Askofu Gwajima: Tanzania ni yetu sote na ni Tanzania kwanza, mengine yote yanafuata

Askofu Gwajima: Tanzania ni yetu sote na ni Tanzania kwanza, mengine yote yanafuata

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
"Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa, wa bara na znz wanateuliwa na Rais na wanaondolewa na Rais pale anapoona hawafai, vile vile kwa mkuu wa jeshi la polisi na magereza. Mkuu huyu (yoyote kati ya hao) akipishana na rais kwenye jambo lenye maslahi ya nchi, halafu akashauri anaona jambo hilo linahatarisha usalama wa taifa anafukuzwa kazi! Kwasababu unaemshauri ana mamlaka tmya kukufukuza kazi, analetwa mwingine. Akionekana naye anakwamisha mambo fulani fulani kwa maslahi ya nchi anafukuzwa pia, akifukuzwa watu, akija wa nne atakubali kwasababu hawa ni binadamu, nao wanafamilia, na wana maisha na matamanio yao. Akiona mwenzake alitetea maslahi ya nchi akafukuzwa itabidi yeye kubali"

"Anafukuzwa sio kwasababu amefanya kosa, ni sababu anatetea maslahi ya nchi. Kwahiyo tukifanikiwa kuwalinda hawa wakuu wa vyombo wasifukuzwe hivi hivi kirahisi watakuwa na uwezo wa kusimamia nchi yetu vizuri bila kupata madhara ya yanayoathiri familia zao, utekaji utaondoka."

 
Back
Top Bottom