Ushauri wa Kilaini ni mbovu haukuzingatia ukomavu wa kiuongozi kwa kiongozi mkuu kama yeye
1.Kwa kiongozi aliyekomaa kiungozi ukidai kitu ukapata inabidi unyamaze usiendelee na kidomodomo.Aliomba kodi iondolewe imeondolewa na serikali ilibidi baada ya kutimiziwa alichotaka anyamaze asiendelee na kidomodomo kwa mtu mkomavu kiuongozi.
Totally disagree with you. Yaani Kilaini atulie eti kwa sababu kapewa alichokuwa anaomba? so unataka kuniambia Serikali iliwa blackmail viongozi wa dini wasipanue midomo yao?
Mkuu hizi ni fikra ni za kibinafsi sana...eti ukipewa unachoomba hutakiwi upanue mdomo wako tena? Kwa nini basi unawalaumu viongozi wanapokea rushwa na kuwasaliti wananchi kwa kukaa kimya badala ya kuendelea kuikemea serikali?
2.Utafiti nilioufanya kwa makanisa madogo nchi mbalimbali duniani hukataa kusajiliwa na serikali kwa sababu huamini kuwa Mungu na kaisari (Mtawala) ni vitu viwili tofauti.
Acha kutudanganya hapa mkuu......umefanya utafiti nchi zipi, na makanisa madogo yepi mkuu....tupe hiyo repoti ya utafiti sio blabla mkuu! Eti makanisa hukataa kusajiliwa na serikali......hii itakuwa true endapo nchi hizo zinaendeshwa kwa misingi ya kidini na si nchi kama Tz ambayo serikali yake haiendeshwi kwa misingi ya dini and so kila taasisi inayofanya shughuli yoyote lazima itambuliwa na serikali ili kuweza kuwalinda raia wake!
Na kwa misingi Hiyo ya utofauti wao hulipa kodi zote serikalini kama Yesu alivyowaagiza kuwa mpeni kaisari kilicho chake kaisari (kodi} na mpeni Mungu kilicho chake Mungu (sadaka).Wao hawaigusi serikali na serikali haiwagusi kila mmoja huheshimu mipaka yake.
Hili mbona liko wazi mkuu....nani anabishia hapo?
Sasa serikali ilikuwa inalia ipewe chake wakatoliki hawataki kulipa cha kaisari (kodi) na wanaona fahari kutomlipa kaisari chake (kodi).
Khaam mkuu sasa unazidi hata kama una chuki binafsi na RC this is too much! Mkuu ni ukweli kwamba hili sakata linawahusu wakatoliki tu...na unaongezea ...wanaona fahari kutomlipa kaisari chake....is this true? ndo RC walivyokwambia?
Makanisa mengi madogo kwa taarifa yake Kilaini hayo anayosema yana watu wachache mengi hayana mpango wa kukwepa VAT. hujenga majengo yao bila kuomba misamaha ya kodi kwenye vifaa vya ujenzi na wala hawana mpango wa kuomba VAT iondolewe.
Makanisa mengi yapi si uyataje ili tuyachambue vizuri.......eti hayana mpango wa kuomba VAT iondolewa......iondolewe mara ngapi wakati sheria ilishaondoa na wakiuziwa bidhaa bei huwa VAT exclusive?......eti hawana mpango wa kuomba VAT iondolewe ....iondolewe kutoka wapi tena wakati sheria ilishaiondoa?
Iwe simenti,nondo,baisikeli,magari,vinanda,magitaa n.k huvinunua na VAT zake hivyo hivyo na hawataki kuomba msamaha wa kodi kutokana na imani yao ya kidini kuwa lazima kodi ilipwe kama Yesu ALIVYOAGIZA.
Wewe unaijua vizuri jinsi sheria ya VAT 1997 inavyofanya kazi? Anybody supplying goods or services to the VAT relieved person is not supposed to charge VAT.......religious organisations ni relieved from paying VAT so they are enjoying this benefit kimyakimya.....need we say more on this!
Labda yeye Kilaini na usomi wake atueleze ni kwa mamlaka gani aliyonayo aweza kataa kulipa kodi wakati Yesu mwanzilishi wa kanisa alilipa kodi.
Ebu nionyeshe wapi na lini Kilaini amekataa kulipa kodi na pia niambie mamlaka husika kwa nini hazijamchukulia hatua kwa kufanya hivyo?
