PostGE2025 Askofu Mwamakula apendekeza Ibada Maalumu Kwa waliouwa Oktoba 29

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Inside10

Platinum Member
Joined
May 20, 2011
Posts
34,776
Reaction score
42,933
Askofu wa Kanisa la Uamsho la Moravian Tanzania, Emmaus Mwamakula, amependekeza kuwa kila mkoa ambako mauaji yalifanyika, Oktoba 29, 30 na 31 mwaka hii, ipangwe siku ambayo watu watakusanyika uwanjani kufanya sala za wafu na kuweka mashada ya maua.
‎
‎Askofu huyo ameandika hayo Desemba 15, 2025, kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Facebook akipendekeza Desemba 29, 2025 iwe siku ya kufanya tukio hilo, na kwamba lisiwe tukio la kiserikali, lakini viongozi wa kiserikali pia wahudhurie.
‎
‎Amesema katika tukio hilo la kumbukumbu, "Viongozi wa dini wafanye sala za wafu, majina ya watu hawajaonekana, wanaosadikiwa kuwa waliuawa katika mauaji hayo yaorojeshwe kwa kila wilaya au mkoa na yatumike hayo kutajwa katika sala kulingana na imani za dini zao".
‎
‎Ameongeza kuwa baada ya utaratibu huo wa kitaifa kufanyika, ndugu walioondokewa na wapendwa wao waende katika vijiji na mitaa yao na katika familia zao ili kumaliza taratibu za msiba. Amesema kwa kufanya hivyo waliopoteza maisha Oktoba 29, watakuwa wameenziwa na kama taifa "tutakuwa tumetimiza wajibu unaopasa kwa marehemu".
‎
‎"kwani kwa mujibu wa mila, desturi na tamaduni zetu, lazima kuwe na utaratibu wa kuhitimisha maisha ya mtu au marehemu hapa duniani", ameandika Askofu, Mwamakula.
‎
‎Aidha amesema hatua hiyo itatoa nafasi kwa ndugu wa waliopoteza maisha kuwaomboleza ndugu zao kwa uwazi kuliko sasa wakati wako kwenye majonzi ya kimya. Hata hivyo, Mwamakula ameipendekeza siku ya tarehe 29 Desemba 2025 iwe siku ya kufanya maombolezo hayo kwani itakuwa imetimia miezi 2 kamili baada ya mauaji hayo yafanyike.
1765794095137.png
 
Sisi tunataka itangazwe siku ya kulipa kisasi kila familia ya askari polisi tuone imefunga turubai ndiyo tutakwenda sawa.
 
Askofu wa mtandaoni, rc walishaanda Misa za kukumbuka waliofariki yeye ndio Leo anakumbuka.
 
Askofu wa Kanisa la Uamsho la Moravian Tanzania, Emmaus Mwamakula, amependekeza kuwa kila mkoa ambako mauaji yalifanyika, Oktoba 29, 30 na 31 mwaka hii, ipangwe siku ambayo watu watakusanyika uwanjani kufanya sala za wafu na kuweka mashada ya maua.
‎
‎Askofu huyo ameandika hayo Desemba 15, 2025, kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Facebook akipendekeza Desemba 29, 2025 iwe siku ya kufanya tukio hilo, na kwamba lisiwe tukio la kiserikali, lakini viongozi wa kiserikali pia wahudhurie.
‎
‎Amesema katika tukio hilo la kumbukumbu, "Viongozi wa dini wafanye sala za wafu, majina ya watu hawajaonekana, wanaosadikiwa kuwa waliuawa katika mauaji hayo yaorojeshwe kwa kila wilaya au mkoa na yatumike hayo kutajwa katika sala kulingana na imani za dini zao".
‎
‎Ameongeza kuwa baada ya utaratibu huo wa kitaifa kufanyika, ndugu walioondokewa na wapendwa wao waende katika vijiji na mitaa yao na katika familia zao ili kumaliza taratibu za msiba. Amesema kwa kufanya hivyo waliopoteza maisha Oktoba 29, watakuwa wameenziwa na kama taifa "tutakuwa tumetimiza wajibu unaopasa kwa marehemu".
‎
‎"kwani kwa mujibu wa mila, desturi na tamaduni zetu, lazima kuwe na utaratibu wa kuhitimisha maisha ya mtu au marehemu hapa duniani", ameandika Askofu, Mwamakula.
‎
‎Aidha amesema hatua hiyo itatoa nafasi kwa ndugu wa waliopoteza maisha kuwaomboleza ndugu zao kwa uwazi kuliko sasa wakati wako kwenye majonzi ya kimya. Hata hivyo, Mwamakula ameipendekeza siku ya tarehe 29 Desemba 2025 iwe siku ya kufanya maombolezo hayo kwani itakuwa imetimia miezi 2 kamili baada ya mauaji hayo yafanyike.
View attachment 3515776
Huyu siyo Askofu wa kanisa lolote kwa vile sijawahi kuona mahali anafanyia ibada wala waumini wa kanisa lake. Huyu ni teja tu wa siasa za CHADEMA maana 24/7 ana push agenda za CHADEMA. Tapeli wa makanzu ya kanisani toka Ipinda Kyela
 
Kamtekeni ni mwepesi sana ana kilo 56 tu.
 
Back
Top Bottom