Askofu Michael Msonganzila wa Jimbo la Katoliki Musoma ameeleza kuwa Wananchi waliomba Uchaguzi wa amani lakini imekuwa tofauti watu wengi wamepoteza maisha mbaya zaidi hata wasio na hatia waliokuwa majumbani mwao na wengi kujeruhiwa
Askofu Msonganzila ameongeza kuwa nchi inanuka imepakwa mavi na yawezekana wauaji walipewa order kuua lakini kwanini mtu auwe, hii siyo mila na desturi ya Tanzania kwani ni ngumu sana kurejesha heshima ya Taifa iliyojulikana ya amani na kuwa ya mauaji
"Tumechafua, tumeinyea nchi yetu, inanuka mavi tena mavi ya kuharisha. Hii itatugharimu sana kurudisha heshima. Na ninajua kabisa wakati mwingine yawezekana ilitoka order uwa, kwa nini uuwe?"- Amesema Askofu Musoganzila
Huyu askofu naye kilaza tu...
Walio uwa watatubu kwa MUNGU wao na Muda wao! askofu amevaa uungu wa kuwalaani (hapa ndo ukilaza wa askofu unaanzia)
walioiba na kuvunja na kuchoma mali, na wenyewe watubu wapi? wasije laaniwa? au hapa askofu umevaa miwani ya jua?
amri za MUNGU zipo kumi (kwa ukristo)..kama sijasahau usiibe na usiue ni kama zmetangulizana...we askofu wa chadema hukuiona amri ya kuiba?
AU kwa mungu wa huyu askofu kuna dhambi ndogo na kubwa?