Mpendwa kipimo kipi kitatumiwa na serikali kujua hili kweli kanisa na lipi si kanisa? Je idadi ya watu ndo calibration ya hiyo meter itakayopima hayo makanisa? Nadhani hayo yatakuwa si makanisa kwa maana ya kanisa bali NGOs, CBOs, or any other organizations. Jaribu kukubali ukweli bila kuweka hisia. Huoni kuwa Askofu Kilaini na Gamanywa hapo anatetea uhai wa Kanisa lake kwani serikali kutoa democracy ya kuamini chochote inawapa freedom wakatoliki na wapentekoste kuhama ukatoliki au upentekoste kwenda kwingine? Ndo maana siamini katika dini kabisa maana binadamu wachache wana monopolise dini kwa faida binafsi na kuacha agenda ya Mungu nje yaani Imani. Kama kweli Kilaini anaamini katika roho mtakatifu yeye anashida gani? maana Yesu alisema hataliacha kanisa mpaka ukamilifu wa dahari meaning anauwezo wakulilinda lisifutike sasa hilo lake mbona anataka kulilinda kwa nguvu ya kidunia badala ya kimungu? Kama Mungu yupo pamoja nae nani atakua kinyume nae? Na kama issue ni kodi kwani hata kanisa likiwa na watu milioni thelathini matapeli je hawata kwepa kulipa kodi? Je hata kama hao milioni thelathini ni waaminifu Askofu wao akawa tapeli je hilo kanisa halitakwepa kulipa kodi?
Kama mkristo na utata na hiyo kauli kama inatakia mema wakristo na aliye kinyume chetu ni adui yetu; kama imani yangu inavyonituma basi aelewe kuwa kuutumia ukristo kupinga ukristo ni kupinga nguvu za kristo mwenyewe na kwasababu hiyo sina wasiwasi roho mtakatifu atawashughulikia kwa haki kabisa na kama nia yao ni kupinga injili yakristo basi itadhihirika muda si mrefu. maana injili ni habari njema kwa watu wote tena inanguvu hata kuleta uwokovu kwa yeyote aaminie kwa Myunani kwanza na kwa mataifa mengine pia. Hii inamaana ya kuwa yeyote mwenye habari njema ya upendo wa Mungu wa kweli haijalishi unajina gani Juma, Rajul, Tsetung, Masanja, etc huo ujumbe wako uta prevail no matter what maana unapeleka upendo wa Mungu kwa wasioujua huo upendo bila kujali umesoma, hujasoma, mfupi, mweusi, mweupe mnene, mwembamba, unaheshimiwa, unadharauliwa etc. Na habari njema ni hii kuwasaidia maskini, kuwatetea wanyonge, kuwafungua waliofungwa na nguvu za giza kama ufisadi, uchawi, uzinzi, ulevi etc, kuwapa matumaini waliokata tamaa na kutangaza nguvu za Mungu jinsi zinavyoweza kuondoa yote hayo. Ila kuna ziada katika kufanya hilo uwe na ile nguvu ndani yako yaani ukisema umaskini kesho utakwisha Tanzania na iwe kama utakavyosema bila hivyo wewe ni mwongo na unambeba shetani ndani yako kwakujua au kutokujua na kazi ya huyo ni kuiba, kuharibu na kuua.
So kanisa la leo la kristo kama ninavyoamini mimi wewe linaanzia kwa mtu binafsi meaning number sahihi ya kanisa ni mtu mmoja, akitokea mwenye mawazo kama yako anakuwa wapili and so on ili mpeleke hiyo habari njema hapo juu mkipata msamaha wa kodi Mungu ashukuriwe msipopata hewala, mmepewa sadaka asante Yesu mmenyimwa Mungu abarikiwe yaani mtumwa asie na faida ukiona mnaanza kugombana kwaajili ya kodi na sadaka na namba za watu mjue hapo wala hakuna injili kuna njaa tu na nibora mkafanye kazi mpate uhalali wakula vyakwenu kwakujinafasi.