Askofu Kilaini achemsha kwa ushauri huu!


Hiyo ''experience'' ameipata baada ya Waziri Mkulo kutangaza kuwatoza kodi? Kilichomsukuma kutoa tamko sasa hivi na siyo kabla kiko wazi tu.
 
Tutajuaje kama kanisa flani ni la ukweli na kanisa flani ni la uongo? Kwa idadi ya waumini?

Hapa hoja kubwa kwa upande wa serikali si kujua kanisa lipi ni la kweli na lipi ni uwongo.....! Kama zilivyo taasisi nyigine inachotakiwa kujua ni je, hayo yanayojiita makanisa yanafuata sheria za nchi? Kama ndiyo hakuna shida...shida zinaanza pale ambapo makanisa hayo yanaanza kukiuka taratibu zilizopo na kuvunja sheria!
 
Mwanaluguma, hebu nipe link kati ya ''ukibwetere'' na ''idadi ya waumini + kusamehewa kodi". Sioni.

Hajasema habari ya idadi ya waumini. Anachozungumzia hapa na ndicho haswa moyo wa mada ni kuratibu shughuli za haya makanisa yetu ili kujua mwenendo wake unaendana na madhumuni ya kuundwa kwake...(ikiwemo kuhakikisha misamaha ya kodi haitumiki vibaya) Sasa kwa sababu mnazozijua wenyewe mmeamua hii mada kuichukua na kuipeleka 'kusikojulikana' na kuingiza hoja ambazo hazipo.
 
Hiyo ''experience'' ameipata baada ya Waziri Mkulo kutangaza kuwatoza kodi? Kilichomsukuma kutoa tamko sasa hivi na siyo kabla kiko wazi tu.

Ndg unaonekana husomi hata unacholeta hapa jamvini. Hebu soma hii sehemu:

..miaka ya tisini, tatizo hilo lilionekana na serikali iliahidi kushughulikia makanisa hayo, lakini leo serikali inayaandikisha ovyo tu na katika muungano wa makanisa hayamo

Ina maana hili suala limekuwa likifuatiliwa kitambo, na sasa serikali inakumbushwa wajibu wake baada ya kukurupuka na kukimbia wajibu wake wa kuratibu shughuli za makanisa yote na hivo kubaini yapi yanaendeshwa ndivyo sivyo, na kutaka kuya-penalize wote bila ya sababu ya msingi.
 
No. Ni wewe mwenyewe ulibaki square one. Mimi nipo square two. Nasema kwamba matamshi ya Askofu Kilaini kwamba taasisi za kidinii zichujwe wakati wa kuandikishwa yanakinzana na uhuru wa kuabudu unaotolewa na katiba.

Taasisi za dini zinachujwa mazee..hiyo sio option. Sheria inataka hivyo na ndio maana huwezi kuunda kikundi chako kiholela bila kujulikana kwenye mamlaka husika. Ukienda kujiandikisha lazima ukidhi vigezo na huko kama ndiko unakokuita kuchujwa basi hiyo ndo maanake. Sielewi unachopinga hapa maana kila kitu kiko wazi, ndoa huandikishwa kuwa halali, bendi za muziki zinaandikishwa BASATA, makampuni BRELA and the list goes on and on. Hili halikwepeki.
 
By the way kudhibiti au tuseme ku-monitor taasisi zote ikiwemo dini zote ni kazi ya serikali. Hivi mnakumbuka kilichotokea Uganda mwaka 2000 wakati Kibwetere alivyoteketeza watu na kutoweka. Serikali ya Uganda ilijuta sana kwa hili maana haiku-monitor mwenendo wa makanisa. Mnakumbuka sakata la Gayana miaka ya 1970? Hakuna Demokrasia isiyo na kikomo.

Mwaka jana huko USA wachungaji wa makanisa ya kilokole wamewekwa kiti moto na Congress kwa kufuja pesa za waumini wao kwa kuishi kifahari kupindukia na huku wakipewa misamaha ya kodi na serikali? Congress inataka makanisa ya namna hiyo yadhibitiwe vilivyo. Hivyo Kilaini hayuko mbali na hili.
 
 
 
Hapa umepiga ikulu, ila subira sasa wenyewe waje!
 
