carbohydates
JF-Expert Member
- Oct 13, 2026
- 260
- 607
Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Alex Malasusa, ameitaka Serikali kusimamia sheria za kudhibiti matumizi ya pombe kupita kiasi, akisema ulevi unatishia nguvu kazi ya Taifa.
Wakati Askofu Malasusa akieleza hayo, aliyewahi kuwa mwenyekiti Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, amelalamikia baadhi ya watumishi wa umma wanaokwamisha maendeleo kwa sababu za kisiasa.
Viongozi hao wamesema hayo leo, Novemba mosi, 2026, katika ibada ya uzinduzi wa kanisa jipya la KKKT Nshara Machame, mkoani Kilimanjaro, iliyohudhuriwa na Waziri Mkuu, Dk Mwigulu Nchemba, aliyekuwa mgeni rasmi kwa niaba ya Rais Samia Suluhu Hassan.
Akizungumza katika ibada hiyo, Askofu Malasusa amesema matumizi ya pombe kupita kiasi, hasa miongoni mwa vijana, yanaweza kudhoofisha nguvu kazi na kuathiri maendeleo ya Taifa.
Amesema Serikali inapaswa kuhakikisha sheria zinazodhibiti ulevi zinatekelezwa ipasavyo, huku jamii ikiwajibika kuwakinga vijana dhidi ya tabia zinazoweza kuathiri maisha yao.
“Nasema kwa upendo kabisa, Waziri Mkuu, tusaidieni. Muone kama kuna uwezekano wa kutenga muda na kushughulikia suala hili ili tusije tukawa na Taifa lenye walevi. Sijawahi kuona Taifa lililofanikiwa likiwa na walevi,” amesema.
Askofu Malasusa amesema ulevi ni miongoni mwa sababu zinazotajwa katika ajali za barabarani, ambazo athari zake huwakumba watumiaji wengine wa barabara na familia zao.
Chanzo : Mwananchi.