PAYE
JF-Expert Member
- Jun 19, 2025
- 459
- 644
Mwenyekiti wa Baraza la Makanisa ya Kikristo Tanzania (CCT) Mkoa wa Dodoma, Askofu wa Kanisa la Mennonite Tanzania (KMT) Joseph Mtolela, ametoa wito kwa wananchi kuendelea kudumisha amani na utulivu baada ya uchaguzi, akisisitiza umuhimu wa kuheshimu misingi ya utulivu wa taifa.
Soma: Viongozi wa Dini Mbulu waliombea Taifa Amani na Utulivu kabla ya Uchaguzi Mkuu
Akizungumza wakati wa kongamano la Viongozi wa Dini mbalimbali wa Kanda ya Kati (Dodoma na Singida) lililoandaliwa kwa ajili ya kuliombea Taifa amani na utulivu kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 29, 2025, Askofu Mtolela alisema uchaguzi ni sehemu ya mchakato wa kidemokrasia unaopaswa kuendeshwa kwa utulivu na heshima.
“Ndugu zangu, hata baada ya uchaguzi kuna matokeo, tunahitaji amani. Tumeshaambiwa kwamba unapopiga kura unarejea nyumbani — ni sawa kabisa. Amani na utulivu wa nchi hii ni msingi mkuu kwa mustakabali wa mihimili yetu ya nchi; bila amani wananchi hatupo, tutakimbia, na tutakimbilia wapi?” amesema Askofu Mtolela.