TANZIA Askofu Mstaafu wa Jimbo la Njombe, Raymond Mwanyika afariki dunia

RIP BABA. Kanikumbusha Njombe na marehemu Askofu Sangu wa Mbeya. RIP. Mungu awapokee mbinguni. Amen
 
R.I.P Baba Askofu Mwanyika.Hawa maaskofu wa zamani walifanya kazi kubwa ya kujenga shule na hospitali ambazo ndio zimekomboa watanzania wengi.Namkumbuka pia Askofu Sangu wa Mbeya, Msakila wa sumbawanga na wengineo.
 
Pumzika kwa amani baba Askofu R.Mwanyika.Kazi yako ya kumwakilisha Kristo umeifanya vyema.Mungu akuweke mahala pema peponi AMINA.
 
Raha ya Milele Umpe Ee Bwana na Mwanga wa Milele Umwangazie, Astarehe kwa Amani. Amina
 
Pumzika kwa amani Baba Askofu, Bwana alitoa, Bwana Ametwaa, Jina lake lihimidiwe
 
pumzika kwa amani askofu kipenzi cha watu wa njombe.....nakumbuka moja ya mahubiri yake ni wakati padri flani ameuawa kwa kuchomwa spoku akiwa, alisema kwamba "nagharamia sana kuwaandaa hawa vijana (mapadre)...kama mmewachoka mniambie niwapeleke kwa wanaohitaji...mimi sifyatui mapadre kama tofali...wanatoka kwenu....je mmenipa ili muwaue?" aliongea kwa hisia mpaka anatoa machozi....in fact machozi yalinitoka.... RIP baba.
 
Mungu ampuzishe mahali pema peponi, rekebisha kidogo hapo kwenye miaka ya uaskofu,sio 42 bali 31.
Donge, aliyetoa mada yuko sahihi kitakwimu. Kumbuka kwamba baada ya kustaafu, anaendelea kuwa na hadhi ya Uaskofu kamaAskofu mstaafu. Akiombwa na askofu aliye madarakani, anaweza hata kutoa daraja ya upadre (mwaka jana Askofu Mstaafu Mathias Isuja wa Dodoma alitoa daraja ya Upadre kule Morogoro). Nadhani utakuwa umeelewa
 
Setuba Noel, unapaswa tu kuuliza kwamba huu utamaduni umetoka wapi na kama unaweza kubadilishwa. Ukisema kwamba endapo huu utaratibu ukiendelea kwa miongo kadhaa makanisa yatageuka kuwa makaburi, unaonesha ulivyo na ufinyu wa kufikiria. Kumbuka kanisa katoliki lina umri wa miaka zaidi ya 2000. Kule Ulaya ambapo kanisa lilianza wamekuwa wanazika maaskofu makaburini tangu enzi hizo. Kama utafiti wako ungekuwa sahihi, makanisa kule yangeshageuka kuwa makaburi. Usikurupuke kuongea kitu, jaribu kufanya research kwanza
 

Poor we
 
Mwanzilishi wa jimbo katoliki la Njombe na askofu mstaafu wa jimbo hilo mhashamu askofu Raymond mwanyika amefariki dunia jana wakati akipatiwa matibabu katika hospital ya mji wa Njombe .

Wakili wa askofu wa jimbo katoliki la Njombe padri Justine sapula amesema kuwa mauti ya mhashamu askofu Mwanyika yanatokana na kupanuka kwa moyo, damu kushindwa kufanya kazi pamoja na umri wake.

Mhashamu askofu Mwanyika alizaliwa mwaka 1930 katika kata ya Uwemba mkoani Njombe na kubatizwa pamoja na kumuniyo ya kwanza april 8 mwaka 1939 kabla ya kupatiwa sacrament ya kipaimara October 9 mwaka 1940.

Alipata daraja takatifu la upadre October 11 mwaka 1959 kabla ya kupata daraja takatifu la uaskofu april 25 mwaka 1971 na kustaafu mwaka 2002 katika jimbo la Njombe kutokana na maradhi yalyokuwa yanamsumbua.
 
Raha ya milele umpe eeh Bwana, na mwanga wa milele umwangazie, apumzike kwa amani.
 
Raha ya milele umpe ee bwana na mwanga wa milele umwangazie,apumzike kwa Amani!
 
Mwanga wa bwana ukuangazie na upumzike kwa amani baba Askofu Mwanyika. Pole kwa wanaNjombe wote mliofikwa na msiba huu mzito.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…