Ileje
JF-Expert Member
- Dec 20, 2011
- 13,667
- 21,296
ASKOFU AJIBU HOJA ZA SIMBACHAWENE JUU YA DKT. NCHIMBI NA KATIBA MPYA!
Ndugu Watanzania!
Mbunge wa Jimbo la Kibakwe mkoani Dodoma na aliyekuwa Waziri Mwandamizi katika serikali ya Samia na Serikali ya Magufuli, Mhe. George Simbachawene kasikika akisema kuwa katiba ya Tanzania iko imara na haina matatizo sana.
Simbachawene katoa sababu tatu ambazo ni: kutuvusha Rais Magufuli alipofariki, kutuvusha salama katika chaguzi mbalimbali zilizofanya na kutuvusha wakati Makamu wa Rais Mhe Dkt Emmanuel Nchimbi alipojiuzulu. Sasa inatubidi kumjibu Mhe. Simbachawene ili afahamu kuwa Watanzania wote sio wajinga. Kwa muono wetu sisi, Mhe. Simbachawene katoa hoja hiyo ikiwa na lengo la kuwapumbaza Watanzania ambao wanataka katiba mpya, pia ni kutaka kuipooza hoja ya Dkt. Nchimbi ya kuwataka Watanzania kupambania katiba mpya.
Mosi, Mhe. Simbachawene hawezi kuijua zaidi katiba yetu kumzidi Hayati Mwalimu Julius K. Nyerere ambaye kimsingi ndiye aliyeiandika na alijua makusudi ya kuiandika. Wakati anatoka madarakani, Mwalimu Nyerere alisema wazi ya kuwa katiba yetu ilikuwa na mapungufu sana na ilimpata dikiteta, wote twafwa! Kwa maneno mengine, Nyerere alisema kuwa katiba yetu ni ya kidikiteta. Hivyo kwa Mhe. Simbachawene kusifia katiba yetu anatueleza kuwa serikali ya CCM ni ya kidikiteta na ndio maana inaipenda hiyo katiba na ndio sababu haitaki ibadilishwe.
Pili, Simbachawene hawezi kuwa na utashi wa kuelewa zaidi kumzidi Kikwete na serikali yake yote ambao waliridhia kuundwa Tume ya Jaji Warioba kutafuta maoni ya wananchi kuhusu katiba yetu. Hakuna mahali ambapo Ripoti ya Tume hiyo ilisema kuwa katiba yetu inafaa.
Tatu, Simbachawene hawezi kuwa na utashi wa kuelewa zaidi ya Marais Mkapa na Mwinyi ambao waliwahi kuunda Tume kuhusu kupata maoni ya Katiba yetu. Ripoti za Tume zote tatu - Tume ya Nyalali, Ripoti ya Tume ya Bomani na Ripoti ya Tume ya Kisanga; hakuna hata moja iliyokuja na mapendekezo kuwa katiba yetu ni nzuri na iko imara. Kwa ujumla, ripoti zote zilipendekeza mabadiliko makubwa ya katiba.
Tatu, hoja ya Simbachawene kuwa katiba yetu ilitupitisha wakati wa kifo cha Rais Magufuli ni kwa sababu ya ubora na uimara wa katiba hii ni hoja iliyopotoshwa sana. Ukweli ni kuwa, tayari katiba ilishachezewa mara baada ya Magufuli kufariki dunia. Ndio maana hakuna Mtanzania anayejua kwa hakika Magufuli alifariki lini, siku gani, tarehe gani na saa ngapi!
Kilichotuvusha haikuwa ubora wa katiba, bali ni uadilifu wa Jenerali Mabeyo ambaye aliwazuia waliotaka kufanya yao. Kwa maneno mengine, Jeshi ndilo lililotuvusha salama kipindi kile na wala sio ubora na uimara wa katiba. Kwa hiyo, katiba inayotegemea utashi na uadilifu wa CDF (Mkuu wa Majeshi), hiyo ina udhaifu mkubwa.
Na kama Mabeyo asingesimama imara, Samia asingelikuwa Rais baada ya Magufuli.
Huenda Mhe. Simbachawene huenda hajui au anafanya makusudi anaposema ya kuwa nchi yetu haikupata misukosuko baada ya kifo cha Magufuli kulinganisha na nchi nyingine. Mhe. Simbachawene hajatoa mfano hata mmoja wa nchi za Kiafrika ambazo zilipata msukosuko baada ya Rais kufia kitini kama Magufuli. Sisi tunampa mfano wa Kenya, Malawi na Zambia ambazo ndio majirani zetu. Wakati Marais wao walipokufa wakiwa kitini, nchi hizo pia zilipita salama bila misukosuko. Lakini na Kenya pia kupita salama baada ya Kenyatta kufia kitini, hawakuacha kudai katiba mpya. Kupita salama Rais anapofariki akiwa kitini hakuhusiani na uzuri wa katiba kwani hata nchi za kidikiteta pia Marais hufia vitini na hubadilisha uongozi.
Kuhusu katiba kutupitisha salama nyakati za chaguzi hiyo nayo ni hoja ya uwongo. Katika kila chaguzi zetu kunakuwa na uporaji wa kura, uporaji wa uchaguzi na mauaji ya watu mamia kwa mamia. Kinachotuliza nchi katika nyakati zote hizo, sio katiba bali na majeshi ambayo ni sehemu ya CCM. Siku majeshi yakiacha kuwa upande wa watawala hali inaweza kuwa tofauti.
Hakuna mtu mwenye akili tamamu anayeweza kuisifia katiba yetu akitazama matukio haya ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2019, Uchaguzi Mkuu wa 2020, Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa 2024 na Uchaguzi Mkuu wa 2025. Mauaji ya mamia au maelefu ya watu kwa ujumla wote katika chaguzi hizo ni ishara ya ubovu, udhaifu, ubaya na upungufu uliomo katika katiba yetu.
Kuhusu katiba kutupitisha kipindi hiki baada ya Makamu wa Rais Dkt. Emmanuel Nchimbi pia kusemekana kujiuzulu na kupatikana mwingine kwa amani ni hoja ya kiinimacho. Hadi wakati huu kuna minong'ono ndani ya CCM na ndani ya serikali ya CCM kuwa Nchimbi hakujiuzulu ila kalazimishwa kujiuzulu. Minong'ono kuwa Nchimbi yuko chini ya ulinzi au kafichwa iko imeenea kila mahali. Kama kweli Dkt. Nchimbi alijiuzulu kwa hiari, ni kwa nini hakuonekana siku ya uapisho wa Makamu wa Rais mpya?
Kama kweli katiba yetu iko imara, ni kwa nini ile barua ya kujiuzulu kwa Nchimbi itaje tarehe 4 Septemba kuwa ndio siku ya kujiuzulu kwake rasmi lakini uapisho wa Makamu wa Rais mpya ufanyike wiki moja kabla? Kwa mantiki hiyo, ni kuwa hadi sasa tuna Makamu wa Rais wawili, pengine ndio sababu ya kuendelea kumficha Nchimbi ili wamuachie baada ya hiyo tarehe 4 Septemba 2026.
Kwa ufupi hayo ndio majibu yetu kwa hoja ya Mhe. George Simbachawene.
Je, nini kimekushangaza? Je, nini maoni yako?
Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Itunge, Dar es Salaam; 31 Agosti 2026; Saa 6:10 usiku