TANZIA Askofu Mstaafu wa Jimbo la Njombe, Raymond Mwanyika afariki dunia

TANZIA Askofu Mstaafu wa Jimbo la Njombe, Raymond Mwanyika afariki dunia

barafu

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2013
Posts
6,739
Reaction score
32,880
Askofu mstaafu wa kanisa katoliki Jimbo la Njombe, Raymond Mwanyika amefariki dunia jana mkoani Njombe.

Askofu Mwanyika alizaliwa mwaka 1930 huko kijiji cha Uwemba-Njombe,baada ya makuzi na majiundo yake ya kiroho na kimwili alipata daraja takatifu la Upadre 11/10/1959;mnamo 16/01/1971 Baba Mtakatifu Paulo VI alimteua kuwa askofu wa Njombe,na 25/04/1971 alisimikwa kuwa Askofu rasmi wa Jimbo la Njombe.

June,8 2002 Askofu Mwanyika alipumzika na nafasi yake kuchukuliwa na Askofu Maluma.

Askofu Mwanyika amekuwa Padre kwa miaka 54 na Askofu kwa miaka 42,atakumbukwa kwa majitoleo yake ktk kuwahudumia watu wa Njombe bila kujali tofauti zao za kiimani,alikuwa mstari wa mbele ktk kuendeleza huduma za jamii kama hospitali na shule,huduma za maji na umeme ktk maeneo mengi ya Njombe,Makete mpaka Ludewa.

Anatarajiwa kuzikwa 29/10/2013 ndani ya kanisa katoliki la Njombe(Njombe Cathedral)....Bwana alitoa na Bwana ametwaa,jina lake lihimindiwe.

AMINA
 
askofu mstaafu wa kanisa katoliki jimbo la njombe, raymond mwanyika amefariki dunia jana mkoani njombe.
Askofu mwanyika alizaliwa mwaka 1930 huko kijiji cha uwemba-njombe,baada ya makuzi na majiundo yake ya kiroho na kimwili alipata daraja takatifu la upadre 11/10/1959;mnamo 16/01/1971 baba mtakatifu paulo vi alimteua kuwa askofu wa njombe,na 25/04/1971 alisimikwa kuwa askofu rasmi wa jimbo la njombe.
June,8 2002 askofu mwanyika alipumzika na nafasi yake kuchukuliwa na askofu maluma.askofu mwanyika amekuwa padre kwa miaka 54 na askofu kwa miaka 42,atakumbukwa kwa majitoleo yake ktk kuwahudumia watu wa njombe bila kujali tofauti zao za kiimani,alikuwa mstari mbele ktk kuendeleza huduma za jamii kam hispitali na shule,huduma za maji na umeme ktk maeneo mengi ya njombe,makete mpaka ludewa.
Anatarajiwa kuzikwa 29/10/2013 ndani ya kanisa katoliki la njombe(njombe cathedral)....bwana alitoa na bwana ametwaa,jina lake lihimindiwe..amina
asante kwa taarifa nimesikitika sana maana alikuwa ni mtu mwema na mpole sa na,amefanya mambo makubwa sana ya maendeleo,mpaka kuna wakati niliwahi kusema kama huyu askofu asiye kusanya kodi amefanya makubwa hivi je serikalia inashindwaje?nitajitahidi nihudhurie mazishi yake ingawa nipo mbali sana.mungu amhurumie na kumweka mahali pema peponi.amina.
 
Pumzika kwa amani baba Askofu...! Wewe Mbele sisi nyuma,

Raha ya milele umpe ee bwana!
 
Mungu ampuzishe mahali pema peponi, rekebisha kidogo hapo kwenye miaka ya uaskofu,sio 42 bali 31.
 
Pumuzika kwa amani baba Askofu, kumbukumbu yangu kwako ni siku uliyonipa Kipaimara.

Bwana ametoa na Bwana ametwaa, raha ya milele ikuangazie.
 
Poleni wafiwa Mungu awape nguvu ya kustahimili. Naomba kuuliza, ni kwanini wakatoliki wanazika maaskofu wao ndani ya makanisa? Akifa askofu kanisa linageuzwa kaburi, kwanini jamani? Kama Moshi kule naambiwa kuna maaskofu 3 wamezikwa ndani ya kanisa moja. Hali hii ikiendelea miongo mitatu kanisa linaweza kugeuka cemetery kabisa! Kuna sababu gani za kiimani kwa jambo hili, na je haziwezi kubadilishwa?
 
Mungu, utufanye kila tunapoona watu wanatutoka, tusihuzunike tu kwa vifo vyao, bali tukumbuke kuwa hapa tunapita, na kila mmoja kwa imani yake akukumbuke wewe uliye Muumba. RIP Askofu Mwanyika, hakika umeenda umeshiba siku zako nyingi. AMINA.
 
Pumzika kwa amani baba Askofu njia yetu ni moja

Sent from my kiberiti
 
RIP Askofu.

Pole David Mwanyika "Daz Baba" kwa kufiwa na Baba Mdogo/Mkubwa.
 
Back
Top Bottom