Kwangu mimi huu ni Ushauri wa hovyo na wa hatari kwa nchi iliyojiwekea misingi ya uhuru wa kuabudu kwenye katiba yake. Yaani watz 200 wakitaka kuabudu wasihalalishwe kuabudu! Idadi gani ni halali?
mi nadhani wasiomuelewa ndio wapo kisiasa zaidiKilaini yupo Kisiasa zaidi !!!
Ni wazi anachosema ni hiki: Wako watu wanadanganya wao ni Kanisa, na kwa hivyo wasamehewe kodi. Hao serikali isiwape msamaha wa kodi.
There are con men who couldn't care less about God, but want tax exemption. So, they start a "Church" for the specific purpose of cheating on taxes. Sasa Kama Baba Askofu anataka wathibitiwe kuna mbaya gani?
Mi ninafikiri kwanza kuwa kijikanisa leo inaweza kukufanya miaka 50 ijayo uwe kanisa kubwa. Kama tungetumia jugdement anayotaka Kilaini na Gamanywa itumike miaka 100 iliyopita basi labda madhehebu makubwa kama RC, LUTHERAN nk yasingekuwepo leo. Je uhalali wao ni kwa vile wao walianza zamani au tuweke vigezo vya kupima mwelekeo wa kiimani na baraka yake kwa waabudu? Kama Martin Luther na Reformers wengine wangepimwa wakati wa vuguvugu la mabadiliko na kukosoa yaliyokuwa yamepinda yangeachwa mikononi mwa mapapa wa kikatoliki wangesemaje juu ya Reformers hawa? Bila shaka wangesema wauawe mara moja bila shaka. Je tunataka kurudi huko?
Pili ningependa kuuliza, kuna uhusiano gani kati ya kusajili kanisa na msamaha wa kodi. Maana si kila kanisa lililosajiliwa linapata msamaha wa kodi automatically. Kama kuna sababu yoyote ya kupata msamaha kwa ajili ya huduma unayoitoa kwa kawaida unaomba msamha for that particular issue. Hakuna kibali general cha msamaha wa kodi ambacho mtu anatembea nacho. Ili kupata msamaha lazima ueleze unachotaka kufanya au kununua au kuingiza nchini. Lazima useme huo mradi au shughuli unaifanyia wapi. Lazima mkuu wa wilaya husika athibitishe kuwa ni kweli uko katika wilaya yake na unayfanya unayodai kuyafanya. Wakati mwingine TRA watetembelea site ya shughuli hiyo na kuandika recommendation kabla ya kamishna kutoa huo msamaha. Sasa swala la usajili wa kanisa hapo linaingiaje?
Mpendwa kipimo kipi kitatumiwa na serikali kujua hili kweli kanisa na lipi si kanisa? Je idadi ya watu ndo calibration ya hiyo meter itakayopima hayo makanisa? Nadhani hayo yatakuwa si makanisa kwa maana ya kanisa bali NGOs, CBOs, or any other organizations. Jaribu kukubali ukweli bila kuweka hisia. Huoni kuwa Askofu Kilaini na Gamanywa hapo anatetea uhai wa Kanisa lake kwani serikali kutoa democracy ya kuamini chochote inawapa freedom wakatoliki na wapentekoste kuhama ukatoliki au upentekoste kwenda kwingine? Ndo maana siamini katika dini kabisa maana binadamu wachache wana monopolise dini kwa faida binafsi na kuacha agenda ya Mungu nje yaani Imani. Kama kweli Kilaini anaamini katika roho mtakatifu yeye anashida gani? maana Yesu alisema hataliacha kanisa mpaka ukamilifu wa dahari meaning anauwezo wakulilinda lisifutike sasa hilo lake mbona anataka kulilinda kwa nguvu ya kidunia badala ya kimungu? Kama Mungu yupo pamoja nae nani atakua kinyume nae? Na kama issue ni kodi kwani hata kanisa likiwa na watu milioni thelathini matapeli je hawata kwepa kulipa kodi? Je hata kama hao milioni thelathini ni waaminifu Askofu wao akawa tapeli je hilo kanisa halitakwepa kulipa kodi?
