Askofu Munga, aadhimisha ibada(Albadir) ya kulaani waliomvamia Tundu Lissu

figganigga

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
25,724
Reaction score
55,906
Askofu wa KKKT, Stephen Munga ameadhimisha ibada maalumu ya kulaani mashambulizi yaliyofanywa na ‘watu wasiojulika’ dhidi ya Tundu Lissu
62a9469751d1034dbd206e441ccd6570.jpg

KKKT NAO WAWASOMEA ‘ALBADIR’ WALIOMPIGA LISSU

NA OSCAR ASSENGA, TANGA

ASKOFU wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini- Mashariki, Dk. Stephen Munga ameadhimisha ibada maalumu ya kulaani mashambulizi yaliyofanywa na ‘watu wasiojulika’ dhidi Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu. RAI linaripoti.

Hatua hiyo imekuja ikiwa ni wiki chache zimepita baada ya baadhi ya viongozi wa dini ya kiislamu mkoani humo kusoma dua maalumu maarufu kama ‘Ibada ya Albadir’ kwa ajili ya watu hao wasiojulikana.

Akizungumza katika ibada hiyo iliyofanyika mjini Tanga hivi karibuni Askofu Munga yupo tayari kutengwa na kama akionekana ameegemea upande wowote kwani amani haina chama wala itikadi za kisiasa.

Alisema mtaji mkubwa wa watu wanaohangaika na maisha yao ni amani hivyo pale suala hilo linapotoweka hata mihangaiko yao inakuwa maradufu jambo ambalo linakwamisha fursa za kujiingizia kipato.

“Tanzania ni nchi yetu, nyumba yetu ambayo Mungu ametujalia tuishi lakini nyumba hiyo hivi sasa imeingia joka na amani hakuna tena zaidi ya kuishi kama wakiwa. Watanzania lazima watambue kuwa amani haina chanzo na bila kuangalia itikadi za kisiasa za CCM na Chadema kila mmoja anapaswa kuidumisha “ alisema.

Alisema matukio ya watu kuvamiwa kama ilivyotokea kwa Lissu na kupigwa risasi yamekuwa matukio ya kawaida kwa sababu amani imetoweka.

“Kuwepo kwa kadhia hiyo lazima watu tuongee kupitia kwa Mungu ili kuifanya nyumba iweze kuwa na amani ambayo ndio msingi mkubwa wa maendeleo. Hatuhitaji jambo lolote kwa Serikali au vyombo vya dola zaidi ya amani ndio maana tunalipa kodi, hawa watu wasiojulikana wasiokamatwa ni chanzo cha nyumba yetu kutokuwa na amani“ alisema.

Aidha, aliliomba Jeshi la Polisi kutumia weledi wake kuhakikisha hali ya usalama inarejea nchini ili watu waishi kwa amani kwa maendeleo ya Taifa.

“Lakini pia niwaambie tusicheze na Mungu wetu linapokuja hitaji kwa ushabiki wa aina yoyote ile kwani Tanzania tokea uchaguzi kuisha kumekuwa na kutokuelewana. Viongozi waliopo madarakani wanakazi kubwa ya kuliunganisha Taifa hili kwa kuwa umoja na mshikamano ndio chanzo cha kuwa na amani ambayo

ndio nguzo kuu ya mafanikio kwa nchi yoyote dunia.

“Tumekuwa na mivutano ya kisiasa ambayo imetufikisha hapa. Mivutano hii haijatutoka kwenye usingizi, visa na visasi vya uchaguzi inabidi tumuombe Mungu atuondolee hali hiyo kwani sio nzuri “ alisema.

Alisema kazi ya Rais ni kuunganisha Taifa hivyo lazima Serikali itoemwelekeo mmoja kwani hata huko kunyoosheana vidole sio jambo nzuri kwa mustakabali wa nchi.

“Lakini pia hatuna umoja, mgawanyiko ndio joka kubwa ambalo limeingia hapa nchini kwani hakuna uzalendo pasipokuwa na umoja ndani ya nchi ya namna hiyo hakuna amani.

“Watu wanasema Askofu hauogopi lakini kwa jambo ambalo linazungumzia suala la amani tuombe tukamwambie Mungu nchi iweze kubadilika kwani jambo hilo hata Yeremia alisema atalihubiri bila kuchoka“ alisema.

