5523
JF-Expert Member
- Nov 13, 2014
- 2,275
- 2,410
Askofu Mkuu wa Canterbury ametangaza kujiuzulu wadhifa wake kufuatia ripoti ya kulaaniwa kuhusu mnyanyasaji mkubwa wa watoto anayehusishwa na Kanisa la Uingereza.
Uchunguzi uligundua kuwa Justin Welby, 68, "angeweza na alipaswa" kuripoti unyanyasaji wa John Smyth kwa wavulana na vijana kwa polisi mnamo 2013.
Katika taarifa, Bw Welby alisema kuwa "ni wazi kabisa kwamba lazima nichukue jukumu binafsi na la kitaasisi" kwa majibu yake baada ya kuambiwa mara ya kwanza kuhusu unyanyasaji huo.
"Ninaamini kwamba kujiondoa ni kwa manufaa ya Kanisa la Uingereza."
"Natumai uamuzi huu unaonyesha wazi jinsi Kanisa la Anglikana linaelewa kwa uzito hitaji la mabadiliko na kujitolea kwetu kwa kina kujenga kanisa salama.
Msemaji wa Waziri Mkuu Keir Starmer alisema "anaheshimu uamuzi ambao umechukuliwa na kuwa yuko pamoja na waathiriwa wote".
Haijabainika mara moja ni lini askofu huyo mkuu ataacha wadhifa wake lakini huenda mchakato wa kumpata mtu mwingine ukachukua takribani miezi sita.