Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Dk Msafiri Joseph Mbilu,amewataka waumimi na Watanzania kwa ujumla kujiepusha kuchukua rushwa kwa wanasiasa wanaotarajia kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kwenye uchaguzi ujao na wasiwachague.
Akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa tano baada ya Jubilee ya Miaka 125 ya Injili uliofanyika Magamba wilayani Lushoto mkoani Tanga kwa siku tatu na kuhitimishwa leo Aprili 5,2025 Askofu Mbilu amesema moja ya jambo kubwa ambalo wananchi wanatakiwa kujiepusha nalo ni kushawishika kupewa rushwa,ili kuwapa nafasi wagombea badala ya kupita kwenye mifumo sahihi.