Anasema watu wanataka amani na umoja katika Taifa kwani Bunge linaweza kuzungumza mambo yake kama Bunge lakini pia tumemchagua Rais atuunganishe na mataifa na kuendelea amani iliyokuwepo “ alisema.
 
Askofu wa KKKT, Stephen Munga ameadhimisha ibada maalumu ya kulaani mashambulizi yaliyofanywa na ‘watu wasiojulika’ dhidi ya Tundu Lissu
62a9469751d1034dbd206e441ccd6570.jpg

KKKT NAO WAWASOMEA ‘ALBADIR’ WALIOMPIGA LISSU

NA OSCAR ASSENGA, TANGA

ASKOFU wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini- Mashariki, Dk. Stephen Munga ameadhimisha ibada maalumu ya kulaani mashambulizi yaliyofanywa na ‘watu wasiojulika’ dhidi Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu. RAI linaripoti.

Hatua hiyo imekuja ikiwa ni wiki chache zimepita baada ya baadhi ya viongozi wa dini ya kiislamu mkoani humo kusoma dua maalumu maarufu kama ‘Ibada ya Albadir’ kwa ajili ya watu hao wasiojulikana.

Akizungumza katika ibada hiyo iliyofanyika mjini Tanga hivi karibuni Askofu Munga yupo tayari kutengwa na kama

akionekana ameegemea upande wowote kwani amani haina chama wala itikadi za kisiasa.

Alisema mtaji mkubwa wa watu wanaohangaika na maisha yao ni amani hivyo pale suala hilo linapotoweka hata mihangaiko yao inakuwa maradufu jambo ambalo linakwamisha fursa za kujiingizia kipato.

“Tanzania ni nchi yetu, nyumba yetu ambayo Mungu ametujalia tuishi lakini nyumba hiyo hivi sasa imeingia joka na amani hakuna tena zaidi ya kuishi kama wakiwa. Watanzania lazima watambue kuwa amani haina chanzo na bila kuangalia itikadi za kisiasa za CCM na Chadema kila mmoja anapaswa kuidumisha “ alisema.

Alisema matukio ya watu kuvamiwa kama ilivyotokea kwa Lissu na kupigwa risasi yamekuwa matukio ya kawaida kwa sababu amani imetoweka.

“Kuwepo kwa kadhia hiyo lazima watu tuongee kupitia kwa Mungu ili kuifanya nyumba iweze kuwa na amani ambayo ndio msingi mkubwa wa maendeleo. Hatuhitaji jambo lolote kwa Serikali au vyombo vya dola zaidi ya amani ndio maana tunalipa kodi, hawa watu wasiojulikana wasiokamatwa ni chanzo cha nyumba yetu kutokuwa na amani“ alisema.

Aidha, aliliomba Jeshi la Polisi kutumia weledi wake kuhakikisha hali ya usalama inarejea nchini ili watu waishi kwa amani kwa maendeleo ya Taifa.

“Lakini pia niwaambie tusicheze na Mungu wetu linapokuja hitaji kwa ushabiki wa aina yoyote ile kwani Tanzania tokea uchaguzi kuisha kumekuwa na kutokuelewana. Viongozi waliopo madarakani wanakazi kubwa ya kuliunganisha Taifa hili kwa kuwa umoja na mshikamano ndio chanzo cha kuwa na amani ambayo

ndio nguzo kuu ya mafanikio kwa nchi yoyote dunia.

“Tumekuwa na mivutano ya kisiasa ambayo imetufikisha hapa. Mivutano hii haijatutoka kwenye usingizi, visa na visasi vya uchaguzi inabidi tumuombe Mungu atuondolee hali hiyo kwani sio nzuri “ alisema.

Alisema kazi ya Rais ni kuunganisha Taifa hivyo lazima Serikali itoemwelekeo mmoja kwani hata huko kunyoosheana vidole sio jambo nzuri kwa mustakabali wa nchi.

“Lakini pia hatuna umoja, mgawanyiko ndio joka kubwa ambalo limeingia hapa nchini kwani hakuna uzalendo pasipokuwa na umoja ndani ya nchi ya namna hiyo hakuna amani.

