Askofu kazua balaa ibadani

Askofu kazua balaa ibadani

Ndo maana malaya wanaojiuza ni wanawake sio wanaume kwanzia kwenye enzi za bible ni hivo mkuu
Ila kiimani hii au kiroho hii haina upande...zinaa ni zinaa tuu haijalishi katenda Me au Ke.
 
Habari ya asubuhi wadau, samahani kwa kuleta uzi asubuh asubuh kama hivi siku ha kazi 😁.

Leo nilikua nikiendelea kutafakari tukio moja limejitokeza siku ya jumapili ya juzi tarehe 16 January hukooo kanisani kwetu "Assemblies of God" likaweka sintofahamu kubwa sana kwenye nafsi za sisi wengine.

Ilikua hivi, kuna askofu mmoja alikuja kushiriki nasi kama mgeni akitokea huko mikoa kanda za kati. Huyu askofu sababu kubwa iliyomleta anasema alipata msukumo toka kwa Mungu aje kusema na kusanyiko la wacha Mungu hapa kwetu hivyo akaona sio sawa kugomea wito aliopewa kusema na kanisa.

Lakini pia huyu askofu ni kama god-father wa mchungaji wetu na ni kama mentor wake maana alimlea kabla hata pastor wetu hana mawazo ya kuwa mchungaji kipindi hiko anapiga kazi kwenye miradi ya mashirika ya umoja wa mataifa sooo hata alipopata wito wa kuacha kazi ili aanza kuchunga kondoo wa Bwana ilikua ngumu sana kukubali na kwanza hata hakua akielewa haya mambo licha ya kuwa mwamini safi.

Na hapa ndipo huyu askofu alimsaidia sana namna ya kumuelewa Mungu toka katika angle nyingine tofauti ni ile ya kuwa kama mwamini wa kawaida. Sasa ndio hivyo akamsaidia sana kum mentor mpaka akakubali kuacha kazi na kuingia kuhudumu akianza kwanza kufungua kanisa kisha ndipo waumini sis tukapatikana.

Tukampeleka chuo cha uchungaji..Sio yeye tu na mke wake pia tukampeleka akasome Theology baada ya hapo maisha yakaendelea....so historia kwa ufupi iko hivyo.

Sasa nirudi kwenye topic kuhusu yaliyotokea hapa juzi Jumapili.

Askofu akiwa katika session ya mahubiri "akafunuliwa" jambo na akasema kuwa Mungu amemwambia alionye kanisa na hasa kuhusu Kwaya za kanisa.

Hakutaja kwaya ipi maana kanisani tuna kwaya ya Kanisa halaf tuna kwaya ya akina mama / wanawake na pia kuna Praise&Worship team ambaya wamo waimbaji (sio wote ila baadhi) toka kwaya zote mbili hizo tajwa hapo kwamza na muda huu wa mahubiri tayar kwaya zote zilikua zimeshaimba.

Pastor akasema nimeonyeshwa humu ndani kwamba kuna waimbaji humu jinsia KE wanahujumu NDOA. Sasa hakuweka bayana kama walioolewa af wanachepuka au ambao hawajaolewa ila wanatembea na waume za watu.

Akaendelea kusema kwamba anaweza kuwa point hata rangi za mavazi walioyavaa ila hatafanya hivyo kwakua roho mtakatifu alimkataza asije akawaaibisha na sio vizuri ila anawaomba baada ya ibada wakawaone wachungaji ili watengeneze maisha yao.

Sasa baada ya kumaliza mahubiri akaitwa waimbaji waje waimbe kabla ya kuingia kwenye maombezi 😂😂😂 aiseee hali ikawa ngumu sana maana ni kama watu kwa kiwango kikibwa wakapoteza confidense hivyo wengine hawakwenda japo wengine wakajikaza wakainuka kuhudumu.

Baada ya ibada nikaona kiongozi mmoja wa kike top pale kanisani kawaida wanawake waimba kwaya na kuongea nao ila ni kama maongezi hayakua mepesi ni kama kukawa na zogo la chini kwa chini huku mabinti wakionekana kukereka zaid lakin sikufanikiwa kujua nini kilijiri.

Sasa ile hali ikanifanya nijiulize vitu vingi sana na kimoja wapo ni kwamba je ni wanawake tu ndio wenye shida hii ya zinaa kanisani wanaume hakuna?

Mbona nimeshashiri vikao vingi sana vya kusuruhisha ndoa tatizo likiwa mwanaume kjchepuka???Hawa hawajaonekana au?

Isitoshe hata mimi hapa nachepuka kisela ingawa toka mwaka huuu uanze sijafanya hivyo na nilidhamiria kuacha maana najionea kero tu but inawezekanaje tukawekwa kando?

Nikajiuliza labda pengine kwenye kwaya wanawake ni wengi zaid kuliko wanaume ndio maana wakawa major concern? Maana kanisani kwetu sisi wanaume hawapend kabisa mambo ya kwaya, but hata hivyo dhambi ya zinaa madhabahuni pa Mungu ina uzito ule ule hata kama ingetendwa na mwanaume mmoja huku wanwake ni 7 bado zinaa ni zinaa tu sasa kipi hasa kilifanya wanawake wawe main talk?