Kama mkristo na utata na hiyo kauli kama inatakia mema wakristo na aliye kinyume chetu ni adui yetu; kama imani yangu inavyonituma basi aelewe kuwa kuutumia ukristo kupinga ukristo ni kupinga nguvu za kristo mwenyewe na kwasababu hiyo sina wasiwasi roho mtakatifu atawashughulikia kwa haki kabisa na kama nia yao ni kupinga injili yakristo basi itadhihirika muda si mrefu. maana injili ni habari njema kwa watu wote tena inanguvu hata kuleta uwokovu kwa yeyote aaminie kwa Myunani kwanza na kwa mataifa mengine pia. Hii inamaana ya kuwa yeyote mwenye habari njema ya upendo wa Mungu wa kweli haijalishi unajina gani Juma, Rajul, Tsetung, Masanja, etc huo ujumbe wako uta prevail no matter what maana unapeleka upendo wa Mungu kwa wasioujua huo upendo bila kujali umesoma, hujasoma, mfupi, mweusi, mweupe mnene, mwembamba, unaheshimiwa, unadharauliwa etc. Na habari njema ni hii kuwasaidia maskini, kuwatetea wanyonge, kuwafungua waliofungwa na nguvu za giza kama ufisadi, uchawi, uzinzi, ulevi etc, kuwapa matumaini waliokata tamaa na kutangaza nguvu za Mungu jinsi zinavyoweza kuondoa yote hayo. Ila kuna ziada katika kufanya hilo uwe na ile nguvu ndani yako yaani ukisema umaskini kesho utakwisha Tanzania na iwe kama utakavyosema bila hivyo wewe ni mwongo na unambeba shetani ndani yako kwakujua au kutokujua na kazi ya huyo ni kuiba, kuharibu na kuua.
So kanisa la leo la kristo kama ninavyoamini mimi wewe linaanzia kwa mtu binafsi meaning number sahihi ya kanisa ni mtu mmoja, akitokea mwenye mawazo kama yako anakuwa wapili and so on ili mpeleke hiyo habari njema hapo juu mkipata msamaha wa kodi Mungu ashukuriwe msipopata hewala, mmepewa sadaka asante Yesu mmenyimwa Mungu abarikiwe yaani mtumwa asie na faida ukiona mnaanza kugombana kwaajili ya kodi na sadaka na namba za watu mjue hapo wala hakuna injili kuna njaa tu na nibora mkafanye kazi mpate uhalali wakula vyakwenu kwakujinafasi.
Kusajili kanisa na misamaha ya kodi kuna uhusiano kwa sababu makanisa ni beneficiary wa misamaha ya kodi. Vile vile huo utaratibu unaouzungumzia upo lakini imethibitika kuwa utaratibu huo kuna watu wanaukiuka ndo maana Mkulo akafikiria kuifuta hii misamaha. Watu wanamwambia kwa nini asiwakamate hao wanaoutumia vibaya utaratibu huo au wasizuiwe kufaidika? Tatizo ni gharama za kuziba mashimo ambayo unajua kila ukipita leo mwenzio anapita kesho kuchimba mashimo.
Suluhisho si kuendelea kuziba mashimo; ni ama upambane na anayeyachimba au utengeneze kiasi kwamba hawezi kuchimba! Naamini kuzuia kabisa matumizi yasiyo halali ya misamaha hii, ni kuiondoa kabisa isiwepo. Full stop. Misamaha ikiendelea kuwepo, kila mtu atajiuliza afanyeje ili kunufaika na misamaha hiyo? Ndo issue ya usajili wa makanisa inapokuwa issue.
Pendekezo la wengi ni kujaribu kuziba mianya inayotumiwa na watu kunufaika na misamaha ya kodi isivyo halali. Lakini uzoefu wetu kama nchi unaonesha kuwa kitu hicho ni kigumu mno. Kila unapoweka taratibu, wenzio wanafikiria jinsi ya kuzivunja.
Njia bora kabisa ni kusema kila mtu na alipe kodi!! Kila mtu na ajue kodi ipo na itabidi ilipwe. Kama anatoa msaada na huo msaada hawezi kuutoa ikiwa atalazimika kulipa kodi, na aache!! Hilo itakuwa rahisi kulisimamia kwani kutolipa kodi kwa aina yoyote itakuwa ni kuvunja sheria. Kodi itaheshimiwa na kila mtu.
Kuwepo kwa utaratibu ambao baadhi ya watu au taasisi zinazoonekana kuwa ni safi kustahili kulipa kodi, ndo kunafanya tutunge sheria zinazowaondoa viongozi kwenye wigo wa kodi. Maana yake kodi inaonekana ni kitu wanachostahili kulipa watu wachafu tu. Watu wakubwa kama wabunge na marais, malipo wanayopewa mengi yasikatiwe kodi.
Tulipe kodi wote na tulipe!
Tatizo ni moja. Kufukuzana na wakwepa kodi kwa kutumia mianya iliyopo ni ngumu sana na ni gharama ku-enforce. Hilo tunaonekana kutolizingatia. Hatuwezi kufanikiwa asilimia mia moja hata tukisema kodi ni compulsory. Lakini tunapunguza uwezekano wa watu kuibua visingizio hivi na vile. Tena inakuwa rahisi na cost effective kunapokuwa na sheria rahisi ya kodi.
Unapoanza kuweka taratibu hizi na zile za kuwaepusha baadhi ya watakatifu na balaa la kodi hapo ndo unapoanza kuharibu. Kwanza tatizo litaanzia hapo hapo, tafsiri halisi ya nani anastahili kupewa misamaha hiyo na kwa shughuli gani. Haya yote yanafanya zoezi zima la utozaji wa kodi kuwa complicated na la gharama pia.
Ndo maana naona wote tuguswe na mkono wa kodi. Hao ng'ombe wasiochinjika ndo tatizo.