“Watu wanasema Askofu hauogopi lakini kwa jambo ambalo linazungumzia suala la amani tuombe tukamwambie Mungu nchi iweze kubadilika kwani jambo hilo hata Yeremia alisema atalihubiri bila kuchoka“ alisema.

Anasema watu wanataka amani na umoja katika Taifa kwani Bunge linaweza kuzungumza mambo yake kama Bunge lakini pia tumemchagua Rais atuunganishe na mataifa na kuendelea amani iliyokuwepo “ alisema.
We figganigga hilo neno la kishirikina 'albadir' liishie huko huko usililete kwenye Ukristo
Koma kabisa
 
Askofu Munga nakukubali sana. Hongera kwa kutumbusha juu ya amani ya nchi yetu na umoja wa kitaifa na kimataifa pamoja na mshikamano ambao ni asili yetu watanzania.

Hukifanana na hufanani na wale waliohongwa barabara za kwenda kwenye vilinge vyao vya kuwachuna wasiojitambua!
Wewe ni mchunga kondoo wa kweli na Mungu huyu tunayemwamini akusimamie na kukuongoza ili ukatulishe neno lake ambalo zao lake ni amani. Hufanani na mazedukayo na mafarisayo walioamua kutuchangisha zaka zetu na kufunga macho na midomo yao iliyojaa mikate michachu! Ukabarikiwe sana.
 
Bora askofu amekuwa mtumishi wa Kwanza kuliongelea jambo hili hadharani.
wewe ndio umekuwa wa kwanza kuuona huu uzi na si yeye kawa wakwanza kulitamka

wameshatamka maaskofu juu ya uvunjifu Amani ila kwa MB 5 ulizonazo hukuweza kuziona hapo awali.
 
Huyu askofu lazima atajibiwa na mkulu km alivyomjibu mstaafu anaewashwawashwa
 
Mleta mgawanyiko mkubwa hapa nchini ni yule anayedai kuwa yeye ndiye "Mzalendo" na wengine wote wenye mawazo tofauti na mtazamo wake ni "Wasaliti"
Mvurugaji wa amani yetu ni yule anayewafukuza watu wengine kazi wakiwa na taaluma zao kwa kisingizio cha kukosa vyeti vya Form IV, huku wapambe wanaotumika kuvuruga amani wanasifiwa hata kama majina yao ya elimu ni feki.
Nenda kwenye Mkutano wowote wa kitaifa ujionee, hasa wa kiserikali jinsi ubaguzi ulivyotamalaki. Ukiwa upinzani hata kama una haki ya kutambulishwa watajifanya vipofu ilimradi jina lako lisisike.
Imejitokeza nadharia ya kishetani kwamba kuna kitu kinaitwa "Vita ya Uchumi" ambayo usipofikiri kama wao basi umekaribisha "Watu wasiojulikana" mlangoni.
Kwamba sasa "Watu wasiojulikana" ndio wamekuwa watetezi wakubwa wa serikali ya Chama cha Mapinduzi ni jambo lililo bayana. Ukiwauripoti Polisi unaona dhahiri jinsi Polisi wanavyowagwaya.
Leo hii inasikitisha na kutia kinyaa unapokutana na kada wa CCM anayetamba bila lepe la aibu kuwa: "Apotezwe tu naye amezidi" Yaani CCM iliyokuwa tayari kujikosoa na kukosolewa, leo imekuwa chama kinacholea ukatili dhidi ya walio na hoja kinzani.
Chama kilicholeta kauli mbiu ya "Kushindana bila kupigana," leo kimeishiwa hoja na kubakiza vitisho vinavyotumiwa na magenge ya "Wapotezaji"
Kwa hakika CCM IMEIVURUGA MAMA TANZANIA KWA SIASA ZA CHUKI NA VISASI!!!
Mhe. Askofu ombeni sana, maana tumeingiliwa, si na joka tu, bali pia na "Wakana Mungu" wenye kiu ya damu za raia wenzao!!!!!!!
 
Acha kupotosha ,kkkt hakuna huo upuuzi wako
 
Mkuu uwe unaanzisha thread mara moja moja. Nimependa uandishi na hoja zako.
 
Back
Top Bottom