya uongozi wa Samia.

👉Kwa upande mwingine, hoja yake kwamba CCM iko hatarini kuanguka inapingwa na takwimu na uhalisia wa kisiasa. CCM ina wanachama zaidi ya milioni 13 na mashina zaidi ya laki mbili kote nchini. Ni chama kilichojijenga kwa sera imara, mtandao mpana na historia ya ushindi wa kudumu. Kwa nguvu hii, ushindi wa CCM si swali la kama, bali ni suala la lini.

👉Kama haitoshi, kwanini nimediriki kusema Gwajima ni Mnafiki na muongo, Gwajima mwenyewe amewahi kutamka hadharani kwamba kazi yake ya uchungaji ni kubwa kuliko urais au ubunge, na kwamba hawezi kugombea nafasi hizo.

👉Lakini haikupita muda akajitosa kugombea ubunge na kushinda, akisaidiwa na ukaribu wake wa kikabila na Rais Magufuli. Tukio hili linaonyesha tabia ya kutokuwa na msimamo na mtu anayefuta mkumbo wa kisiasa.

👉Gwajima sio mtu wa kuaminika, historia yake binafsi imejaa tuhuma za kimaadili, ikiwemo madai ya kushiriki ngono na mfuasi wake wa kanisani. Hii ni doa kubwa kwa mtu anayejionyesha kama kiongozi wa kiroho na maadili. Ni unafiki mkubwa kuhubiri uadilifu hadharani huku mwenyewe ukipuuza misingi yake.

👉Hotuba ya Gwajima haijengi taifa. Ni jaribio la kupandikiza chuki za kidini. Tanzania haiwezi kurudi nyuma katika mshikamano na amani yake kwa sababu ya kauli za mtu mmoja anayetanguliza maslahi binafsi mbele ya maslahi ya taifa.

👉Rais Samia Suluhu Hassan na CCM wamesimama imara kwa mshikamano na maridhiano, na kauli za kijinga kama za Gwajima ni kelele za kisiasa zisizo na msingi mbele ya historia na mustakabali wa nchi yetu.
Wewe si Mwashambwa kabisa wewe, anyway, tu- assume unachosema no kweli, lakini kuna maswali muhimu ya kuyajibu;
1. Umeeleza vema kwamba mwaka 2017 Tundu Lissu alipigwa RISASI, na Gwajima hakusema chochote! Kwa akili yako, alitakiwa kuendelea kufumbia macho uonevu,Hilo lingekufurahisha?

2. Kufungwa kwa makanisa kwa sababu za "kisheria" unajua taratiibu zinazotakiwa kufuatwa unapofungia kabisa au taasisi yoyote ya dini? Je unaweza kutwambia makanisa ya Ufufuo na uzima yamefungwa kwa sababu gani za kisheria? Gwajima amesema sababu aliyoambiwa ni kwamba kabisa limejengwa karibu na Barbara, (kama Una sababu nyingine twambie) lakini kama sababu ni hiyo, je, makanisa yote ya Ufufuo na uzima nchi nzima yapo karibu na barabara? Lakini zaidi Sana, imesemwa kwamba karibu na kanisa kuna msikiti pia, kwanini limefungwa kabisa na msikiti umeachwa? Kwanini Mimi mkristo niipate hisia kwamba huu NI mwanzo WA kuushughulikia ukristo?

3. Mauaji ya watu na utekaji, unakiri kwamba matukio hayo yapo, na hayakuanza Leo, Bali tangu Enzo za JPM, okay,kwa hiyo unataka kuhalalisha uuaji na utekaji kwa sababu Tu, vilikuwepo toka enzi za JPM, na unaharamisha maoni yake kwa sababu Tu,mauaji yanayofanywa sasa ni mwendelezo WA waliokuwa wakifanya Samia na JPM?

Kama hii ndiyo namna mnavyotaka basi mjue mnachochea Moto ambao mwisho wa siku utaunguza wote, mnaofurahia na wanakwenda matendo yote ya uonevu, tutajikuta wote tunalia!
Himizeni haki, nchi yetu nzuri itastawi!
 
Back
Top Bottom