Askofu Kanisa la Anglikana akutwa amekufa baada ya kutoweka siku tatu

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
1670016794969.png

Askofu mstaafu wa Kanisa la Anglikana Tanzania Dayosisi ya Victoria Nyanza (DVN), Boniphace Kwangu amekutwa amefariki dunia katika mazingira ya kutatanisha.

Marehemu alitoweka tangu Novemba 28 na mwili wake kukutwa ukielea katika Ziwa Victoria eneo la Bukumbi Wilayani Misungwi.

Akizungumza na Mwananchi kwa njia ya simu leo Ijumaa Desemba 2, Askofu wa Kanisa la Anglikana Tanzania Dayosisi ya Victoria Nyanza (DVN), Zephania Ntunza amethibitisha kifo cha mtangulizi wake huyo ambaye mwili wake ulikutwa ukiwa umetelekezwa wilayani humo jana.

"Ni kweli Baba Askofu Kwangu ametwaliwa. Bado hatujafahamu kwa kina chanzo cha kifo hiki. Sisi Kanisa na familia tumeliachia Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi kubaini chanzo cha kifo cha mpendwa wetu," amesema Askofu Ntunza.

Akizungumzia taratibu za mazishi, kiongozi huyo wa kiroho amesema; "Tayari tumefanya vikao na familia kuhusu msiba huu mzito lakini bado hatujapanga siku wala eneo la mazishi hadi polisi watakapokamilisha taratibu zao za kiuchunguzi,"amesema.

Kabla ya mwili wake kukutwa Bukumbi wilayani Misungwi, Askofu Kwangu aliyekuwa kiongozi wa nne wa DVN anadaiwa kutoweka kwa siku tatu zilizopita tangu alipoaga familia yake kuwa anaenda wilayani Sengerema kwa shughuli binafsi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Wilbroad Mutafungwa hakupatikana kuzungumzia tukio hilo baada ya kupokea simu yake ya kiganjani na kujibu kuwa yupo kwenye kikao na kuomba atumiwe ujumbe ambao nao haukujibiwa.

Chanzo: Mwananchi
 
Wachungaji wanauwana na kurogana sana

USSR
 
Askofu mstaafu wa Kanisa la Anglikana Tanzania Dayosisi ya Victoria Nyanza (DVN), Boniphace Kwangu amekutwa amefariki dunia katika mazingira ya kutatanisha.

Marehemu alitoweka tangu Novemba 28 na mwili wake kukutwa ukielea katika Ziwa Victoria eneo la Bukumbi Wilayani Misungwi.
Wamerudi au ni wale wale?
 
askofupiic.jpg

Askofu mstaafu wa Kanisa la Anglikana Tanzania Dayosisi ya Victoria Nyanza (DVN), Boniphace Kwangu

Mwanza. Askofu mstaafu wa Kanisa la Anglikana Tanzania Dayosisi ya Victoria Nyanza (DVN), Boniphace Kwangu amekutwa amefariki dunia katika mazingira ya kutatanisha.

Marehemu alitoweka tangu Novemba 28 na mwili wake kukutwa ukielea katika Ziwa Victoria eneo la Bukumbi Wilayani Misungwi.

Akizungumza na Mwananchi kwa njia ya simu leo Ijumaa Desemba 2, Askofu wa Kanisa la Anglikana Tanzania Dayosisi ya Victoria Nyanza (DVN), Zephania Ntunza amethibitisha kifo cha mtangulizi wake huyo ambaye mwili wake ulikutwa ukiwa umetelekezwa wilayani humo jana.

"Ni kweli Baba Askofu Kwangu ametwaliwa. Bado hatujafahamu kwa kina chanzo cha kifo hiki. Sisi Kanisa na familia tumeliachia Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi kubaini chanzo cha kifo cha mpendwa wetu," amesema Askofu Ntunza.

Akizungumzia taratibu za mazishi, kiongozi huyo wa kiroho amesema; "Tayari tumefanya vikao na familia kuhusu msiba huu mzito lakini bado hatujapanga siku wala eneo la mazishi hadi polisi watakapokamilisha taratibu zao za kiuchubguzi,"amesema.

Kabla ya mwili wake kukutwa Bukumbi wilayani Misungwi, Askofu Kwangu aliyekuwa kiongozi wa nne wa DVN anadaiwa kutoweka kwa siku tatu zilizopita tangu alipoaga familia yake kuwa anaenda wilayani Sengerema kwa shughuli binafsi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Wilbroad Mutafungwa hakupatikana kuzungumzia tukio hilo baada ya kupokea simu yake ya kiganjani na kujibu kuwa yupo kwenye kikao na kuomba atumiwe ujumbe ambao nao haukujibiwa.
 
View attachment 2433639

Wamejuaje kama huo ni mwili wa askofu!?

Maana kuitambua maiti iliyozama maji ni vigumu sana!
 
Back
Top Bottom