Mbunge wa jimbo la Kawe ambaye pia ni kiongozi wa kiroho, nawasihi sana msipuuzie kuhusu hoja na maono yake kuhusu suala hili la chanjo ya UVIKO 19. Maandiko matakatifu yanafunua unabii kuhusu wa farasi wa kijivujivu.
Farasi kiunabii huwakilisha vita vyenye kutumia nguvu za mfumo wa kidini na kidola dhidi ya kusambazwa kwa injili ya kweli ya Kristo duniani.
Farasi mweupe aliwakilisha mfumo wa dini ya Kiyahudi ukiambatana na dola ya kipagani ya Kirumi injili ikaanza kusambaa ndani ya sehemu za Uyahudi. Farasi mwekundu akiwalisha hatua za awali za utawala wa makaisari wa dola ya Rumi katika kipindi cha awali cha historia ya kanisa , injili ikisambaa kwa watu wa mataifa na mwanzo wa mgawanyiko wa mlengo wa kimadhehebu kwa Wakristo wa awali, yaani matendo ya "Unikolai"
Farasi wa rangi nyeusi, ni kuwepo rasmi kwa mfumo wa dini ya Kikristo na mgawanyiko rasmi wa kimadhehebu wenye kukubalika kama mbadala wa "imani ya awali ya mitume". Na farasi wa kijivujivu ni kuwepo kwa mfumo rasmi wa dini moja ulimwenguni kote chini ya mtawala mmoja mwenye nguvu zote mkononi mwake za kisiasa na kidini, ambaye atatambulika kama ndiye Mungu hapa duniani.
Kwa wale wenye maono ya kiunabii, ebu kwa pamoja tupitie nukuu hii ya maandiko matakatifu;
UFUNUO 6:7-8
7 Kisha Mwanakondoo akavunja mhuri wa nne. Nikamsikia yule kiumbe hai wa nne akisema, “Njoo!” 8 Nami nikatazama, na kumbe alikuwapo farasi mmoja hapo, rangi yake kijivu. Na jina la mpanda farasi wake lilikuwa kifo, na Kuzimu alimfuata nyuma. Hao walipewa mamlaka juu ya robo moja ya dunia, wawaue watu kwa upanga, njaa, tauni na kwa wanyama wakali wa dunia.