Jiwe ni muoga sana,sijui kwa nini! Askofu Niwemugizi wa Kanisa Katoliki Rulenge Ngara Kagera,alipomkosoa alimind sana,hadi kuanza kuchunguza uraia wake ,wakampora hati yake yakusafiria yaani passport,sina uhakika kama alisharudishiwa!! Na hapa nikutokana na nguvu za Kanisa Katoliki tu,la sivyo Askofu Niwemugizi angekiona cha moto!!
Gwajima alikiona cha moto hadi kunyoosha mikono juu,nakujiunga na timu yakuabudu!
Kakobe alimkosoa jiwe,akatishwa na mzuka wa TRA akaufyata kimya,hadi leo anaabudi chochote kutoka kwa Magu!!
Lakini kipindi cha JK,viongozi wa dini walikua wanaiponda sana serikali ya Jakaya!
Katoliki kulikua na Kitima Charles rafiki yake mkubwa na Magu,alikua anaponda sana serikali ya Jakaya, Pengo pia alikua anaponda sana serikali ya Jakaya!
KKKT kuna Askofu mmoja nadhani wa Arusha, Malasula wa Dar Es Salaam,walikua wanaikalia kooni serikali ya Kikwete...
Angalikana kulikua na Valentine Mokiwa,aisee ilikua balaa,waliponda sana serikali ya Jakaya..
Kina Shekhe Ponda na taasisi yake,waliponda sana serikali ya Jakaya, Jakaya hakuwahi wapiga hawa viongozi wala kuwapa kesi za ajabu,yeye alikuaga na maneno yake tu yakuwakera,ilikua kwenye sherehe au mazishi ya kiongozi mmoja wa Kanisa,Jakaya alisema baadhi ya viongozi wa dini wanauza poda! Aiseee aliwasha moto balaa,alishambuliwa sana!
Vitabu vya dini vipo kwa ajiri yakuwakosoa watawala wa serikali,Magu ana urafiki na Kanisa Katoliki, ndiyo maana wala hawamsemi,subiri aje mwingine,watamsema,watatoa walaka utakua unasomwa makanisani hadi basi!!
Sent from my TECNO CA7 using
JamiiForums mobile app