Huo unafuu wa kusamehewa kodi kautoa kitabu gani cha biblia au kaupata wapi?
Mkuu nchi hii haiendeshwi kwa vifungu vya biblia inaendeshwa na sheria za nchi mkuu. Mbona hujiulizi wa kati huo huo, kifungu gani kinasema hawa kina Kilaini kutoa huduma za kijamii chini ya Caritas, mahospitali, mashule, orphanage centres, miradi ya maji kwa wananchi wote.....and they have been very successiful on this side. Kutoa huduma za kijamii ni jukumuu la na Kanisa? wanatekeleza hayo majukumu kwa niaba ya serikali kwa ujira upi sasa......please try to think out of the box...sio bible bible tu mkuu!
.......yeye kilaini na papa benedicto ni akina nani wasilipe kodi?
Eeeh mkuu...kweli umedata....nilifikiri utaishia kwa Kilaini.....sasa Benedict anatuhusu nini kny mjadala huu hapa....kama sio chuki binafsi na RC? Yaani umeshidwa japo uwataje, KKKT,Anglican, Mashekhe waliokutana na PM pale Dodoma na kukubaliana kudatilisha uamuzi wa kuondoa misamaha, ukamtaje Pope.....kweli RC inakuudhi mchungaji!
Kanisa linalokiuka hata maagizo ya Bwana wao la kutaka walipe kodi na halitaki ni hatari.
Wewe kama sio RC unamjua bwana wao alisema nini, unaijua misingi ya RC wewe kama sio muumini wake? Acha kupayuka ndugu yangu huijui RC hata kidogo.....wivu tu.
BWT: Unakaribushwa kuwa muumini wa RC if you like mkuu.
Napendekeza kanisa katoliki lifutiwe usajili au likubali kulipa kodi kama Yesu alivyoagiza ili liendelee kutambuliwa kama kanisa na si genge la maharamia wakwepa kodi ya VAT waliojificha nyuma chini ya altare ya kanisa ya kugawia sakramenti.
Acha mnkari mkuu, usajili wa RC Tanzania utafutwa si kwa shinikizo lako bali tu kama itagundulika kuwa linakiuka sheria na taratibu za nchi. Lakini ni kuhakikishie kama kilio chako ni kuua ukatoliki...ha!ha!ha! ukatoliki ni imani ya watu ambayo imekuwepo miaka nenda rudi.....so sisi tutapita ukatoliki will be there to stand kama zilivyo imani nyingine!
Unaita RC ni genge la maharamia....is this true kweli mkuu?
Kushambulia makanisa madogo kayaonea na mimi kama mpiganaji wa porini AMBAYE NI SAUTI KWA WASIO NA SAUTI nasema hapana.
Narudia tena...ukirejea tundiko la Cynic Kilaini alitoa tu mfano ....na hakusema eti makanisa yote madogo yasisajiliwe ndugu yangu
Hongereni.Nyie mtaenda huko mnakoita mbinguni na Kilaini na wenzie wataenda gizani jehanamu kwenye kona yenye moto mkali siku ya kiyama kwa kukataa kumpa kilicho chake kaisari(VAT) kama Yesu alivyoagiza.
Heee..!
Netanyahu kesha kuwa Hakimu mwandamizi wa sir GOD....? yaani tayari unauwezo wa kujua nani na nani wataenda heaven .....please if you don't mind advise mi taenda upande upi?.....i guess kule uliko mpeleka Kilaini sio?
Kilaini alipaswa ajue kuwa Kutolipa VAT siyo kitu cha kuchekelea kwa makanisa yote kama ilivyo kwa Lutheran,Angilikana,katoliki na hicho kinachoitwa Baraza la makanisa ya wapentekoste cha akina Askofu Mwasota
Heh...kumbe na wengine wapo?
Kwa makanisa mengi madogo kukataa kukataa kulipa kodi kama VAT ni upotofu wa kiimani.Na ndio maana waliamua KUJITENGA NA kuanzisha yao yenye waumini wachache lakini wenye nidhamu ya hali ya juu ya kulipa kodi zikiwemo za VAT wakipinga mfumo wa kishetani ndani ya makanisa makubwa yaendayo kinyume na Yesu alivyoagiza.
Taja hayo makanisa matakatifu mkuu.....mbona unauza chai tu?