April 2019
Geneva, Switzerland
China yakataa kuvikwa kilemba cha ukoka kuwa ni nchi 'Tajiri' ya dunia ya kwanza
Taifa la China katika kikao cha Shirika la Kimataifa la Biashara / World Trade Organization (WTO) limekataa kutambuliwa kama taifa lililoendelea kama nchi za Marekani, Ufaransa, Ujerumani na kusisitiza kuwa China bado ni nchi 'Inayoendelea' kupigana na umasikini wa watu wake ili labda baada ya miongo kadhaa ndiyo itakuwa imefikia kiwango cha nchi hizo tajwa tajiri zilizoendelea.
Watu wengi wameshangazwa na taifa hilo la China lenye uchumi mkubwa wa pili duniani baada ya Marekani, kuwa bado ipo pamoja na nchi za uchumi duni kama Tanzania, Nepal, Guatemala ikipambana na umasikini.
Pengine pamoja na uchumi mkubwa lakini China yenye idadi ya raia Bilioni 1.4
Population, total - China | Data ina masikini wengi kuliko Marekani. Nchi ya Marekani sensa yake ya mwaka 2018 inaonyesha ina idadi ya watu milioni 330 na kiwango kidogo cha watu masikini kulinganisha na China.
Kutokana na ulinganifu huo pamoja na China kuwa na madaraja mengi, reli zenye urefu mwingi na maendeleo makubwa ktk vitu lakini China imekubali kuwa bado maendeleo ya watu nchi humo yapo duni hivyo haistahili 'kilemba' hicho cha ukoka ambacho nchi mabeberu wanataka kuivisha.
Kilemba hicho cha ukoka kuwa 'wewe ni tajiri' huenda na majukumu mengi ambayo nchi tajiri zilizoendelea wamejiwekea na China kubaini hawana uwezo wa kuyatekeleza kwa sasa.
Tanzania inabidi kujifunza kukubali nchi yetu bado ipo nyuma si tu ktk Maendeleo ya Vitu bali lililo baya zaidi pia tupo nyuma sana ktk Maendeleo ya Watu.
Nchi kama Cuba imeweza kupata maendeleo ya watu ktk nyanja za elimu na afya yanayofikia nchi tajiri zilizoendelea ila bado ipo nyuma katika maendeleo ya vitu. Umri wa kuishi watu nchini Cuba ni wa juu kama wa nchi za Marekani ya Kaskazini na ulaya. Lakini pia huduma za afya na kinga dhidi ya magonjwa nchini Cuba ni ya kiwango cha juu kama nchi tajiri huku ikiwa na wastani mzuri wa daktari kuona wagonjwa wachache kama nchi zilizoendelea kutokana na vyuo vikuu kuelimisha madaktari na wauguzi wengi kama nchi zilizoendelea tajiri.
China refuses to give up ‘developing country’ status at WTO despite US demands
Despite being the world’s second-largest economy and its biggest exporter, Beijing continues to label itself as “the world’s largest developing country”
China is categorised as a developing country at the Geneva-based institution, which affords it “special and differential treatment”. This enables China to provide subsidies in agriculture and set higher barriers to market entry than more developed economies.
The dispute reflects a fundamental divide within the WTO that has threatened the future of the global multilateral trading system.
The United States
has long complained
that too many WTO members – about two-thirds – define themselves as developing countries to take advantage of the terms the status permits them to trade under.
Source: China refuses to give up ‘developing country’ status at WTO