Je, ndio mfumo dume ule ule hata makanisani kwamba kunya anye kuku tuu ila akinya bata kaharisha?

Lakini je hili lisingewekwa pending angalau wakaitwa wanawake peke yao likafanyiwa kazi? Ingawa ni kwel dawa ya uovu/dhambi kiimani ni kuikiri mbele ya watu ikusaidie na wewe kutorudia lakin hii haiwezi kumu destruct mtu?

Halaf kwa wale wanaume ambao wake zao wanaimba kwaya nikawaza watakua wako kwenye hali gani?? Watawafikiriaje wake zao?

Anyway ni hayo tu kwa leo.

Wajuzi wa maadili ya kiroho na kiimani naomba mtusaidie.
Nyie si mnajiitaga walokole, waliosikika na hamtendi dhambi tena kama sisi tusiookoka? Huyo roho mtakatifu anayesingiziwa na wazushi kuna siku atawageuka
 
Nyie si mnajiitaga walokole, waliosikika na hamtendi dhambi tena kama sisi tusiookoka?
Aaahhhh mkuu...ujue mkuu hii bado haiondoi ule ukwel kwamba kuna walokole ambao wako safi hawana makandokando.
Ni sisi wachache tu ndio tunawaharibia.
Tunatamani kuw kama wao ila misuli yetu bado
 
Hivi kweli mazoezi ya kwaya hadi saa 2 usiku na unakuta vijana hawajaoa wala kuolewa damu moto mara utasikia kuna ziara ya bagamoyo hapo ni mwendo kutafunana tu
 
Kwanza hilo Kanisa la TAG Lina laana Roho Mtakatifu hapendi hata kukuona .lipite huku [emoji118]
 
......mara utasikia kuna ziara ya bagamoyo hapo ni mwendo kutafunana tu
Hili pia ni tatizo mojawapo.Kanisa limeiga sana na kuingiza mfumo wa maisha ya kijamaa kanisani badala ya ku stick kwenye mawanda ya kiiman tuu.

Moja ya kitu sipend kanisani na oia huwa si support ni kitu kinaigwa "siki ya wanandoa" ambao wenye ndoa ztu huandaa outing kikanisa kila mmoja akiwa na mkewe au mumewe mnakaa somewhere mna barizi..
Kula vizuri...kunywa vizur ....mnavaa sio zile nguo zetu za vitenge kanisan hapana japo za ziwe na kimaadili mnakaa ku exchange mawazo.

Sio kitu kibaya lakin huwa sion mantik hake kiroho
 
Kwanza hilo Kanisa la TAG Lina laana Roho Mtakatifu hapendi hata kukuona .lipite huku [emoji118]
Hapend kuliona kanisa au hapendi kuniona mimi!??

Halafu ni nani alilaani?

Na wewe pia unaweza nambia una moral authority ipi ya kuwa condemn wenzio kiwango hicho.??
What is so wrong with that so called TAG maana hata sijalitaja kama ndio hao !!.
 
unamu underate Roho mtakatifu sana!! kaa ukijua Roho mtakatifu ni Mungu kamili kwaiyo anaweza ona kila kitu na kama anaweza kuona basi anaweza kuonyesha icho kitu kwa uwazi kabsa.
.
mbona ivo vitu ni vidgo sana hata ww unayesali hapo kama ukikaa vzr anaweza kuonyesha live sio vitu vingum vyakushindwa kuviona
Kama utakuwa na uwezo wa kusoma saikoloji ya mtu kupitia maandishi,,nazani utaelewa kuwa nimecomment kwa kile nilichokielewa kwa hiyo thread na si kwamba namu-underrate roho mtakatifu na kamwe siwezi kufanya hivo.
 
Nakubaliana na wewe mkuu. Na hii kitu mke wngu anayo.
Mara 3 kabla ya zote kuchepuka asubuh kabisaa alikua akiamka ananiambia kuwa ameota nafa ha zinaa na mwanamke.. na kwel mara zote...
2 wakorintho 11:14 "wala si ajabu maana shetani mwenyewe hujigeuza awe mfano wa malaika wa Nuru"....nijibu swali dogo tu,,tunawezaje kutambua ni nuru gani ambayo ni ya Mungu na ni nuru gani ambayo ni ya shetani tukiwa ndotoni??
 
2 wakorintho 11:14 "wala si ajabu maana shetani mwenyewe hujigeuza awe mfano wa malaika wa Nuru"....nijibu swali dogo tu,,tunawezaje kutambua ni nuru gani ambayo ni ya Mungu na ni nuru gani ambayo ni ya shetani tukiwa ndotoni??
Ahsante....ila kwa yf sio ishu ya shetani.Mke wangu ni mtu wa prayers sanaaaaaaaa af mwenyewe pia ndio hao hao japo nachechemea..
 
Back
Top Bottom