Askofu Malasusa ameigeuza KKKT kuwa jumuiya ya CCM

Inasikitisha na inahudhunisha sana Askofu mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), ndugu Alex Malasusa, ameligeuza kanisa hili pendwa kuwa kama jumuiya ya CCM. Wakati alipokuwa kwenye nafasi ya uaskofu mkuu kwa mara ya kwanza, Askofu huyu ambaye ni kada maarufu wa CCM, alifanikiwa kupenyeza aya kwenye vitabu mbalimbali vya kanisa zinazoisifu, kuiombea na kuitukuza serikali ya CCM.
View attachment 3641865

Ndugu Alex Malasusa, kada maarufu wa CCM
Kana kwamba hilo halitoshi, kwenye aya hizo kuna maneno yanamuombea Rais, Wakuu wa Mikoa na Wilaya na viongozi wote wa nchi hii. Cha ajabu zaidi, hata baada ya mauaji ya MO29, bado askofu huyu ameendelea kuhimiza wachungaji, wainjilisti na waumini kumuombea Samia na “serikali” yake wakati inajulikana fika siku ya Oktoba 29, 2025 hakukuwa na uchaguzi bali mauaji ya raia wasiokuwa na hatia na uporaji wa uchaguzi.

MAONI YANGU
Wakati umefika waumini kuchukua hatua stahiki kukomesha ujinga huu unaofanywa na Askofu Malasusa ndani ya kanisa la KKKT. Anapaswa akumbushwe kwamba hili kanisa ni taasisi inayojitegemea na kwamba lilikuwepo kabla yake na litaendelea kuwepo hata baada ya yeye kuondoka. Asije akadhani kwamba KKKT ni mali yake na ya familia yake.

Natoa rai kwa waumini wa dhehebu hili kumshikiza adabu, hata ikibidi kwa njia ngumu, kwamba KKKT haiwezi kutumiwa kwa misingi ya kisiasa na kwa faida ya familia moja tu, huku maelfu ya waumini ambao wapendwa wao waliuliwa Oktoba 29 bado hawajapewa miili ya ndugu zao wakazike. Tena jina la Samia linapotajwa mara kwa mara ndani ya kanisa linawakasirisha sana ndugu na jamaa waliowapoteza wapendwa wao wasiokuwa na hatia siku ya mauaji ya halaiki (Oktoba, 29).

Ujinga huu huwezi kuusikia ndani ya kanisa katoliki au makanisa mengine yanayojitambua. Unasikika tu ndani ya KKKT na ndani ya kanisa la Mwamposa, ambao ni machawa na vibaraka wakubwa wa CCM.

Nawasilisha.
​
Huyu mzee sijui amekuja kuwaje siku hizi. Ukiwaleta watawala ndani ya kanisa lazima uwalambe miguu ili ukae nao sawa na kuwanyenyekea ili upate michango. huo ujinga katoliki haupo.
 
Huyu askofu hovyo sana
 
Huko Loliondo waumini wa KKKT waligoma kusali ndani ya kanisa wakipinga wizi wa sadaka zao unaofanywa na watu wao wa mungu wamjuae.
 
Ajabu ni kwamba KKT wana mali, mahospitali na Taasisi za Elimu ila bado mnawaita Chawa
Sasa kama wanafanya uchawa kwa CCM, umiliki wa hospitali unawaondolea uchawa mkuu?
 
Huyu mzee sijui amekuja kuwaje siku hizi. Ukiwaleta watawala ndani ya kanisa lazima uwalambe miguu ili ukae nao sawa na kuwanyenyekea ili upate michango. huo ujinga katoliki haupo.
Kanisa Katoliki halina upumbavu kama huo mkuu. Haya makanisa ya mchongo ndiko kuna shida.
 
Mtoa mada sio MKKKT hiyo ya kuombea serikali ipo kitambo sana hata Malasusa hajui kama atakuwa Askofu.

Huwa wanaweka jina la Rais kutegemea nani ni Rais wa Muda huo.

Ila sikubaliani na hizi tetesi za kulipa kanisa kuu mamlaka ya kubadili Askofu wa Jimbo.
 
Wenye afya hawahitaji tabibu bali walio wagonjwa. Kuna kuombea ili mgonjwa apone na kuna kuombea walio na afya waepushwe na maradhi.
Ndiyo maana mnahimizwa kuomba bila kukoma na tena bila kuchoka maana maombi ya pande hizo kuu mbili.
Mume mlevi na aliyetekeleza familia bado ana haki ya kuombewa na akaweza kuponywa na maombi ya mkewe ili arejee katika viwango vya Baba na Mume bora
Mume mlevi...
Na Mke Mlevi Je..??​
 
Mtoa mada sio MKKKT hiyo ya kuombea serikali ipo kitambo sana hata Malasusa hajui kama atakuwa Askofu.

Huwa wanaweka jina la Rais kutegemea nani ni Rais wa Muda huo.

Ila sikubaliani na hizi tetesi za kulipa kanisa kuu mamlaka ya kubadili Askofu wa Jimbo.
Kwani hawo KKKT hawafahamu kwamba serikali ya Samia ni haramu? Kwanini waiombee serikali haramu ambayo haikuchaguliwa na wananchi? Wana maana gani?
 
Cha mlevi (KKKT) huliwa na mgema (CCM).
 
Kwani hawo KKKT hawafahamu kwamba serikali ya Samia ni haramu? Kwanini waiombee serikali haramu ambayo haikuchaguliwa na wananchi? Wana maana gani?
Uchaguzi ulifanyika hakuna serikali haramu.
 
Back
Top Bottom