Wanabodi,
Manabii wa Uongo na Tutawatambuaje?
Kwa sisi waumini wa dini ya Kikristo, tunayemwamini Bwana wetu Yesu Kristo, kabla hajapaa mbinguni, alituhusia kuwa "kutajitokeza manabii wa uongo, ambao watahubiri neno na kutoa mapepo kwa jina langu lakini sii wangu". Wanafunzi wake wakamuuliza, "Jee tutawatambuaje?", Yesu akawajibu, "Mtawatambua kwa matendo yao".
Askofu Dr. Josephat Gwajima ni Nabii wa Kweli au Nabii wa Uongo?
Hii ni thread ya swali kumhusu Kiongozi Mkuu wa Kanisa la Ufufuo wa Uzima, alijipa
mwenyewe daraja la uaskofu, na kujipa udakitari wa
mchongo kwa kujipa
Ph.D ya mchongo, Askofu Dr. Josephat Gwajima, Je ni Mtumishi wa Mungu wa Kweli?!, ni Nabii wa kweli au ndio wale manabii wa uongo aliowazungumza Bwana wetu Yesu Kristo?.
Askofu Dr. Gwajima, amejitapa yeye ni zaidi ya rais wa JMT!,
View: https://youtu.be/3uu59k7ExjY
jee ya kweli haya?
Akiwa katika mimbari, madhabahuni, mbele ya meza ya Mungu na wana kondoo wake, badala ya kuihubiri Injili na neno la Mungu lenye uzima na lenye kujenga upendo, amani na mshikamano miongoni mwa jamii, yeye anahubiri siasa kwenye nyumba ya ibada!, tena badala ya kuhubiri amani na upendo, yeye anahubiri chuki dhidi ya binadamu mwingine hadi kumuita "huyu kiumbe"!.
Japo ni kweli Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda alimdhalilisha Askofu Gwajima kwa kumtaja kujihusisha na madawa ya kulevya, Makonda alipewa tu list yenye majina na kazi yake ilikuwa ni kuwataja tuu, aliyemtaja Gwajima kuwa anajihusisha na biashara haramu ya madawa ya kulevya, sio Mkuu wa Mkoa, Makonda, bali ni muumini wake mtiifu, ambaye nimemtaja hapa chini
The bold: Waraka
sasa kosa la Makonda ni lipi?!.
Je namna ambayo Askofu Gwajima, anavyomzungumzia Mkuu wetu wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa ubaya na kumsingizia uongo, ndivyo Bwana wetu Yesu Kristo alivyotufundisha namna ya kuwashughulikia wale walio tukosea?!. Yesu alifundisha mtu akikupiga kibao shavu la kushoto, mgeuzie na la kuume!. Yesu ametufundisha "adui mpende". Yesu ametufundisha "samehe hata saba mara sabini". Vipi kuhusu Baba Askofu Gwajima kumuishi Bwana Yesu kwa maneno na matendo?
Je, Maneno na Matendo ya Askofu Gwajima ni kama Yesu, ni ya KiMungu?
Swali ni je huu ndio utendaji wa watu wa Mungu, kuwatakia wenzao mabaya?, kuwazushia uongo mchana kweupe tena madhabahuni kwenye mimbari ya Mungu?!. Yesu alitufundisha, "tumpe Kaisari yaliyo ya Kaisari, na tumpe Mungu yaliyo ya KiMungu, kwanini Askofu Gwajima, analeta ya Kaisari mezani kwa Bwana?!. Je huyu Askofu Gwajima, ni mchungaji wa Mungu au ni wa mungu?.
Askofu Gwajima kama mtu wa Mungu wa kweli, anaweza kweli kusema uwongo kama ule madhabahuni kwa Bwana?!. Je huyu ni mchungaji wa kweli anayemtumikia Mungu wa kweli, au ndio wale wachungaji aliyewasema Bwana wetu Yesu Kristo kuwa "kutajitokeza manabii wa uongo, ambao watahubiri neno na kutoa mapepo kwa jina langu lakini sii wangu". Wanafunzi wake wakamuuliza, "Je tutawatambuaje?", Bwana Yesu akawajibu, "Mtawatambua kwa matendo yao".
Je kwa matendo kama haya, kuna kitu chochote cha kutambua?
Askofu Gwajima ni Nabii wa Mungu, au nabii wa mungu?.
Japo nimewahi kushiriki Ibada kwa Askofu Gwajima, naomba mimi nisiseme kitu bali msikilize mmoja wa waumini wake ambaye pia ni mwanachama mwenzetu hapa jf.
Kwa ushuhuda huu mtaona tuhuma za kuuza unga kwa Askofu Gwajima hazikutolewa na Makonda kwa wivu wa helicopter au vita vya Jimbo bali Makonda alipewa majina na akayaanika.
Jumatatu Njema.
Paskali
Update
Wanabodi, kwenye siasa, hakuna rafiki wa kudumu, wala adui wa kudumu, kuna just common interest.
Japo katika bandiko hili, nilitofautiana na Gwajima, lakini kufuatia kwa sasa na mimi ni kada, wa Chama Cha Mapinduzi na mgombea aliyepitishwa na chama changu kugombea ubunge wa jimbo la Kawe kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi, ni Askofu Gwajima, then naomba kudeclare kuwa sasa namuunga mkono Askofu Gwajima 100% kwa 100% tukalikomboe jimbo la Kawe lilokuwa utumwani kwa kipindi cha miaka kumi, tulirejeshe CCM!.
Kwa Kawe ya Maendeleo, chagua CCM, Chagua Gwajima, na kwenye uRais ni Magufuli, Mbunge ni Gwajima na madiwani wa CCM.
Mimi na Gwaji Boy...dam dam!.
P