Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Walete chanjo mradi iwe hiari Tu
Asilazimishwe mtu kuchanja
Kwa imani yangu uhai ni zawadi ambayo Mungu amempa kiumbe wake.
Askofu Gwajima hakufanya utafiti wa kutosha kwanza FDA anasema ni Flag and Food Administration badala ya Food and Drug Administration pili mRNA anasema MRA kwa kujirudia.
Anasema kuna shirika linaitwa Emergency Drug Authorization ndilo lililoruhusu hizo vaccines za US huo ni uongo mkubwa tena, Regulatory Authority ya Vaccines Drugs na Food ni moja US ambayo FDA ndio ilifanya emergency use authorization ya Pfizer na Moderna vaccines sababu ya transmibility au maambukizi ya haraka sana na rate ya vifo vingi huyu Askofu anazidi kusema uongo mbele ya Bunge.
Awe kimya kama wabunge wenzake kwenye masuala ya Kitaalam Raisi ameunda time ya wataalam tuipe muda itakuja na report yake sio kuropoka uongo tu bungeni.
Halafu dunia nzima inahangahika na hili janga watz wengi walipotoshwa sana na madhara yake yako mpaka sasa kwani ukiaangalia mitandaoni ile isiyo makini wengi wanampongeza huyu mpotoshaji sababu ya kuwa brainwashed na wanasiasa.
Na hili liwe fundisho kwa nchi za Kiafrika Viongozi wa kisiasa wana ushawishi mkubwa sana kuliko wataalam wakiabuse hizo nguvu zao kuna madhara makubwa na ya muda mrefu.
Mungu anapenda nchi zote duniani sio Tanzania peke yake na tusiwe kisiwa hata nchi ndogo majirani zetu zinatushinda kwenye uelewa wa mambo nyeti ya sasa duniani.
Awamu ya 5 ilipatia kwenye kukataa lockdown lakini masuala mengi ya Corona kulikuwa na mismagement kubwa sana na kutokujipanga Mama ana kazi kubwa kutudisha kwenye mstari mmoja na Dunia.