Mleta mgawanyiko mkubwa hapa nchini ni yule anayedai kuwa yeye ndiye "Mzalendo" na wengine wote wenye mawazo tofauti na mtazamo wake ni "Wasaliti"
Mvurugaji wa amani yetu ni yule anayewafukuza watu wengine kazi wakiwa na taaluma zao kwa kisingizio cha kukosa vyeti vya Form IV, huku wapambe wanaotumika kuvuruga amani wanasifiwa hata kama majina yao ya elimu ni feki.
Nenda kwenye Mkutano wowote wa kitaifa ujionee, hasa wa kiserikali jinsi ubaguzi ulivyotamalaki. Ukiwa upinzani hata kama una haki ya kutambulishwa watajifanya vipofu ilimradi jina lako lisisike.
Imejitokeza nadharia ya kishetani kwamba kuna kitu kinaitwa "Vita ya Uchumi" ambayo usipofikiri kama wao basi umekaribisha "Watu wasiojulikana" mlangoni.
Kwamba sasa "Watu wasiojulikana" ndio wamekuwa watetezi wakubwa wa serikali ya Chama cha Mapinduzi ni jambo lililo bayana. Ukiwauripoti Polisi unaona dhahiri jinsi Polisi wanavyowagwaya.
Leo hii inasikitisha na kutia kinyaa unapokutana na kada wa CCM anayetamba bila lepe la aibu kuwa: "Apotezwe tu naye amezidi" Yaani CCM iliyokuwa tayari kujikosoa na kukosolewa, leo imekuwa chama kinacholea ukatili dhidi ya walio na hoja kinzani.
Chama kilicholeta kauli mbiu ya "Kushindana bila kupigana," leo kimeishiwa hoja na kubakiza vitisho vinavyotumiwa na magenge ya "Wapotezaji"
Kwa hakika CCM IMEIVURUGA MAMA TANZANIA KWA SIASA ZA CHUKI NA VISASI!!!
Mhe. Askofu ombeni sana, maana tumeingiliwa, si na joka tu, bali pia na "Wakana Mungu" wenye kiu ya damu za raia wenzao!!!!!!!