The Palm Beach
JF-Expert Member
- Dec 30, 2015
- 1,967
- 4,267
Hatimaye Roho Mtakatifu asema na Askofu Josephat Gwajima wa makanisa ya Ufufuo na Uzima Tanganyika na duniani kuhusu watu na wanaharakati wakosoaji wa sera na mipango ya serikali, CCM na hususani Rais Samia Suluhu Hassan kutekwa, kuteswa kisha wengine kuuwawa na kutupwa kama mizoga ya panya porini au nyikani...
Haya ndiyo aliyosema Askofu Josephat Gwajima Kwa ufupi:
ASKOFU GWAJIMA: Tanzania pameanza kuwa si mahali salama tena.....
ASKOFU GWAJIMA: Nani atafuata kutekwa. Si ajabu mimi. Lakini nawaambia kwa Jina la Yesu Kristo hapa hatekwi mtu ng'o hata waje kwa njia za kichawi.....!
ASKOFU GWAJIMA: Kama akija polisi, huko nitakwenda kwa sababu nafahamu police ni law enforcers. Lakini hawa wanaokuja na tuvitambulisho vya ajabu, akikujia mwambie sogea kwanza tupige "selfie" ili niweke kumbukumbu sawa......
=========================================
UPANDE WA PILI;
Rais wa TLS Adv. Boniface Mwabukusi amshangaa Spika wa Bunge Tulia Ackson kuzuia mjadala kuhusu suala la utekaji na kuuwawa kwa watu ktk mazingira ya kijambazi na kigaidi huku polisi wakiwa hawaoneshi juhudi zozote kuzuia ujambazi na uhalifu dhidi ya uhai na maisha ya watu kwa kigezo cha "kanuni za Bunge kutofustwa...."
Mwabukusi amesema labda Spika Tulia Ackson atashituka na kuona thamani ya uhai wa maisha ya binadamu pale mumewe au mwanae atakapokuwa amepatwa na wahalifu hawa.....
Amesema, kuna mambo ya dharura hasahasa yanayohusu uhai wa mtu, huhitaji kufuata kanuni kulifanya intervention ili kurebisha mambo. Kinachohitajika spika kutumia power na authority yake tu kuli - table swala husika kwa judicial notice ili Bunge litoe maelekezo kwa serikali nini cha kufanya....?