Sijapewa username bado
JF-Expert Member
- Aug 15, 2024
- 1,775
- 2,891
Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk Alex Malasusa amewataka Watanzania kumlilia Mungu ili roho za uovu dhidi ya watu wengine zipotee, huku akiwasihi kumuombea Padri Charles Kitima aendelee kuimarika kiafya.
Padri Kitima ambaye ni Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), alishambuliwa katika eneo la Kurasini, Temeke jijini Dar es Salaam, zilipo ofisi za makao makuu ya TEC.
Akizungumza leo Jumamosi Mei 3, 2025 jijini Dar es Salaam, Dk Malasusa amesema kitendo alichofanyiwa Padri huyo kinaumiza na kinaashiria kuwepo kwa roho za uhasama miongoni mwa watu, hivyo ni wajibu wa Watanzania kusimama katika maombi ili taifa liendelee kuwa na amani.
Aidha, ametoa rai kwa Watanzania kuendelea kuliombea taifa kwa ujumla wake, akisema ni kupitia maombi ndipo hali ya utulivu na mshikamano inaweza kuimarika katika jamii.
Soma pia: Ukimya wa Mkuu wa KKKT, Askofu Alex Malasusa tukio la Padri Kitima unatia shaka