Ndugu unasema kweli juu ya mambo ya ulipaji kodi, lakini kuna jambo moja unalojisahau: na wakati bajeti zinasomwa jamani tuwe makini kuangalia comments zinazotolewa na wataalam wa mambo ya fedha na washauri wa serikali juu ya mambo yanayohusu bajeti na kodi za kila aina.
Baada ya bajeti kusomwa, kuna tax manager mmoja wa PriceWatehouse Coopers Tanzania aliandika swala juu ya mada hii. Iko hivi:
Sababu ya Serikali kukusanya kodi kwa namna yoyote na katika vyombo vyovyote ni ili iweze kutumia fedha hizo kuleta huduma katika jamii. Kila Mtanzania anafahamu namna ambavyo madehebu ya kidini yalivyosaidia serikali kuleta huduma, na pia huduma nyingi bado zinatolewa na madhehebu ya kidini karibu asilimia 45 ya huduma za kimaendeleo, waweza kuzitaja tu hapa, mashule, mahospital, vituo vya mayatima, vituo vya ufundi stadi na mengine labda unayafahamu zaidi. Wakati madhehebu mbalimbali ya kidini yanapata msamaha wa kodi, ni kwa sababu vifaa vinavyoingizwa vinaenda moja kwa moja kutumika katika mambo hayo yaliyotajwa.
Tunaposema kwamba madhehebu ya kidini yalipe kodi, (na hii sio kwa Kanisa Katoliki tu ndugu yangu kwa sababu, baada ya muda kidogo, mashehe wataongea, wachungaji wataongea pia kuhusu swala hili, ni kwa vile tu Kilaini ameanza kuongea, lakini wote walikuwa wanapata msamaha wa kodi). Serikali inaposema walipe Kodi, ina maana kwamba serikali sasa itachukua mzigo wa kutoa huduma zote hizo ambazo madhehebu ya kidini yalikuwa yakizitoa, kwa sababu wamelipa kodi, na fedha hiyo sasa inapaswa kufanya kazi yake kama jinsi inavyofanya kupitia makanisa na madhehebu mbalimbali.
Kwa bahati mbaya, nafasi hii serikali iliyotoa kwa madhehebu mbalimbali kupata msamaha wa kodi imechezewa na baadhi ya madhehebu, kwa kupitia msamaha huu, wengi wamejiingizia mali za kila aina kwa kupitia makanisa yao kwa faida zao na familia zao, and I guess this is what upsets the government, na hata viongozi wa dini ambao wanafanya juu chini kuona huduma zinawafikia wananchi. Hii ndio sababu iliyomfanya Kilaini akaongea.
Pili: Ningependa mjadala huu uelekezwe zaidi kwenye swala la kodi, kwa sababu ndilo swala linalojadiliwa hapa wala sio ni dini ipi ya kweli au kanisa lipi la kweli au linafuata maandiko, kumbukeni tupo kwenye jamii forum, na inaitwa Home of Great Thinkers! Kama mnataka tujadili swala la maandiko, toeni topic hiyo ili great thinkers waanze kazi ya kuandika..
 
Hapa umepiga ikulu, ila subira sasa wenyewe waje!

Amepiga ikulu ya wapi? Mambo mengi ni off-topic na pumba zisizohusiana na mada. Ila tulia keti kitako na usipagawe tutakapoanza kujibu hoja kwa hoja, na pumba kwa pumba..
 

You said it all baddy!
 
Amepiga ikulu ya wapi? Mambo mengi ni off-topic na pumba zisizohusiana na mada. Ila tulia keti kitako na usipagawe tutakapoanza kujibu hoja kwa hoja, na pumba kwa pumba..
Kwani na wewe ni miongoni mwao... Au kimbele mbele kimekushika!?
 

I think you are missing the point. Swala si kurudisha misamaha ya kodi. Swala ni nini kilipelekea mpaka serikali ikatoa misamaha hii kwa dini . nk. Kama hakuna ufumbuzi wa tatizo hili huko mbeleni serikali itaja toa tena. Ndio maana Askofu Kilaini anaitaka Serkali iwe makini na hao makajanja katika kuangalia "who is genuine and honest and who is not" Nazi moja au mbili mbovu zisiharibu uzuri wa nazi zilizo nzima. Kukua au kutokuwa sio issue, swala ni kufuata utaratibu. Mnakumbuka yaliyotokea Uganda 2000? Jina la Kibwetere bado mnalikumbuka? Ndio makajanja anayosema Askofu Kilaini.
 

Salale! This is a fallacy. Inaonekana huelewi tatizo ktk dimension zake. Tukumbushane tu kuwa hii ishu inahusu ukwepaji kodi kwa jina la Mungu. Hii si tu inaleta madhara kwa mapato ya serikali bali pia inaleta picha mbaya kwa makanisa yote na kulitweza jina la Mungu kwa namna moja au nyingine. Baada ya serikali kurudisha misamaha ya kodi bila kusema itachukua hatua gani , ni haki kwa mtu aliyeliona tatizo kuzungumza kama alivyofanya Kilaini. Sielewi unawezaje kushindwa kuliona hili. Sielewi ukomavu unaouongelea ni ukomavu gani huenda labda unayo definition yako ya neno ukomavu na kidomodomo..zile zetu standard tunaona hazi-apply hapa
 

Mazee ingependeza ungeleta huo utafiti na huko ulikofanyika ili tuujue na tuufanyie kazi kitaalamu. Suala la kulipa kodi au kutolipa ni makubalino na masikilizano kama taifa na kuona nini kifanyike kwa ajili ya manufaa ya wananchi wa taifa husika. Kama Tanzania tumeona utaratibu wa kusamehe kodi ni mzuri na unaifaa jamii yetu hakuna ubaya na wala si dhambi kuendelea kutumika. Hivyo hoja kuwa kwa kuwa nchi X makanisa hulipa kodi zote haimaanishi utaratibu huo utaleta matunda hapa Tanzania. Ni vyema tukajua kila nchi ina mazingira tofauti, huduma za kijamii tofauti, na vipato vinatofautiana..kuna mambo mengi ya kuzingatia..

Mwisho, kwa kumalizia hii hoja, ule mfano wa Bible haumaanishi kumpa Kaisari yaliyo ya Kaisari na Mungu yaliyo ya Mungu haulengi kwenye mambo ya pesa kama unavyo-suggest. Ule msemo ni wa kiroho zaidi na kama wewe sio mmojawapo wa walioamini ukaacha kupotosha maana inayokutikana mle.
 

Ok, Kilaini amesema kuna makanisa yameandikishwa na serikali na wala hayajajiunga na 'muungano wa makanisa' na serikali pia inalalamika kuwa makanisa yanatumia vibaya misamaha ya kodi, hii ina maana kuwa serikali haiyajui hayo makanisa 'madogo' ambayo mimi nayaita ya 'mfukoni', ila wewe sijui uliyapata wapi na wakakueleza kuwa hawana mpango wa kukwepa VAT...!

Hili suala la kuhusisha idadi ya waumini na kanisa tuliomba hapahapa jamvini tuwekane sana..je sheria za kuandikisha makanisa zinataja idadi ya chini ya waumini ni wangapi ili kuandikishwa ..hili suala halijajibiwa na matokeo yake watu mnarejesha pumba zilezile na kulichosha jamvi kwa maneno mareeeeefu yasiyo na ushahidi..

Pia naona unashupalia sana kuwa eti Yesu alisema tulipe KODI! Lakini kadr unavyozidi kuishupalia hii ishu ndivyo hivyohivyo unavyozidi kuonesha hukuelewa kadhia nzima. Hivi labda nikuulize ni kanisa lipi ambalo Yesu aliagiza lilipe kodi kipindi kile? Maana nijuavyo kanisa limeanza kitambo baada ya Yesu kutoweshwa duniani.

Bible niliyonayo inasema watu wa walimuendea Yesu kumtega akiwa karibu sehemu ya kuabudia na kumuuliza je tulipe kodi kwa serikali ya kikoloni ya Kirumi? Walimuuliza hivo wakitegemea kuwa awajibu msilipe bali lipeni hekaluni ili wampikia jungu kwa mamlaka..From religious point of view tunasoma kila mamlaka imetoka kwa Mungu, na Yesu hapo aliwaambia mlipeni Kaisari kodi kwa kutumia hii premises. Pia aliwaambia mlipeni Mungu yaliyo yake ikiwa na maana yaliyo yake ni vile matakwa ya Kimungu, sio tu kuhusu kulipa zaka na sadaka. Kumpa Mungu yaliyo ya Mungu ni kuishi matakwa yake, na kumpa Kaisari yaliyo yake ni kutii mamlaka zilizopo. Mambo ya pesa ni subset tu. Sasa kwa misingi hii basi suala kuwa Yesu aliagiza tulipe kodi ni wewe umetafsiri na wala sio uhalisia wa mambo.
 

Nafikiri kama nilivyoonesha hapo juu, hoja yako kuhusu Yesu aliagiza tulipe kodi is VERY MISPLACED. Ni vyema kama hujui watu wengine wanaamini nini vyema ukaketi kitako ukabakia mtazamaji badala ya kuleta vioja. Yesu alilipa kodi kama Yesu na sio kama kanisa, wafuasi pia walilipa kodi kama wafuasi na sio kama kanisa. Na wakatoliki wote popote walipo kama individuals wanapaswa kulipa kodi zote zilizoamriwa na mamlaka halali, na sijasikia popote ambapo Kanisa Katoliki limewazuia watu kulipa kodi...Sasa mazee kabla hujarukia kitu tanguliza busara mbele.
 

Mazee umesema kweli wewe ni mpiganaji wa porini. Ukiwa porini sometimes unashindwa kupata enlightment inayopaswa kurutubisha akili ili kuji-update na ulimwenguni huu uendao kwa kasi.

Point yako kuhusu makanisa madogo ni void, kama nilivyokwisha kuonesha hapo juu.

Point yako kuhusu Yesu kuagiza kulipa kodi pia ni void kama nilivyokwisha hap juu.

Natarajia utatoka huko porini ulipo upagane vita ya kujikomboa kifikra.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…